Hotuba yake ndefu na yenye masikitiko makubwa aliyoitoa kuhusu birthday ya Trump. Ametumia muda mwingi kulalamika, na kujitilisha huruma ili Marekani, washirika wake na jumuiya nzima ya kimataifa waongeze juhudi za kumsaidia kuilinda Israel kutokana na kimbunga kikubwa cha makombora yalioshindwa kuzuiliwa na mitambo yao yote ya kuzuia makombora.
Jordan imejitahidi kufunga anga lake ili kuzuia vyuma visipite, lakini wapi wamechemsha na kujificha pasipojulikana, kuhofia mzigo usipotee njia na kitwanga ikulu ya mfalme wao.
Halikadhalika Marekani, UK, Ufaransa na wengineo wanashindwa kujua wazuie juu au chini. Maana mitambo yao ya kuzuia makombora inaonekana mdebwedo tu mbele ya vyuma vya waajemi.
Mpaka sasa anaeomba msaada wa kijeshi kutoka nje ni Israel ambayo haina vikwazo vyovyote vya kutengeneza, kupewa wala kununua silaha. Iran haijaomba usaidizi kutoka kwa yoyote, maana game ni dogo mno, watalimaliza wenyewe kimya kimya.
Mi nafikiri Netanyahu angeacha kulalamika kuhusu kinachoendelea nchini kwake, bali aendelee nacho mwenyewe kile alichokianzisha.
Inamaana Netanyahu alipoanza kuomba chai, hakujua kwamba huko mbeleni utamuunguza kama sio kumbabua kabisa!
Btw: Vita sio nzuri ni bora Mungu aingilie kati ili kunusuru vifo na uharibifu zaidi.