Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

What if NATO walitaka Ukraine iingie kwenye mpambano ili wajue Russia ana zana gani, hii hatari mno kwa russia kuanza kutumia silaha zake hizo.
Haiwasaidii kitu kizifahamu mapema silaha za Russia.
Hata wakizijua Leo itawachukua miaka kumi kuweza kupata kinga yake.
Na siku wakipata kinga yake,Urusi atakua amegundua silaha ya kizazi Cha mbele zaidi.
Haya ninayoyasema sitanii,wala sipigi propaganda.
Kuna mahali nilisoma hii kitu.
 
Haitawasaidia coz hawawezi kutengeneza anti yake kwa kipindi kifupi tu hiki

Ujue Putin hajakurupuka kuanzisha hii vita. Kwa taarifa Russia ilijiandaa zaidi kwa Nato kuliko kwa Ukraine yenyewe
Da aisee safi sana,umejibu kama nilivyomjibu na Mimi pia,na sikua nimefika Huku kwenye majibu Yako wakati nasoma coments.
Ulichomjibu ndio Hali halisi.
Kuna sehemu nilisoma juu ya mipango ya silaha za Urusi.
 
Kwanini Urusi hawakuitumia hii silaha ya laser 'zadira' tangu awali ili kupunguza madhara ya vifo na majeruhi upande wao ?

T14 Armata mohamedidrisa789 Gwappo Mwakatobe Kalamu1 Kichuguu
lee van cliff
Ndugu yangu Proved ,nakuamini sana kua unaelewa mambo kwa upana wake.
Vita yoyote duniani,hua tunaanza na silaha nyepesi,Huku tukiangalia mwenendo wa vita.
Kadiri ugumu unapokuja nasi huongeza uwezo ama wa askari ama wa silaha.

Kwa mfano katika vita askari wa kawaida wakizidiwa huamua kuleta makomando kuja kuvunja nguvu za Adui.

Sasa kwa swali lako kama ulisoma vizuri maelezo ya Putin ni kwamba wameleta silaha hizo baada ya kuona USA na UK wakipump silaha zao za kisasa kwa Ukraine.

Ni kama vile Sub TU kwenye mechi ya soka,
Timu B ikifanya sub na timu A nayo inafanya sub.

Sasa hivyo ndivyo Putin kawafanyia.
Wamejifanya kuleta silaha zao za kisasa,Putin nae kaleta zake za kisasa.
Kwa bahati mbaya silaha za Putin zinazichoma/zinaziunguza silaha za USA na UK .😀😀😀

Hii ni kama kipindi kile Cha Musa alipokua anashindana na Farao.
Musa alitoa fimbo yake ikageuka kua nyoka,Wachawi wa Farao nao wakatoa na wao fimbo zao zikageuka nyoka.

Musa akaiamuru Nyoka yake ifanye zaidi,
Fimbo/nyoka ya Musa ikazimeza wale nyoka wa Wachawi wa Farao.
Mchezo ukaishia hapo.
Hivi ndivyo afanyavyo Vladimir.
Na. Vita ikiendelea utaona silaha ambazo hazikuwahi kusikila wala kuonekana duniani kutoka Jeshi la Urusi.
 
Kubwa US (NATO,) walitaka mpindua Erdogan miaka ya juzi akatonywa na Mrusi kazima mapinduzi
 
Hivi South Korea,ni NATO? Mbona Urusi inapigana na husu ya dunia??? This is unfair 😌
Mkuu hii mbona Cha mtoto.
Urusi ni mwamba nakuambia.
Tukiwaambiaga Urusi ni Superpower hua tunamaanisha.
Ngoja nikuambie hii ni ndogo.
Urusi ilipokua inapigana na Afghanistan ,ikiwa peke yake kama hivi Leo Upande wa Wawaafghan ulikua ukisaidi na nchi zifuatazo.
USA, UK,west German,China, Pakistan,Saudi Arabia,na NATO wengine.
Waliishia kutoa misaada TU ya silaha kama hivi Sasa,alipambana nao miaka 10.


Wakati USA ilipopigana na Watalaban ikisaidiwa na NATO ,pakisata,na vijinchi vingine vingi TU.unawsza ku google.
Wakati watalaban hawakuwahi kusaidiwa na nchi yoyote walipigana miaka 20 na hawakuwashinda watalaban.

