Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Sikusema hao wafanyabiashara wa MArekani ni Khazarian Mafia. Ni hao waliobuni hadithi ya uwongo kuhusu Khazarian Mafia ambayo haiko. Biashara ya intaneti katika nchi hizi ni hivi: unaunda tovuti, unaweka matangazo ya kibiashara ya makampuni kama Amazon, Mcdonald, wauzaji wa kila aina. Wanalipa kama matangazo yao yanatazamiwa. Senti tu. Hivyo kila tovuti inpeleka programu ndogu za "cookies" kwenye vifaa vyetu watumiaji, vinahesabu tunaangalia nini, mara ngapi. Mwenye tovuti anatafuta njia ya kuvuta watu kwake ili walete "clicks" kwenye kurasa zake. Watu kama hao unaonakili wanajaribu kupata clicks kwa kuwaza hadithi za ajabu; kadri damu na jinai na njama ziko nyingi, zinavuta watu wanaoleta clicks. Hawajali ukweli wala nini, wanataka kuvuta watu tuz.
Halafu wanapata pia watu wanaoamini na kusambaza upuuzi huo.
 
Kidume siku ya leo kaishachukua kyiev, mji mkuu wa Ukraine.

● Marekani yuko wapi???

● Umoja wa mataifa uko wapi???

● Umoja wa ulaya uko wapi???

● Umoja wa africa uko wapi???

Wamekalia porojo tu kenge hao.
Mwezi mmoja na siku kadhaa kidume kakimbia 🤣🤣🤣🤣🤣

Russia imewahaibisha watu kama hawa
 
Leo Russia anaonewa wivu 🤣🤣🤣🤣

Vipi No Rubble no gas, ilifanikiwa?
 
Case ya Marekani ni tofauti kabisa na Urusi.Marekani mambo yao wanafanya without provocation,history tells it all.Anything they do is for econonomic and political gain.What Russia is doing in Ukraine is not for economic and political gain,it is purely for self defence.The West wants to destroy Russia by using its' proxy Ukraine and Russia as a nation must defend itself.
 
Malengo yao ama hutaki kujua au hujajaribu kutafuta, au hupendi kusema ukijua. Putin aliwahi kusema waziwazi hakubali Ukraine ni taifa na nchi tofauti na Urusi, alisema ilikuwa kosa kubwa la Lenin kukubali Ukraine iwe jamhuri la pekee nje ya Urusi ndani ya Umoja wa Kisovyeti. Alisema makosa ya zamani yanatakiwa kusahihishwa.
Hii ni lugha ya mkoloni ambaye ahwezi kuachana na makoloni yake. Waingereza waliongea hivyo kwa muda mfupi kuhusu nchi za Afrika kabla ya kulazimishwa kuachana nazo.
 
Mnajua licha ya kupeleka Majeshi Luhansk ila bado Ukraine anakomboa maeneo.

Alafu ndio manataka vita na Poland na Finland 🤣🤣🤣
 
Uko sahihi ila lazima waheshimu mipaka ya nchi nyingine.
 
BS, magharibi iliwekeza sana kujenga uchumi wa Urusi walikuwa na matumaini wanapata nchi mpya ya kujenga uchumi wa mkimataifa. Makampuni ya magharibi yalileta viwanda vya kutengeneza magari (yaani Moskvich na Lada za zamani zilikuwa takataka ) na vifaa vingine. Walileta tekinolojia ya kuimarisha sekta ya gesi na ya mafuta.
Putin alianza kuota ndoto za kurudisha yale aliyoona kama "ukubwa wa Urusi" akaumizwa moyono kwamna koloni nyingi zilipata uhuru akaanza mchezo wa kuzirudisha. Ukraine hasa kwa sababu historia yao ya pamoja ilianza mjini Kyiv, miaka 1000 iliyopizta,
Hataki kukubali kwamba katika miaka hii mingi taifa 3 zilijitokeza, ambayo ni kawaida uiangalia maeneo mengine.
Hakuna anayetaka kumega Urusi (isipokuwa watu kama Chechen bado wanatafuta uhuru) lakini Putin anataka kufuta taifa la Ukraine.
 
Siku hiyo itafika pale Russia itakapojaribu kuongeza eneo la uvamizi zaidi ya ule waliofanya 2014, vinginevyo wasipojiunga NATO nchi yao itaendelea kuchukuliwa vipande vipande mpaka iishe yote.
maneno bila vitendo ni taarab au mziki kama miziki mengine
hakuna siku utaiona UKRAINE ikiwa NATO kama waingojea utaingojea mpaka kufa kwako
 
Putin ni kichwa kigumu
 
Hivyo ndivyo itakavyokuwa
 
Hivi kwa nini NATO ipo?. Nchi zote zikijiunga NATO nani atakuwa adui yao.
Mi nahisi hawa wababe wanatafuta kutawala dunia sera zao ndio zitamalaki. Imagine USA na sera zake kusaidia wengine kwa kukopa huku ikiacha wananchi wake hohehahe. Na Russia kutumia gharama kudhihirisha uwepo wake?. Mwisho wa hii vita ni mbaya sana kwa dunia hasa Russia akishindwa. Sera za USA zitatamalaki na upinde ndio itakuwa Dini ya dunia.
Siku hiyo itafika pale Russia itakapojaribu kuongeza eneo la uvamizi zaidi ya ule waliofanya 2014, vinginevyo wasipojiunga NATO nchi yao itaendelea kuchukuliwa vipande vipande mpaka iishe yote.
 
Acha ujinga wewe,kwani hata kama waliweka viwanda Urusi,waliweka kwa kuwa wanawapenda Warusi,si waliweka for their economic gain and advancement of the wider NWO agenda.Amkeni people,mbona mnampigia chapuo Shetani?
 


UKRAINE kuna masharti ya URUSI inatakiwa iyafuate sababu URUSI na WEST ni maadui?

Ndo maana nakuambia huko ni kuwa bully kwa nchi zenye uwezo mdogo kijeshi.

UKRAINE ingekuwa nchi inayojimudu kijeshi na ina uwezo wa kuitandika MOSCOW, URUSI ingeishi nayo kwa utaratibu upi? URUSI ina maslahi pale UKRAINE ndio maana haitaki ijimudu kijeshi.

Kwani ALASKA si jirani na URUSI?

CHINA ikitaka kuunda urafiki na WEST, URUSI itaenda kufanya oparation ya kufuta jeshi la CHINA?
 
Acha ujinga wewe,kwani hata kama waliweka viwanda Urusi,waliweka kwa kuwa wanawapenda Warusi,si waliweka for their economic gain and advancement of the wider NWO agenda.Amkeni jamani,mbona mnampigia chapuo Shetani?
Nani anaweka viwanda kwa kupenda? Waliweka kwa faida! Kama Urusi ina faida katika biashara ya amani, wengi wengine wanapata faida. Msingi ni kufaidiana. Ila kama anatumia utajiri kwa fujo, wote wanapata hasara.
 
Kifupi Ukraine Ikijiunga NATO ndio mwisho wa Russia. Au hii vita ikiisha na Russia akapigwa ndio mwisho wa Russia na NATO itabakia kummaliza China then India.
Siku hiyo itafika pale Russia itakapojaribu kuongeza eneo la uvamizi zaidi ya ule waliofanya 2014, vinginevyo wasipojiunga NATO nchi yao itaendelea kuchukuliwa vipande vipande mpaka iishe yote.
 
Ila wamekutana na kigingi. Sema Japan kwa Russia sio kitu. Hiyo kazi ni ya kiduku

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…