SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Mashairi na ngonjera tumekataa leta videos au source za za mashambulzi ya Israel ambayo sio AI
 
Hivi haya mashambulizi ya Israel kwenye vinu vya nukilia vya Iran mbona hayaja sababisha mionzi ya kinyukilia kuvuja au Uranium ilisha hamishwa kabla ya shambulizi?
According to Iran wamehamisha vinu vyao, probably role ya Mrusi Iran ni hio,

Na pia toka Zamani vinu ambavyo vipo juu ya Ardhi ni geresha tu, kila mtu anajua project zote za Iran zinafanyika chini ya Milima.
 
Anaongelea yale mabox ambayo Israel aliyapiga, Iran Aliweka ndege feki F14 (Tomcat) IDF akazipiga waka upload kwenye mtandao.
Ko Israel hawana akili wapige madubwasha, basi sawa ndege zipo mbona hamzirushi angani au ndege zenu ni mikate zinakaa kwa shelf
 
B-2 itaenda kupiga nuclear site ya fordow? Maandalizi yote yanaonekana. Hii sites pekee ambayo Israel hawana makombora ya kushambulia na kuharibu, ni marekani pekee ndio wanaweza kuipiga na kuiharibu
 
Ukisoma vizuri historia utafahamu kwamba mataifa ya Magharibi yamekuwa yana kiwewe (Obsession) na madola ya Uajemi tokea kipindi cha kale. Amini nakwambia hata kina Ayatollah na dola la kiislamu wakipinduliwa na Iran likawa dola la Kikristo, Marekani, Israel na Uingereza hawawezi kuwaacha waajemi waishi maisha yao.

Madola yote ya kale makubwa, kuanzia Macedonia, Rome, Rashidun Caliphate, Mongol Empire, Holy Roman Empire, British Empire, Russian Empire na The Soviet Uniona yote yamewavamia waajemi kwa nyakati tofauti katika historia ya miaka 2000 iliyopita. Leo hii Marekani inafanya hivyohivyo. Chanzo kikubwa ni kwamba Iran ina utajiri mkubwa mno, lakini pia iko katikati ya barabara ya kimataifa inayounganisha Europe, Middle East, Central Asia na Far East.

Wagiriki walivyofanikiwa kuvamia Uajemi, walifanikiwa kufika hadi India na kutengeneza makoloni makubwa kama Greco-Bactria yaliyokuwa jirani kabisa na Uchina. Waislamu walipofanikiwa kutawala Iran (Sassanid Empire) ndiyo wakaleta ustaarabu mkubwa duniani kwa kuunganisha Ulaya na Asia. Leo hii Urusi, Israel na Marekani zinagombania njia ya Iran na Pakistan ambazo ni muhimu kwa biashara ya dunia na ulinzi.

Kumbukwa mwaka 1946, Joseph Stalin na Harry Truman waligombana mno kwasababu Urusi alikataa kutoka Iran baada ya vita vya pili vya dunia. Marekani alifahamu kabisa kwamba kama Urusi akikalia Iran ingekuwa basi tena kwasababu ni sehemu muhimu kimkakati. Leo hii, mbali na mengine, anayetafutwa Iran ni Uchina. Iran ikianguaka litakuwa ni pigo kubwa mno kwa Uchina, kiusalama, kibiashara na Kimkakati kutokana na umuhimu wake.

Mambo ni mengiiiii sana.


NB: Hii njia ni moja ya sababu kubwa inayoweza kuondoa kabisa nguvu ya G7 kwenye biashara ya dunia, na kuzifanya Iran-Pakistan kuwa, THE NEW SUEZ/MALACCA CANALS. Jambo kama hili likitokea G7 itakuwa na hali mbaya.

Sababu ni nyingi mno, ila fahamu kwamba tatizo siyo Ayattolah wala Uislamu, tatizo ni lilelile la miaka yote: EXCESSIVE EMPIRIALISM.
​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…