1. Katekwa na Polisi ili kuwatisha waropokaji. Polisi wamepelekwa mahakamani. Wamekana na kushinda kesi. Wako huru. Hawajamteka.

2. Katekwa na Chadema ili kuwasingizia polisi. Siku zimekuwa nyingi; polisi hawaogopi kusingiziwa. Umma unaamini ni polisi. Chadema wakimpoteza Soka moja kwa moja, itakula kwa polisi. Polisi wakishindwa kumwokoa Soka toka mikononi mwa Chadema, itakula kwao. Mpira uko eneo la goli la Polisi.

3. Ametekwa na wajanja wanaotumia jina la Polisi (Rogues). Kutokamatwa kwao ni hatari kwa kila mtu na kila taasisi. Wakiishazoea watateka viongozi wetu na kusababisha hali ya hatari. Watekaji wasiokamatika ni sawa na silaha moja kupotea kutoka ghala la silaha. Polisi wako lawamani katika nadharia hii.

4. Soka na wenzake wamejiteka ili polisi na chama cha watani wa jadi walaumiwe. Kazi mojawapo ya polisi ni kufichua waliojiteka. Kwa kujiteka ukafanikiwa kutokamatwa, wanaolaumiwa ni polisi. Sifa moja ya Polisi na serikali ni kuwa na MKONO MREFU. Nani kaukata ukawa mfupi usimkamate Soka aliyejiteka?

5. Soka ametekwa na chama cha watani wa jadi wa Chadema kwa sababu Soka ni Chadema. Kwa kuwa kuna mzimu “unawaroposha” wanachama wa chama hicho kukiri utekaji; Polisi wana ushahidi wa mazingira kuwatumia watopokaji kuisaidia polisi. Asipopatikana si kosa la chama kilichoteka. Ni kosa la taasisi inayojihusisha na kuzuia utekaji. Bado Polisi hawajachomoka. Niwasaidieje?

Mpaka hapa, naweza kusema, aliyemteka Soka na wenzake, ameiteka polisi maana nadharia 4 kati ya 5 zinagota kwa polisi. Nani aikomboe polisi kutoka mikono ya watekaji?

Tumewahi kuuona mkono mrefu wa Polisi ukiwa kazini. Majuzi tu, ndani ya masaa 24, waliomuua Binti Asiimwe mwenye ualbino walikamatwa.

Tumesikia habari za mganga wa kienyeji aliyezika watu. Tunaogopa tusijeambiwa akina Soka wako humo. Kwamba walienda kupiga ramli chonganishi
 
Hao wanaotekwa ni watu wapogo tu, hawana, serikali, hawana silaha, hawana pesa, wana visimu tu.

Please, Mheshimiwa mbona unaacha mambo haya yaharibu historia yetu, free them.
 
Aubiri dini aache siasa!,...
 
Hao wanaotekwa ni watu wapogo tu, hawana, serikali, hawana silaha, hawana pesa, wana visimu tu.

Please, Mheshimiwa mbona unaacha mambo haya yaharibu historia yetu, free them.
Magu alikamata na kusweka lupango, aliteka kidogo sana! Na hakuchagua papa, kambale na sharubu zake ama perege na vidagaa....
This time around mapapa na makambale yako mikono salama kabisa....🙌🏿🙌🏿🙌🏿🏃🏿🏃🏿🏃🏿🏃🏿😭😭😭
 
e tuna jela za siri nje ya mfumo Tanganyika? Je tuna vyumba vya siri Tanganyika visivyo rasmi? Je tuna watesaji na wauaji wenye mafunzo rasmi lakini nje ya mfumo? Je ni Watanganyika?
Jibu ni NDIYO. Utawala huu umetisha, mwanamke anakuwa katili mithiri ya Idd Amin na Hitletr!
 
Kwasababu hawajulikani, basi hawa watakuwa ni mashetani wenye umbo la binadamu kwani wameshindikana kupatikanika.

Hata hivyo, wacha tuone hawa mashetani kama wataendelea kuteka na kuua ili tujue sasa tunafanyaje baada ya haya yaliyotokea leo.
 
Je waliopotea ndio basi mkuu wangu?
 
Kwasababu hawajulikani, basi hawa watakuwa ni mashetani wenye umbo la binadamu kwani wameshindikana kupatikanika.

Hata hivyo, wacha tuone hawa mashetani kama wataendelea kuteka na kuua ili tujue sasa tunafanyaje baada ya haya yaliyotokea leo.
Hakuna mamlaka duniani utaipanda kichwani ikuache, hata anaejiita baba wa demokrasia anaitawala dunia kwa kumwaga dam za watu.

Chadema wanapaswa kuheshimu mamlaka.
 
Hakuna mamlaka duniani utaipanda kichwani ikuache, hata anaejiita baba wa demokrasia anaitawala dunia kwa kumwaga dam za watu.

Chadema wanapaswa kuheshimu mamlaka.
Watekaji waheshimiwe ili waendelee kuteka?
 
Hakuna mamlaka duniani utaipanda kichwani ikuache, hata anaejiita baba wa demokrasia anaitawala dunia kwa kumwaga dam za watu.

Chadema wanapaswa kuheshimu mamlaka.
Ndo useme hao baba wa demokrasia ambao wanaweza wakaacha kuwakamata watu wanaofanya utekaji na mauaji.
Kwa akili yako,unadhani Mange Kimambi angekua hapa,angeachwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…