SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Usiku wa leo umethibitisha tena kuwa Israel Air Defense System si lolote si chochote.

Iron Dome na THAAD zimetepeta badala ya kuintercept missiles za Iran ndio kwanza Iron Dome na THAAD zinaachia njia vinu vishuke

Hizi missiles za Iran zimepewa jina Shahed Haj Qassem with a range of 1000 miles

Hapa Marekani na washirika wake wakajipange tena kuja na mifumo itakayoweza kuzuia hypersonic missiles za Iran

Iran iendelee na hii consistency Wayahudi lazima wakae.

Myahudi asipewe muda wa kuvuta pumzi iwe ni vinu juu ya vinu

​
View attachment 3369143
If you can't beat them join them
Sema we jamaa mtetea china na mpinga USA, muda mwingine uwe unaongea facts upunguze ushabiki kama umetazama video kwa yale makombora Iran alirusha isingekuwa iron dome si Israel ingekuwa kifusi
 
Meya wa Israel: Nimeona mengi, lakini mashambulizi yaliyofanywa na Iran sijawahi kuyaona



[https://media]

Meya wa mji wa Israel wa Rishon Letzion wa kusini mwa Tel Aviv ameeleza kupigwa mshangao na kushtushwa na kiwango kikubwa cha uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya makombora ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema: Sijawahi kuona uharibifu mkubwa kama huu.

Leo Jumamosi, shirika la habari la IRNA limenukuu duru za habari za Kizayuni zikitangaza kuwa, meya wa mji wa Rishon Letzion ulioko kusini mwa Tel Aviv alisema jana Ijumaa kwa njia ya video kwamba: "Hii ni siku ngumu na yenye uchungu sana kwetu. Nilikuwa nimeona vitu vingi sana lakini sijawahi kuona uharibifu mkubwa kama huuu; matukio haya yanauma sana."

Licha ya kwamba utawala wa Kizayuni unachuja mno habari na unamtia mbaroni mtu yeyote anayepiga picha athari za mashambulizi ya Iran, lakini pamoja na hayo jana Israel ilikiri kwamba katika siku ya kwanza ya mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran, Wazayuni 80 wameangamizwa na kujeruhiwa huku hali ya baadhi ya majeruhi ikiwa mbaya sana.

Jana usiku vyombo vya habari vya Kizayuni viliripoti kuanza wimbi la tano la mashambulizi ya makombora ya Iran na kutangaza kuwa, wimbi la tano la makombora ya Iran limepiga maeneo yote ya Israel.

Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti kuwa, wimbi la tano la makombora ya Iran limepiga maeneo ya Tiberias, Miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni pamoja na Galilaya ya Chini. Ving'ora vya tahadhari vilisikika katika maeneo hayo vikifuatiwa na sauti za miripuko mikubwa. Vyombo vya habari vya Kizayuni vilitangaza kuwa kutokana na udhibiti mkali, picha za vipigo vya makombora ya Iran kwenye maeneo hayo ni marufuku kuchapishwa na kusambazwa.

Vyombo vya habari vya Kizayuni vimetangaza kuwa, wakati wimbi la nne la makombora ya Iran limepiga maeneo ya kaskazini mwa Israel, wimbi la tano la makombora hayo limepiga maeneo yote ya Israel hata yale ambayo hayajawahi kushambuliwa, tena kwa usahihi mkubwa.

View attachment 3369476View attachment 3369477
Umejishindia kuingia kwenye List ya watu ambao nitawanunulia soda leo
 
Kuna haja Dunia kuwa fair na kuanza kutatua hii migogoro ya mashariki ya kati kwanamna yenye usawa vinginevyo hakuna siku mashariki ya kati itakuwa na amani mpaka mwisho wa Dunia.
Amani haiwezi kutokea Mashariki ya kati maana Israel akiua watoto, kupiga hospital na makazi ya watu huko Gaza haionekani kama ni kosa, sasa kakosa adabu kaanza kwenda kumpiga hadi Iran bila sababu za msingi, hii Unfair treatment iliyopo Iran hawezi kukubaliana nayo na yeye lazima apige makazi ya watu tu maana amevumilia sana sasa kachoka
 
