SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

mkuu Moisemusajiografii hizo ndege atazipitisha anga ipi maana kutoka iran hadi israel unapita nchi tatu hapo kati Iraq,Syria na Jordan ndio uingie israel na hizo nchi kuna base kibao za US,France na UK pamoja na meli vita huko baharini na hizo base ndio zinatumika kutungua ndrone na missiles za iran zisifike israel na pia hizo base za US france na UK hasa Iraq ndizo israel anazitumia kupiga hapo iran..ndiomaana unaona israel inajiamini kurusha ndege zake kushambulia sababu anaamini wa kumkinga mashambulizi au kupunguza madhara wapo tayari kumsaidia hivyo ana jeuri..ila israel peke yake hana ubavu wa kutamba middle east kama anavyofabya sasa..hivyo iran kurusha ndege vita kwenda israel ni ngumu mno labda aanze kuwafagia kwanza hizo base za US ,France na UK hapo middle east njia iwe nyeupe maana hawa ndio kikwazo kikubwa na wanampunguza nguvu sana kuitia adabu israel na ndzo zinampa kiburi israel kuwapiga wenzie kutokea karibu hivyo maangamizi anayofanya ni makubwa na yaliyojaa sifa..yeye iran anapiga tokea km 2000 parefu mno na hizo base za US France na UK zinazompunguza nguvu iran...mimi nawashangaa sana wanaoibeza na kuidharau Iran wanaopigana na nchi tano hapo kati hadi kufikia target yake sio jambo la kubeza sema wengi humu tunajitoa ufahamu tu licha ya kuyajua yote hayo..vipi kama Israel na Iran wangeachiwa uwanja wenyewe bila hao washirika kina US France na UK mnafikiri nini kingetokea ili tupate mbabe wa haki bila kubebwa.
 
Uzuri hata kwa Hezbollah na Hamas ilianza hivi hivi baada ya wiki tukaongea mengine. Wacha tuone
Acha kubadilisha maneno siku ya kwanza ya shambulizi la Israel mlidai mifumo yote ya ulinzi na kurushia makombora ya Iran imeharibiwa haiwezi kujibu au sio nyinyi?
Tukiacha ushabiki Iran ilipigwa pigo la kushutukiza na lisilo tarajiwa kabisa hivyo ilikuwa ni razima wajipange kwanza ndo waanze kufikiria mengine.
Israel ilipigwa ambush ya kushutukiza na hamas lakini iliichukua siku 2 kuajipanga na kuanza kujibu mapigo,ina maana Hamas ingekuwa ni jeshi kamili lenye miundo mbinu na silaha zinazo hitajika wenda wangeiteka mpaka Jerusalem ndani ya mda mfupi.
Uliliona Shambulizi la Ukraine kwa Urusi kwenye jimbo la Kursk iliichukua wiki 2 kuanza kujibu mapigo ya kuwarudisha nyuma wanajeshi wa Ukraine.
Hii vita ni ngumu sana kwa pande zote na ndio maana jana Israel imeiomba Marekani hiingilie kati Marekani ikakataa.
 
Hotuba yake ndefu na yenye masikitiko makubwa aliyoitoa kuhusu birthday ya Trump. Ametumia muda mwingi kulalamika, na kujitilisha huruma ili Marekani, washirika wake na jumuiya nzima ya kimataifa waongeze juhudi za kumsaidia kuilinda Israel kutokana na kimbunga kikubwa cha makombora yalioshindwa kuzuiliwa na mitambo yao yote ya kuzuia makombora.

Jordan imejitahidi kufunga anga lake ili kuzuia vyuma visipite, lakini wapi wamechemsha na kujificha pasipojulikana, kuhofia mzigo usipotee njia na kitwanga ikulu ya mfalme wao.

Halikadhalika Marekani, UK, Ufaransa na wengineo wanashindwa kujua wazuie juu au chini. Maana mitambo yao ya kuzuia makombora inaonekana mdebwedo tu mbele ya vyuma vya waajemi.

Mpaka sasa anaeomba msaada wa kijeshi kutoka nje ni Israel ambayo haina vikwazo vyovyote vya kutengeneza, kupewa wala kununua silaha. Iran haijaomba usaidizi kutoka kwa yoyote, maana game ni dogo mno, watalimaliza wenyewe kimya kimya.

Mi nafikiri Netanyahu angeacha kulalamika kuhusu kinachoendelea nchini kwake, bali aendelee nacho mwenyewe kile alichokianzisha.

Inamaana Netanyahu alipoanza kuomba chai, hakujua kwamba huko mbeleni utamuunguza kama sio kumbabua kabisa!
Btw: Vita sio nzuri ni bora Mungu aingilie kati ili kunusuru vifo na uharibifu zaidi.
 
Siogopi kitu najua IDF wako Iran wanafanya kazi yao maana anga yote ni yao, na wanapiga sehemu nyeti tu, kila wanapowagusa panauma🤌
ADS ya Iran inajitahidi kuzuia mashambulizi na ku minimize.
Athari sio kubwa kama kipindi cha mwanzo ama kama siku ya kwanza.
Ila Israel inatifuka tifuka vibaya sana.
Ikiendelea hivi wiki tu sidhani kama Kuna kitakachosimama Israel.
 
Inavyoonekana Iran hajawekeza sana kwenye ndege vita.

Anajua adui anayedili nae yuko vizuri kwenye AD akisema apeleke ndege au helicopter zikashambulie atakula hasara.

Yeye kawekeza sana kwenye drones na makombora ya masafa marefu anajua akiyatumia yatakuwa effective kuliko kupeleka ndege vita.
Siyo kweli bali Israel iko huru kutumia anga la nchi jirani kama Iraq, Syria na Jordan wakati Iran hawana huo uhuru ndio maana Makombora anayotumwa mengine yanatunguliwa Hapo Jordan na Syria yakiwa njiani. Laiti kama Iran ingekuwa na uhuru kama wa Israel ndege za kijeshi zingeshafika Israel.
 
Jamani sasa inatosha.
IRAN IKUBALI TU KUKAA MEZANI MIZOZO IISHE.
MAAFA YAMEKUA MENGI SANA AISEE HII INATOSHA SASA.
Hata uislam hauko hivi Iran inavuka mipaka.
Sema we jamaa mnafiki kinoma 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom