Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Sio kupata taarifa Ndugu,ni kukonekt dots TU.

Wagner wanapewa silaha na Urusi,
Wagner wanapewa taarifa za kiintelijensia na jeshi la Urusi,
Wagner wanapewa mafunzo ya matumizi ya silaha na jeshi la Urusi,na hata mafunzo ya kijeshi,
Wagner umaarufu wote ni kutokana na logistics za jeshi la Urusi,
Sasa wangwezaje kulishinda jeshi hilo.
Urusi kuna majeshi mengi sana hatari,Kuna Alpha,Kuna spertsnaz,Kuna Vyampel,Kuna Kila aina ya askari maalum.
Wagner Hawa ni wanamgambo TU na wao.
Wagner wako kama 25000 TU hivi,na sio wote wangekua na moyo wa kupigana dhidi ya jeshi jekundu,tufanye nusu wangweka silaha chin hivyo wangebaki 12000.
Je Hawa ndio wangetingisha nchi ya Urusi?
Mkuu kama jeshi la Urusi si tayari kupigana na Wagner, hakuna kazi ya kushinda jeshi hilo... Hivyo ndivyo jinsi ilivyoonekana jana.
 
Mkuu tupo team moja, point yangu kubwa ni kwanini Urusi na Putin walimuacha Prigozhin akawa mkubwa kiasi cha kutishia uhai na usalama wa Urusi kwa kujaribu kufanya coup? Nilitoa mfano wa Marekani anavyompa misaada ya kila aina Zelensky na Ukraine ila kila siku haachi kuwadukua ili isije kutokea siku akapigwa kwa silaha zake mwenyewe ama maslahi yake yakaharibiwa kwa kiburi kinachotokana na misaada yake mwenyewe.
Kujifunza hata kwa adui sio vibaya, na kumbuka tukio la jana halikuanza ghafla, hii shida imeanza nadhani wakati ule Wagner na Urusi wanaelekea kuichukua Soledar kwahiyo watu serious walitakiwa wawe wameshamuweka kwenye mstari tokea wakati ule.
Unawezaje kwanza ku critize wizara yako ya ulinzi katikati ya vita na ukabaki salama? Ni kwanini nyie wenzetu hamuoni tatizo kwenye namna Putin na Urusi walivyomu handle Prigozhin??

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
Mimi napingana na wewe na wengine wengi wenye hoja kama Yako kwa swali langu hili,
Je unajuaje kama vyombo vya usalama vya Urusi havikua vinamdukua Prigo?
Unajua kazi ya military Intelligence ndani ya jeshi,ama hyjua kazi ya GRU,FSB na vyombo vingine vya usalama wa Urusi?
Je hujui kua hata waziri wa ulinzi wa Urusi anaangaliwa achiliabmabali wakuu mbalimbali wa vuyombo na tasisi mbalimbali wanaangaliwa kwa karibu,achilia mbali Urusi hata USA na nchi nyingine,Urusi kweli washindwe kumchunguza Prig?
Kwa kifupi amekua akichunguzwa tokea akiwa mpishi wa Rais Putin.
Shida Yako wewe unataka wawe wanatoa taarifa kua anachunguzwa.haiko hivyo.
 
Kwa hoja yako ya kushindwa kumaliza vita ndani ya muda mfupi tufanye Russia siyo supa pawa. Kwa kutumia hoja hiyo hiyo tumpime supa pawa unayemuamini.
Je marekani ilimaliza vita pale vietnam baada ya muda gani? Je supa pawa alimaliza vita pale Korea baada ya muda gani? Je pale Afghanistan, je Iraq?
Kwa hoja yako inamaanisha hata marekani siyo supa pawa.
Akikujibu nialike tafadhari,ili TU nijue kajibu hoja au viojamaana sio kwa fact hizo ulizompa.
 
