Mtazamo wako ni mzuri sana na uko sahihi, ila mwaka jana mimi niliandika humu kwamba Russia itapoteza wateja wa silaha kutokana na sanctions Warusi wakabisha. Niliandika ilipoanza Egypt kusitisha, ikaja nchi nyingine sikumbuki kama ni Indonesia au nani jirani yake, ikaja India kwenye deal la helicopters mwaka jana huohuo, ikaja India Airforce kwenye fighters ikachukua Rafales ikaachana na additional Russian jets probably Sukhoi 30 MKI ilizonazo.
Hata January hii Indian Navy ilinunua Rafales kwa ajili ya carriers
View attachment 2525111
Inazo Russian Mig 29K ila haikuzitaka. Na hapo kwa Serbia ulivyosema kama Russia inaanza vita (wanayoita operation) kisha wanashindwa kufanya services ya silaha walizouza kwa wateja basi hao hawako serious. Hutokaa usikie eti Marekani imeshindwa kufanyia service ndege za washirika kisa imevamia wapi sijui. Na hii vita sio ya kufanya nchi inayojigamba ina nguvu kushindwa service ya ndege za wateja, mbona air warfare ni ndogo.
India, China, Egypt ndio wateja wakubwa wa ndege za Russia na hawanunui uko tena. Algeria sijui