Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Sawasawa...
 
Haya vyeo hivi sijali kabisa, ukipendelea kanali yako alikuwa mtu mkuuubwa sana huko. Sawasawa. Jambo muhimu ni upuuzi katika nukuu yake na hapa naona unajikunja tu. Upuuzi ulikuwa hii katika post yako #20,359
:
"Nukta yenyewe ni kuwa Russia hawataki majeshi ya Marekani, mizinga ya Marekani, na majeshi ya NATO kwenye mpaka wake na Ukraine (Mashariki ya Ukraine kwenye majimbo yaliyotangazwa huru na Putin).

Colonel Douglas akaendelea kusema: Kiukweli kabisa hata sisi Wamarekani hatukuyataka majeshi ya Russia na mizinga yake ndani ya Cuba, Putin naye hataki mambo hayo mashariki mwa Ukraine. Lazima tukubali madai hayo. Tuache kujifanyisha kuwa madai hayo hayana maana (ni ya kipuuzi).
"
Ninakuambia (pamoja na kanali mkubwa wako): haikuwahi kutokea kwamba vikosi vya NATO vimefika kwenye mpaka huu. (lakini roketi za Urusi zilifika Kuba). NATO ilikataa tangu 2008 kupokea Ukraine.
Putin ameanza vita kwa kutaja jambo ambalo halikutokea wala halikupangwa.

nchi 2 ndogo za NATO zinazopakana na Urusi (bali na Alaska) ni Estonia na Latvia. Katika nchi hizo hazikuwa na wanajeshi wa NATO wa kudumu isipokuwa wenyeji. Baada ya uvamizi wa kwanza wa Urusi katika Ukraine mwaka 2014 NATO ilipeleka kila nchi askari 1,000 wa nje; 1,000 si idadi inayomtisha mtu yeyote, walipelekwa kama ishara kuonyesha tu NATO inasimama upande wa wanachama wake wadogo pia. Hata hao hawakuwa askari wa kudumu, walifika kwa muda na utaratibu wa kubadilishana.

nchini Ukraine haikutokea kitu kama hicho. Hapa nasema nukuu ya mheshimia kanali mkuu ina upuuzi ndani yake.
Wewe utajua kwa nini umeileta, hadi sasa unajificha nyuma ya sare.
 
Bila kusahau,NATO pia walipeleka majeshi kupiga Yugoslavia pale kuiokoa Kosovo,Bosnia and Herzegovina,wakati hizi Jimbo hazikua Wanachama wa NATO.
 
Hujui kusoma ama? EU ndo wateja wakubwa wa gesi na mafuta ya mrussi. Kwa hio wakimgomea(washaanza ) atakuaamepata pigo kubwa sana katika uchumi wake
Unaisi wanaweza waaambie wajaribu ivi mnaisi urusi ni Sawa na Libya kumtoa nje ya mfumo mtu anayewaudumia Kwa asilimia zaidi ya30 si jmabo dogo it need Time na akili sana watabweka Ila mwisho wa siku watarudi kwake Tu kuongea wayamalize
 
Siangalii wanachosema, naangalia wanachotenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…