Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Another one
Screenshot_2022-03-25-13-16-44-373_com.gbinsta.android.jpg
 
Hisabati ni changamoto Tanzania. Unaleta screenshot "what are the 5 highest ranks in the (US) army? halafu unachora nafasi ya kanali ambayi ni nafasi ya sita.
Ndiyo, naona nafasi ya Kanali haiko kati ya vyeo vikuu. Makanali kuna zaidi ya 1600 kwenye jeshi la ardhi la Marekani. Mameya wako zaidi ya 7700. majenerali wako mnamo 230.
Hata sijali kanali yako ni nini au nani. najali upuuzi unaonukuliwa.
Hujaleta ushahidi wowote kuwa vikosi vya NATO vimefika mpaka wa mashariki wa Ukraine. Isipokuwa maneno ya kanali yako ambaye labda hajafaulu kusema yale alichotaka kusema , ila nukuu jinsi ulivyoleta ni upuuzi.
Nimesikia majenerali wakubwa (Warusi safari hii) walioeleza uwongo na upuuzi kuhusu mafanikio ya jeshi lao, serikali ya Kinazi katika ukraine... na kadhalika.

Usijifiche nyuma ya sare ya mtu mwingine. Simama na lete ushahidi kwa yale unayotangaza hapa jukwaani. Kama huna - basi, wako wanzako watakofariji, bila shaka.
Sawasawa...
 
Aisee kweli wewe una uwezo mdogo wa kusoma na kuelewa mambo...Colonel ktk US army ktk hali ya kawaida (nje ya vita) ni rank ya tano...uwe wasoma na kuelewa mambo kabla ya kukurupuka kukomenti.

Na tufanye iwe Colonel ni nafasi ya sita, kwa hiyo kwa akili yako ilivyo ndogo kuwa nafasi ya 6 kutamfanya Colonel asiwe ktk maafisa wa juu wa jeshi la Marekani na hivyo kuwa ktk makuruta?

Maswali mengine sikujibu kwa kuwa yapo wazi kwa mtu mwenye akili ya kawaida, labda kinyume chake. Hata darasani mwalimu akijitahidi kuelezea vipi somo lazima kuna vilaza hawatamuelewa.

View attachment 2163893
Haya vyeo hivi sijali kabisa, ukipendelea kanali yako alikuwa mtu mkuuubwa sana huko. Sawasawa. Jambo muhimu ni upuuzi katika nukuu yake na hapa naona unajikunja tu. Upuuzi ulikuwa hii katika post yako #20,359
:
"Nukta yenyewe ni kuwa Russia hawataki majeshi ya Marekani, mizinga ya Marekani, na majeshi ya NATO kwenye mpaka wake na Ukraine (Mashariki ya Ukraine kwenye majimbo yaliyotangazwa huru na Putin).

Colonel Douglas akaendelea kusema: Kiukweli kabisa hata sisi Wamarekani hatukuyataka majeshi ya Russia na mizinga yake ndani ya Cuba, Putin naye hataki mambo hayo mashariki mwa Ukraine. Lazima tukubali madai hayo. Tuache kujifanyisha kuwa madai hayo hayana maana (ni ya kipuuzi).
"
Ninakuambia (pamoja na kanali mkubwa wako): haikuwahi kutokea kwamba vikosi vya NATO vimefika kwenye mpaka huu. (lakini roketi za Urusi zilifika Kuba). NATO ilikataa tangu 2008 kupokea Ukraine.
Putin ameanza vita kwa kutaja jambo ambalo halikutokea wala halikupangwa.

nchi 2 ndogo za NATO zinazopakana na Urusi (bali na Alaska) ni Estonia na Latvia. Katika nchi hizo hazikuwa na wanajeshi wa NATO wa kudumu isipokuwa wenyeji. Baada ya uvamizi wa kwanza wa Urusi katika Ukraine mwaka 2014 NATO ilipeleka kila nchi askari 1,000 wa nje; 1,000 si idadi inayomtisha mtu yeyote, walipelekwa kama ishara kuonyesha tu NATO inasimama upande wa wanachama wake wadogo pia. Hata hao hawakuwa askari wa kudumu, walifika kwa muda na utaratibu wa kubadilishana.

nchini Ukraine haikutokea kitu kama hicho. Hapa nasema nukuu ya mheshimia kanali mkuu ina upuuzi ndani yake.
Wewe utajua kwa nini umeileta, hadi sasa unajificha nyuma ya sare.
 
Mjomba naomba kuuliza, Nato waliingia libya kama nan? Gadafi alirusha bomu kwa mwanachama wa Nato?
Kikao cha dharula cha nato jana kuijadili ukraine, je walijadili ukraine kama nani? Ikiwa si mwanachama?
Na je wanatoa misaada ya nini? Ndio maana tunasema waingie wakapigane, wasitume silaha tu.
Swali la mwisho, je Nato ni kikundi mchongo cha waoga?
Bila kusahau,NATO pia walipeleka majeshi kupiga Yugoslavia pale kuiokoa Kosovo,Bosnia and Herzegovina,wakati hizi Jimbo hazikua Wanachama wa NATO.
 
Hujui kusoma ama? EU ndo wateja wakubwa wa gesi na mafuta ya mrussi. Kwa hio wakimgomea(washaanza ) atakuaamepata pigo kubwa sana katika uchumi wake
Unaisi wanaweza waaambie wajaribu ivi mnaisi urusi ni Sawa na Libya kumtoa nje ya mfumo mtu anayewaudumia Kwa asilimia zaidi ya30 si jmabo dogo it need Time na akili sana watabweka Ila mwisho wa siku watarudi kwake Tu kuongea wayamalize
 
EU wanasema Tsh unawazungumzia uongo/unawazulia...wao wamekaa kwenye kikao chao cha pamoja (nchi/mataifa 30 dhaifu) wametoa tamko la pamoja (walau lionekane lina nguvu) kuwa Russia asimamishe vita maramoja na kuondoa vikosi vyake na mijisilaha yake Ukraine.

Hili nalo mpaka tuandike 'notice' zake ?!

View attachment 2163813
Siangalii wanachosema, naangalia wanachotenda.
 
Back
Top Bottom