SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Ila Iran walitukosea sana kwenye True Promise 1 & 2, kwanini hawakufanya haya wanayofanya sasa ilhali uwezo wanao?

Walijibu kinyonge ndio maana Israel walipata kiburi cha kushambulia na kuua viongozi kila mara. Sasa hivi sidhani kama watathubutu kushambulia tena kiurahisi kama walivyokuwa wanafanya hapo kabla ya kupewa mwana ukome ya sasa.
Nifah hivi unaona Iran anafanya vizuri?
 
Mpaka sasa Kwa sisi watu wa kubeti GG imetoka.ila matokeo ni ngumu kupata kwa sababu upande mmoja wanakataza kuchukua picha au video. Lakini kwa muonekano ni wazi ubao unasomeka

IRAN 4 - ISRAEL 2
Kila sehemu kwenye vita lazima kuwepo sheria za matumizi ya mitandao kwa tahadhali ya taarifa hizo kumnufaisha adui hivyo kila upande una namna yake kulinda taarifa zake.

Mfano leo hii waandishi wa ujerumani walizuiwa kupiga picha mubashara wakati wa shambulio la Bersheva hii ni hatari sababu Una pa adui nafasi ya kujua amekosea Shabaha au amepatia na kwa video za Live anaweza kuona apigwe wapi tena. Hivyo ni vizuri sheria za kila nchi zikafuatwa. Istoshe video za Live pekee ndiyo zinazuiwa..

Kwa upande wa ushindi vita huwezi kushinda mezani hapa Mshindi ni Israel tu aliyeweza kuvunjwa ngome ya majeshi ya Iran na kuwaua makamanda wake waandamizi 30+ na wanasayansi 60+ kuharibu vinu vya kinuclear kisha kushambulia vituo vya kijeshi na kuangamiza mifumo ya ulinzi wa anga wa Iran mpaka sasa hivi wanalimiliki anga lote la Teheran wanaingia na kutoka bila shida yoyote. Na huo ndiyo ushindi bila chenga.

Upande wa Iran wameshindwa kujibu mapigo ya Israel katika kila Nyanja Jeshi Lao la anga hata halionekani kabisa likileta upinzani kwa majeshi ya adui ya Israel. Majeshi ya Iran yameonyesha wazi kuwa hawana weledi katika uwanja wa vita maana wanapiga maeneo ya kiraia kama vile Hospital makazi ya watu na maeneo ya wazi na wameshindwa kuangusha hata ndege-vita moja ya Israel hata tu kupiga kambi ya Jeshi wameshindwa kabisa . Hivyo kijeshi ni kushindwa vibaya!!!
 
Mungu wa Israel amelala usingizi wa pono.

Mungu wa Israel amedhoofu.

Mungu wa Israel ameshindwa kulinda taifa lake dhidi ya makombora ya Iran.

Mungu wa Israel ni mchomvu na mdhaifu sana.
Jehova kavishwa Sanda na Wahuni wa Iran. Kazi kipimo cha utu
 
Wewe ebu nenda kawatafute watoto wenzako kwenye mabanda ya video muongopeane izo story za Rambo.Ivi unajua ndege 200 au unaongea tu.
Siwezi kukulaum maana najua kwa Wafuga Midevu na Majini kama wewe huwezi kunielewa kwa sababu silaha yenu kubwa ni uongo tu. Nakuwekea hapa chanzo cha habari hapo chini najua pia huwezi kuelewa nakushauli tu utafute anayejua kiingereza akusaidie kuelewa!!

View: https://x.com/ryan___98_/status/1933772102529638812?s=12

View: https://x.com/israeli_sniper/status/1934446098937966793?s=61

View: https://x.com/artisbrutal2021/status/1933528614064304594?s=61
 
Hii wiki nzima Marwan Bishara kwenye uchambuzi wake anacheka sana jinsi Trump anavyoruka ruka na vitisho vipya kila siku.

Kuna ile siku aliyowahi kuondoka kwenye mkutano wa G7, Macron akasema anawahi mambo muhimu yeye (Trump) akakataa kwamba Macron amefanya makosa hakuna anayejua anawaza nini… Marwan akasema hata yeye mwenyewe Trump hajui anawaza nini! Nilicheka sana.

Hii aibu wanayoipata Israel na US inaburudisha sana, Iran wameushangaza ulimwengu.

Kwa jinsi mambo yalivyo Israel wanajuta kumuua yule Mkuu wa Majeshi na wasaidizi wake maana yule anaonekana ndiye aliyekuwa anazuia haya mashambulizi mazito, hawa walioko hivi sasa ni vichaa waliochafukwa!
 
Back
Top Bottom