SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Hivi haya mashambulizi ya Israel kwenye vinu vya nukilia vya Iran mbona hayaja sababisha mionzi ya kinyukilia kuvuja au Uranium ilisha hamishwa kabla ya shambulizi?
Zile process zilizokuwa zikifanyika pale zilikuwa hatua za mwanzo kabisa ya full enrichment so risk ni kidogo pia vingne vilishambuliwa havifanyi kazi kwa muda au kabla ya kukamilika, kasome BBC news or Al Jazeera walielezea vizuri hilo swali lako just kagoogle, sehemu ambapo kunaonyesha kuna risk kubwa itatokea ni fordo japo Iran pia wamesema walihamisha material before ila ukiwauliza kwanini makamanda wako waliuawa eti lilikuwa ni shambulio la kushtukiza 😁😇 I don't need peace I want problem always
 
Kwani mada yetu ilikuwa inahusisha kutisha kwa silaha za Iran, ilikuwa je ni father of technology kwa upande wa kivita, kuhusu kutisha hata Gobole linatisha bashwee
 
🚨BREAKING: Saeed Izadi, head of the Palestinian Division in the IRGC Quds Force, has been eliminated in IDF strikes in Iran. Leading up to the October 7, 2023 Hamas massacre on southern Israel, he armed and funded terror group Hamas.
 
Hivi haya mashambulizi ya Israel kwenye vinu vya nukilia vya Iran mbona hayaja sababisha mionzi ya kinyukilia kuvuja au Uranium ilisha hamishwa kabla ya shambulizi?
Vingine wanatudanganya ionekane richa ya kushambuliwa na Iran wao mchakato wao unaenda vizuri, Kwa mkutano wa jana Chief wa IAEA anasema kabisa statement walioitoa Israel kuwa wameshambulia Bushehr niyauongo na inafaa kukanushwa, na hii nisababu Bushehr nikituo cha Nuclear iran kinasimamiwa na hao hao IAEA
 
Reports from Iran: IDF bombed several targets in Isfahan, including nuclear facility; separately, 15 Iranian air defense soldiers killed in Israeli strikes. via @kann_news & @N12News
 
🔴 AMEUAWA: Saeed Izadi, mwanzilishi wa mpango wa utawala wa Iran wa kuiteketeza Israel, ameuawa kupitia shambulio sahihi la Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) katika eneo la Qom.


Izadi alikuwa kamanda wa Kikosi cha Palestina cha Jeshi la Quds (Quds Force), na alikuwa kiungo muhimu kati ya utawala wa Iran na kundi la Hamas. Pia alikuwa miongoni mwa waandaaji wakuu wa mauaji ya tarehe 7 Oktoba. Alikuwa na jukumu la uratibu wa kijeshi kati ya makamanda waandamizi wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na viongozi wa Hamas.


Katika nafasi yake hiyo, Izadi alihusika moja kwa moja katika kuimarisha ufadhili wa kifedha kutoka Iran kwenda Hamas kwa ajili ya shughuli za kigaidi dhidi ya Israel.


Wakati wa vita, alihusika pia katika kuelekeza vikosi vya Hamas vilivyokuwa vikitekeleza mashambulizi kutoka Lebanon. Tangu hapo, amekuwa mstari wa mbele katika juhudi za kulijenga upya jeshi la Hamas na kuhakikisha kuwa kundi hilo linaendelea kushikilia mamlaka katika Ukanda wa Gaza.
 
Leta video footage inayoonyesha makombora ya Iran yakitunguliwa Jordan sio mnatumia hisia
Ona hii jamaa.


Hapo wanadai kuwa wanahofia kuangukia kwao ndio maana wanatatungua ila tunajua dhahiri ni janja janja ya kumsaidia Israel.
Pia ongezea na mifumo ya anga ya Arrow 3 na mengineyo.
Factless guy wewe.
 
Usitukane kijana ila kafuatilie Israel industrial weapons IWI viwanda vyake vipo wapi pamoja na elibit systems halafu urudi jukwaani kuwapa elimu pro Iran wenzako
Acha kuropoka wewe.
Israel viwanda vyake vipo hapo hapo nchini kwake.
Ukiona silaha zinatoka nje hizo ni za misaada.
Mwaka 2024 US walitaka kuminya misaada ya silaha kwa Israel dhidi ya Hamas Israel alilia kwa kwikwi.
Usituchukulie sisi watoto aisee.
 
Israel inapigana simultaneously ktk "multiple fronts" i.e Gaza, Lebanon, West bank, Yemen, Iran, Hamas and Hizbullah, ndyo maana wana wizara mahususi ya Vita (War Ministry)😀
 
Acha kuropoka wewe.
Israel viwanda vyake vipo hapo hapo nchini kwake.
Ukiona silaha zinatoka nje hizo ni za misaada.
Mwaka 2024 US walitaka kuminya misaada ya silaha kwa Israel dhidi ya Hamas Israel alilia kwa kwikwi.
Usituchukulie sisi watoto aisee.
Wewe pro lran utaambiwa nini kizuri cha lsrael ukubali? Ondoa ushabiki kwanza na ukubali kujifunza ndio utaelewa ukweli ulivyo
 
Kwani mada yetu ilikuwa inahusisha kutisha kwa silaha za Iran, ilikuwa je ni father of technology kwa upande wa kivita, kuhusu kutisha hata Gobole linatisha bashwee
Inatakiwa utambue Iran ni nchi iliyowekewa vikwazo tangu 1979 vya kiuchumi na silaha.
Imeweza kuunda ballistic missiles, cruise missiles na hypersonic missiles kwa wanasayansi wake mwenyewe.
Iran inaunda drone bora za kivita za shahed na zilithibitisha ubora wake kwenye vita ya Ukraine hadi Zelensky alitamka wazi kuwa sipigwi na Urusi tu ila napigwa na Iran pia.
Iran imeunda mifumo yake pekee ya ulinzi pasi na msaada wa taifa lolote ya Khordak-3 ,Khordak-5 na Bavar-373.
Na imeonesha ubora wake hata ukitizama interception yake na iron dome ya Iran Ina intercept kwa haraka zaidi.

Jiulize kama Iran asingewekewa vikwazo vya kiuchumi wala silaha angekuwa wapi!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…