Mkuu Pakistan vita ni nyumbani kwao, hawa wamepigana miaka nenda miaka rudi na wana silaha nzito mpaka nuclear bombs, yaan hawa jamaa wana wataalam kinyama sana, na for your information India na wao ni 50-50 sikwambii kataifa kadogo kama Israel


Pakistani maponjoro tupu, tokea lini maponjoro wanajua vita, hata historia hujui, wale sio wanapigana, bali wanatishiana tishiana tu na kurusha vikombora but akili hakuna wala hawana latest modern tech ya vifaa na vita, najua huamini hili, fuatilia historia, vile vibomu vyao au kupigiana kelele na India isikutishe, ukitaka kujua vita angalia Russia, USA, Israel, hao ndio watu wa vita haswa.. Nchi zingine ni kelele kelele tu..!!
 
Taarifa kamili utapata wakishafukua vifusi kutoa mizoga ya Mazayuni
Yale makombora ya Iran wachambuzi wanasema yana shockwave ya juu sana kuweza kupasua masikio kama upo karibu.. kuvunjamilango au madirisha, pia yanaweza kusababisha uharibifu wa viungo vya ndani hata kama vipande vya kombora havijakugusa..

Tumeona wengi kasi yake linapokwenda kupiga chini ile velocity linavyoshuka likipiga chini unajisaidia pasipo kujua..

Kuna nyumba zimeharibika kwa sababu tu ya blast overpressure.. yaani nyumba haiguswi lakini inaachia nyufa..

Kuna watu Israel wamepata maumivu ya kichwa, wengine wanapoteza fahamu, wengine hadi asubuhi hii wanahisi kizunguzungu mtu anayumba kama amekunywa ulanzi..

Kuna ambao walipata mshtuko na moyo unapiga isivyo kawaida, waliokuwa karibu na yalipokuwa yanatua inasemekana kuna wengine wamepata PTSD..kwa maana yale makombora sauti yake ni zaidi ya dB 140 ambacho ni kikomo kwa masikio ya binadamu kuweza kuhimili... ukiwa kariu kuwa kiziwi ni suala la kawaida..

Baadhi waliokuwa na shinikizo la damu wamekata moto..

Wayahudi mpaka sasa wamechanganyikiwa.. hali ni mbaya sana huko...

Hayasemwi mengi mitandaoni baada ya Israel kuzuia vyombo vya habari kuonyesha casualties...
 
Jeshi la Ukombozi la Iran au Islamic Revolutionary Guards Corps ambao bado mpaka sasa hawajaingia vitani wametishia kufanya hivyo muda wowote kuanzia sasa.

Ikumbukwe IRGC ni sehemu ya jeshi la Iran.

IRGC limetambua sasa kuwa lengo la Israel ni kuuondoa utawala wa Iran au regime change.
 
Tangu kuanza SMO kati ya Russia na Ukraine, pamoja na yanayoendelea hapo nyumbani kwa Israeli muda huu, unagundua kuwa West ni mabingwa wa propaganda za kivita. Huyu Israel ukimsoma kwenye hadithi za THE BOLD, utahisi ni watu flani maalum sana kumbe hata tanzania tunaweza mama akitaka
Bangi mbaya...
 
Sema we jamaa mtetea china na mpinga USA, muda mwingine uwe unaongea facts upunguze ushabiki kama umetazama video kwa yale makombora Iran alirusha isingekuwa iron dome si Israel ingekuwa kifusi
Iron Dome haina uwezo wa kuzuia hypersonic missiles kwa sababu ya speed na complexity yake

Hizo air defense system za Mwamerika haziwezi kufua dafu hata kidogo

Marekani mwenyewe mpaka sasa bado yuko kwenye R&D ya hypersonic missiles
​
 
Kama people zipo kwenye mahandaki kwa nini vikosi vya uokoaji viko busy kufukua vifusi ili kuokoa?

Na video zinazosambaa kwenye mitandao zikionyesha magofu ya Israel zimerekodiwa na akina nani kama raia wote wamejificha kwenye mahandaki?
​
Swali zuri sana. 😂😂😂😂 Itakuwa wanafukua kuokoa furnitures

Hawa walishazoea kupigana kwenye ardhi za wenzao, sasa hv watu wameshawasoma, ukipiga kwangu nami napiga kwako wote tupate hasara
 
Back
Top Bottom