Hebu fikiria kama Urusi na china zingewapa sialha watalaban kama afanyavyo USA na NATO.
 
hiv wale jamaa wa seal team six wale si wangee da kumaliz bii game. au jamaa wa delta force

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Mkuu hivi ulishawa wahi kuwasikia wanyama wanaoitwa Spetsnaz?
Hao ndio askari maalumu wanaogopeka duniani.
Wanamafunzo ya hatari kuliko askari yoyote duniani.
Ukipeleka watu 1000 wakajifunze Kuwa Spent,wanapita askari 100 TU.
Waliobaki utakuta wamevunjika viungo,wamefeli,wameacha,na wengine hata kufa.
Ukimteka Spetsnaz ukianza kumtesa utachoka wewe.

Huko nchi za nje na hata ndani hua Kuna maneno yanasemwa kua Spetsnaz hua hawasikii maumivu,hata akiumia,au umtese vipi hawasikii maumivu.

Mwandishi mmoja alihoji Spetsnaz mmoja.
"Eti nasikia nyinyi hua hamsikii maumivu"

Spetsnaz akacheka,kisha akajibu" hapana hua tunasikia lkn tumefundishwa kuweza kuhimili maumivu."

Kibaya zaidi Spetsnaz ndio askari pekee Duniani wakimaliza ama wakihitimu mafunzo hua wanavalishwa/ wanavaa bullet proof kwa ajili ya hatua ya mwisho ya kuwalenga vifuani kwa risasi za moto kama kupewa spirit ya kutokuogopa risasi.
Hii sio propaganda .
 
NATO wakisikia hivi ndo hawatathubutu kabisa kuingia vitani na Urusi kwa ajili ya kuihami Ukraine.
Tuliwaambia Russia sio Libya.
 
Asante kwa jibu zuri kaka Lee, hali halisi ya uchumi wa Russia ikoje mpaka wakati huu? Je, uchumi wake unaelekea kufanana na uchumi wa Zimbabwe kama alivyotabili mwanadada Coco na wanauchumi wenzake wa mchongo hapa jukwaani?
Mkuu Russia mambo ni kama vile ilivyokua kabla ya vita.
Leo katibu Mkuu wa UN kaiomba Urusi iruhusu chakula kutoka Ukraine na Urusi kisambazwe duniani.
Je kama Hali ya Urusi ni kama zimbabwe kwa Nini katibu Mkuu UN aiombe Urusi iruhusu kisambaza chakula Duniani.maana yake Urusi ndio Ina ufunguo wa chakula Cha Dunia kwa Sasa.
Hata hivyo Urusi machale yamewacheza,wanasema hivi,Wana mashaka kua huenda chakula kisambazwe kinakohitajika Bali kwenda kuwekwa kwenye maghala ya Ulaya.
Mwisho wa siku Russia wesema kua hawata sabaza chakula,Bali chakula kilichopo ni kwa akiba ya raia wa Urusi TU.
Hapa maana yake Urusi anataka kuwaua njaa waliomwekea vikwazo.
Rubo inazidi kupanda thamani,

Kwa kifupi athari za kiuchumi zipo lakini zaidi zinawaathiri wa west.
 
@ Naomba hii aione Frank Wanjiru
 
Medvedev mnoko sana aisee.
 
Ukitoa silaha RUSSIA ananini chengine chakuuza
RUSSIA inatakiwa iheshimiwe mnoooooooooo

Sent using Jamii Forums mobile app
Comrade mbona una swali jepesi hivyo?
Au unatania.
Mimi kwa kujibu TU ni kwamba ana Kila kitu Cha kuuza kama walivyo navyo wachina, wamarekani,waingereza na nchi nyingine.
Kwa kifupi Urusi Iko katika nchi tatu zenye viwanda vingi duniani.
Viwanda vya kila kitu.
Na hii ni tabia za nchi za kijamaa,yaani kuwa na uwezo wa kujitegemea.
Mkuu yaani Urusi inaiuzina Marekani Injini na mashine.kweli hujui.
Inauz magari ,mashine na mitambo n.k
 
Russia's siege of the Ukrainian city of Mariupol stuttered towards its end on Thursday, with hundreds of fighters still holed up in the Azovstal steel works and some 1,700 who have already surrendered facing an uncertain fate.

Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
 
Ahsante mkuu, kwa kukumbushia hili, kwani tuliwahi kulisema huko nyuma juu ya 'prototypes', n.k.

Hukupenda kuliendeleza, lakini huku'acknowledge' ukweli huo hadi hapa leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…