Mahaba ni kitu kibaya Sana , Kwa kweli Kuna makundi ya wamarekani yalionekana Kila Kona yakishangilia ushindi wa bule, Leo wamekuwa wa pole. inawezekana Urusi ikaanguka lakini sio Leo.kadili unavyopigana na vikwazo unaongeza uzoefu na unajifunza mbinu mpya. Kwa maoni yangu urusi anakwenda kuwa na jeshi na vifaa Bora zaidi. Kitu kingine ambacho tunakosea ni kutoa maoni KUTOKANA na hisia zetu kuliko hali halisi
 
Wewe huamui hapa. Swali lilikuwa kuhusu NATO na Iraki. NATO haikuhusika Irak. Ukiona tofauti, lete ushahidi (azimio, tarehe)
Nato haikuhusika Iraq, umejibu vyema kabisa sasa kama Marekani iliamua tu kuipiga Iraq na hakuna aliemzuia wala kumlaumu wala kumpa silaha iraq inakuwaje leo Russia anonekana gaidi na mwonevu pale ukrane? Kwanini hatukuona marekani anafanya makosa ya kibinadamu wakati ule, kwanini marekani hakuwekewa vikwazo wakati ule? Je damu ya watu wa Iraq haina thamani kama damu ya watu wa ukrane?
 
Yani jana kuna muda niliamua kumpa mtoto simu aingie you tube ili amalize bando nisiweze kuingia kujua nini kinaendelea.ila haikupita hata dakika 2 nikashindwa kuvumilia, nikachukua kuangalia tena kuwa Prigozhin kafika wapi[emoji23][emoji23][emoji23].


Yani Moscow ingekuwa karibu kama vile unaenda zanzibar ningekuwa nishafika nimechukua AK-47 kwa ajili ya kujitolea kulinda ikulu.


Mwili wangu mpaka leo haupo sawa kabisa.nilikuwa nasikia kuzunguzungu na mapigo ya moyo kuwa chini sana kwa hali iliyotokea jana
Pole sana!!! Mimi Ile taarifa nilipata mara ya kwanza kutoka notification ya Sputniknews(nimesubscribe)! Nikashtuka. Nikawaza, kama Sputniknews wametoa taarifa hii basi western Media hii habari itakuwa Sasa ndiyo habari inayotanda na watakiwa na taarifa za kina kwa sababu yawezekana PMC wamefika bei.

Mbio, nikaenda BBC nikakuta hakuna kabisa habari hiyo, huyo CNN, Aljazeera, DW kote hola. Sasa nikarudi RT ndiyo nao wakawa wameweka nembo Yao nyekundu ya breaking news. Na habari ikiwa shallow! Nikaanza kuchambua kuwa hii inaweza kuwa mchezo!! Baada ya lisaa nikarudi BBC nao Sasa wakawa wameweka habari hiyo, kusoma maelezo kwa jicho la tatu nikagundua nao hawako well informed na nikama wamepigwa na butwaa nao !

Hapo kidogo wasiwasi ukapungua.
Baadaye nikapata taarifa kutoka hizi micro-blog kuwa helicopter ya Russia imeangushwa nikashtuka Tena...Baadaye Putin akaenda hewani....na nikaona Putin yupo firm wakati anaeleza suala hilo. Nikajua Sasa mchezo umeisha.

Ni kweli wapenda amani na ustaarabu wa kuheshimu uumbaji wa Mungu tulistuka kidogo.
 
Nato haikuhusika Iraq, umejibu vyema kabisa sasa kama Marekani iliamua tu kuipiga Iraq na hakuna aliemzuia wala kumlaumu wala kumpa silaha iraq inakuwaje leo Russia anonekana gaidi na mwonevu pale ukrane? Kwanini hatukuona marekani anafanya makosa ya kibinadamu wakati ule, kwanini marekani hakuwekewa vikwazo wakati ule? Je damu ya watu wa Iraq haina thamani kama damu ya watu wa ukrane?
Mkuu sijui wewe uliona au hujaona nini. Mimi niliona vita ya pili ya Marekani huko Iraq ilikuwa vibaya na jinai. Tofauti na vita ya kwanza iliyokuwa tenda halali la kumwadhibu mwuuaji mbaya aliyewahi kumshambulia jirani mdogo.
 
Shiogu kajichukulia Wagner kiwepesi sana[emoji23][emoji23][emoji23].

Prigozhin itakuwa kaambiwa asimamie Wagner waliyopo Africa na nchi zingine.
Kuna kauli inasema "muda mwengine ili utatue tatizo, anzisha tatizo"

Madhumuni ni kwamba utaficha dhamira yako ni ipi!

