SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Muda huu waziri wa ulinzi wa Israel anasema Ayat Khamenei hapaswi tena kuishi.
Khamenei na Iran waongeze ulinzi, Israel wameamua watamuua. Tusubiri

View: https://x.com/clashreport/status/1935633794469445783?t=iIoDeOKocWXmcilcZwHMEw&s=19
Khamenei akiuawa aisee😂😂😂😂 Israel nahisi itaonewa huruma dunia nzima.
Maana shia hadi wa Yemen na mataifa mengine watajiunga hiyo vita.
Mashia kiitikadi Amiri wao ni mfanano na Hussein.
Vita itageuka ya kidini aisee Israel asithubutu.
 
Kusema Israel ipo taabani hii ni chumvi umeweka mkuu. Israel haipo taabani

Vita ipo kwenye early stage, wacha washambuliane baada ya muda kuna mmoja ataelemewa na wala hauitakua siri wote tutaona
 
Kama akili alizonazo Iran ndizo hizi mlizonazo basi atapigwa so muda,
Una uhakika satellite zimeonyesha facilities zote za nuclear zipo salama ukiacha ya fordow
 
Siamini sana hizi mambo, washirika wengi hupotea hasa Hawa ambao hawapo backed na superpowers. Tusubiri
 
Mkuu hauwezi kuzuia surface to surface missile labda uharibu launcher zote zilizopo aridhini

Kilichotokea Gaza ni kwamba Israel ilihakikisha inaharibu launcher kuondoa uwezo wa kurusha hizo roketi...... na hichi ndio kitu Israel inajaribu kufanya pale Iran

Inaposemwa anga la Iran kivita limetawaliwa na Israel ina maanisha kwamba kwa kiasi kikubwa mifumo ya kiulinzi ya Iran imeharibiwa na kufanya Israel kulitumia anga itakavyo tena kwa kutumia ndege

Missile za Iran zitaendelea kurushwa as long as missile launcher zikiwepo.....
 
KITU Kipya ninapaa. Kinaondoka KWA mbwembwe kali sana. Ayatollah tushakushukuru KWA kuonyesha uwezo, Sasa unazidi hizi ni sifa. Kwa bahati mbaya picha zinachukuliwa Iran kwenye lengo ni kosa la kijeshi kulipiga picha hata likiwa linapambana na iron dome/David Sling / Allow na Thaad KWA mkupuo
 
Hawana cha kufanya kwanza nchi kama uae, quatar na nyingine zilizoendelea haziwezi hatarisha miundombinu ambayo wamejenga kwa miaka mingi kisa ujinga wa Iran, tena zinaweza toa msaada kupambana na Utawala wa Iran hutaamin
 
Waisrael huwa ni watata na wabishi sana, hivyo naona kabisa hauitakua rahisi kwa Iran. Kwa nature ya waisrael walivyo, watatumia kila aina ya njia kushinda. Huwa hawakubaligi kushindwa. Ngoja tusubiri, maana hata wairan nao ni wabishi mno
2006 walikubali wenyewe kushindwa.
Ya 2006 yanajirudia.
 
Daaaah!
Ona hata aibu basi.

Haya ni mavi yako unayafyatua kulinda anga la Iran!?
Hiyo ni jana usiku.


View: https://x.com/BRICSinfo/status/1935220278407135668
Mkuu japokua, sikuchangii bando wala siwezi kukupangia chochote cha kupost au kukomenti humu jf. Ila ni vizuri tu ungempotezea huyo jamaa, Usihangaike kumwelewesha mtu mwenye bichwa ka fuvu la dagaa.

Nimeamini, Iran 🇮🇷 wana air defense system nzuri sana yaani zina intercept kama zinazima moto. Njoo sasa kwa zile za fake Jewish ni vituko.
 
Jamaa ye anaelewa anga kutawaliwa hata kunguru wasiruke angani
 
Wengi wanashindwa kuelewa hili na hasa pro Iran.
Fikiria Leo Kuna mmoja anasema ndege za Israel zinashambulia zikiwa Iraq na sio ndani ya Iran. Hapo ndio kazi ilipo kwa watu walioamua kuwa washabiki
 
Kusema Israel ipo taabani hii ni chumvi umeweka mkuu. Israel haipo taabani

Vita ipo kwenye early stage, wacha washambuliane baada ya muda kuna mmoja ataelemewa na wala hauitakua siri wote tutaona
Mkuu ubishe usibishe Israel ipo taabani.
Kitendo hadi cha raia kuanza kukimbia nchi hiyo inaonesha Israel iko taabani.
Vita ya Hamas Israel walikua bado wako imara ndio maana raia walioamua kuondoka ni wachache.
Ila vita hii ya Iran hakuna sehemu salama Israel kiasi malaki ya raia wanahama nchi.
Tubishe tusibishe Israel iko taabani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…