Hiki kisa cha Mordekai (myahudi) na (Hamani (muajemi/Iran) huwa kina somo zuri sana kuhusu hii vita ya sasa ya Iran na Israel. Hamani alikuwa na chuki na Mordekai na akataka kuwaua wayahudi wote mwisho akaishia kuuliwa yeye na washirika wake. Kama ilivyo leo akina Ayatollah wakitaka kuua wayahudi wote. Kwa ufupi soma haya hapa nimekuwekea
13 Bali haya yote yanifaa nini, pindi nimwonapo yule Mordekai, Myahudi, ameketi mlangoni pa mfalme?
Esta 5:13
14 Basi Zereshi mkewe (mke wa Hamani) akamwambia, na rafiki zake wote, Na ufanyizwe mti wa mikono hamsini urefu wake, na kesho asubuhi useme na mfalme ili Mordekai atundikwe juu yake; ndipo utakapoingia kwa kicheko pamoja na mfalme karamuni. Basi neno likampendeza Hamani, akaufanyiza ule mti.
Esta 5:14
13 Basi Hamani akawasimulia Zereshi mkewe na rafiki zake wote kila neno lililompata. Kisha watu wake wenye hekima na Zereshi mkewe wakamwambia, Ikiwa huyu Mordekai, ambaye umeanza kuanguka mbele yake, ni wa uzao wa Wayahudi, wewe hutamweza, bali kuanguka utaanguka mbele yake.
Esta 6:13
9 Ndipo aliposema Harbona, msimamizi-wa-nyumba mmojawapo wa wale waliohudhuria mbele ya mfalme, Tazama, basi, mti wa mikono hamsini urefu wake, Hamani aliomwekea tayari Mordekai, ambaye alinena vema kwa ajili ya mfalme, upo umesimamishwa nyumbani kwa Hamani. Mfalme akasema, Mtundikeni juu yake.
Esta 7:9
My Take:
Ikiwa Iran amechagua kuifuta Israel na kupigana nayo. Ni lazima ataanguka tu. Utawala wa akina AYATOLA unaangamia na umefika mwisho.