Huu uasi wa Prigo unachanganya sana. Binafsi sijui nisimame upande gani, wa mapunduzi ama maigizo? Maana nadharia zote mbili ni Tata.
Kama ni mapinduzi kweli napata maswali yafuatayo
1. Prigo anadai wanajeshi wake wapatao 2000 walishambuliwa na MoD. Lakini, hatuoni ushahidi wowote juu ya hilo.
2. Huu ujasiri wa kutaka kupindua serikali ambayo anaitegemea kwa Silaha na pesa Prigo aliutoa wapi? Ama kuna majenerali walikuwa wanamsapot?
3. Wagner waliwezaje kuuteka mkoa wa Rostov bila upinzani wowote yaani combat
4. Wagner waliwezaje kutembea km 700 bila upinzani wowote zaidi ya kusemekana walilipua helicopter 4 na ndege 1. Kwanini msafara wao haukupatwa na madhara?
5. Kama Prigo aliweza kuungwa mkono na jeshi maana yake alipata jeshi na vifaa jeshi. Je ilikuwaje asitishe mapinduzi hata kabla ya mapigano ya ana kwa ana?
6. Inawekanaje, Prigo akubali kwenda uhamishoni na kukubali kulipoteza jeshi lake bila hata ya mapigano yoyote? Tena nusu ya jeshi lake ikiwekwa chini ya wanaya wake, Shoigu na CDF.
7. Inasemekana baadhi ya wanajeshi wa Wagner waligomea mapinduzi ya Prigo. Mbona hakukutokea mapambano kati ya makundi hayo mawili?
8. Je, waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi wameondolewa kama yalivyokuwa matakwa ya Prigo
9. Je, Prigo hakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na Putin mpaka afikishe ujumbe kwa njia ya kufanya mapinduzi?
10. Kama Prigo alikuwa na nguvu na ushawishi kiasi hiki imekuaje awe mnyonge kwenye kusitisha uasi mpaka kupoteza nusu ya jeshi lake na uhuru wake wa kuishi Russia?
Kama ni Maigizo najiuliza yafuatayo
1. Je, hili igizo lilikuwa na muhimu gani kiasi cha kuingia hasara ya ndege 4, kubomoa barabara kwa kuchimba mitaro, na kulipua depot ya mafuta
2. Je, Putin haoni kuwa iwapo warusi wakigundua hili ni igizo wanaweza kumchukia yeye na serikali yake maana wameleta taharuki isiyo na maana na pia warubani wamekufa bila sababu ya msingi.
3. Je, hili tukio haliwezi kuamsha uasi kwa waliokuwa wanatamani kufanya mapinduzi lakini wakakosa ujasiri wa kufanya hivyo?
4. Russia inafadika nn na igizo la namna hii?
5. Kitendo cha Prigo kutaka kuasi sababu ya Shoigu na CDF wake hakuleti picha mbaya kwa wawili hao kwa warusi?