Prigozhin anatumika kukamilisha mipango ya Urusi kwa maana ya justification.

Sasa Prigozhin ameshatumika ili Russia a-justify mipango yake ili atimize malengo yake.
 
Tena nakuhakikishia kua hakuna wakati vyombo vya usalama vya Urusi viko makini kama kipindi hiki.wanajua kutakua Kuna njama nyingi mno.toka west.
'Wagner mutiny' japo ilikuwa ya muda mchache imeonyesha huo umakini haupo.
 
Niwape story ya Sergey Naryshkin (mkuu wa ujasusi wa nje SVR) na Vladimir Putin walivyokutana.

Basi wakuu, bwana Naryschkin akiongea katika mahojiano ya nadra na televisheni mwaka 2018, alidokeza jinsi alivyokutana na Vladmir Putin.

Miaka ipatayo 40 ilopita, hawa mazee Naryschkin na Putin waligongana tu pale kwenye jumba kubwa jeupe maarufu kama The Big House.

Hio ni moja ya makazi na ofisi za shirika la Ujasusi la Russia (zamani KGB) sasa FSB mjini Leningrad.

Akiwa ndo kwanza amemaliza masomo yake ya ujasusi katika chuo cha KGB kiitwacho Felix Dzerzhinsky, Naryshkin alikuwa akitembea kwenye viwambaza vya ofisi hizo alipokutana na Putin ambae wakati huo tayari (mwamba) alikuwa akifanya kazi idara ya ujasusi wa nje.

Naryschkin akaendelea kusema kuwa baada ya hapo wakawa marafiki na walipelekwa pamoja kwenye chuo maalum cha ujasusi wa nje kiitwacho Red Banner Insitute.

Naryschkin akasema walicheza michezo ya kwenye barafu (skydiving) na pia kutumia miavuli kuruka angani (Parachute) na alishangaa sana uwezo wa Putin wakati ule.

Baadae mazee hawa walianza kuwa na matamanio ya nafasi za juu serikalini na Putin akaenda kusoma sheria huku Naryshkin akisomea uhandisi wa teknolojia ya sayansi.

Hakuna taarifa zozote zaidi za wapi hawa wawili na yule mazee mwingine Nikolai Patrushev wamefanya kazi zao zaidi ya KGB.

Russia wana mfumo wa kuchagua viongozi wa baadae kupitia kitu chaitwa Checkist ambapo wale wanofanya uzuri katika masomo na wanoaminiwa hupelekwa kusoma Red Banner Institute.

Hapo Red Banner Institute Putin na Naryschkin walikuwa wakiitwa majina maalum yaani codenames Putin akiitwa Kamaradi Platov na Naryschkin akiitwa kamaradi Naumov, huku Putin akisomea masomo ya kigeni kama kijerumani na Naryschkin Kifaransa.

Baada ya masomo mazee hawa wakadondoshwa kazini Putin akipelekwa Dresden Ujerumani mashariki na Naryschkin akitupwa Brussels ambako ni kitovu cha NATO na taasisi zingine za mataifa ya Ulaya.

Kazi kubwa ya Naryschkin akiwa Brussels ni ujasusi wa hali ya juu akiwaajiri vijana kadhaa (kutokana na uzoefu wake wa lugha ya kifaransa) na taaluma yake ya sayansi na teknolojia akawa apata taarifa lukuki za siri za mataifa ya Ulaya magharibi na kuzepeleka Moscow kwenye viwanda vya kijeshi.

Hivyo wakati Mickhail Gorbachev akiwa ahongwa na mataifa ya magharibi na Marekani na kisha kusababisha kuanguka kwa ulokuwa umoja wa kisovieti USSR na uchumi wake mwishoni mwa miaka ya 1980, siri nyingi za kiteknolojia tayari zilikuwa mikononi mwa vijana wa KGB na kuanzia hapo wakaweka msisitizo kuwa agenda kuu ni kuhakikisha kuwa ujajusi wa kiteknolojia uwe juu ya ujasusi wa kisiasa.

Baadae jasusi mwenzie na Naryshckin katika ubalozi wa Russia mjini Brussels akaamua kukimbilia ubalozi wa Marekani na akawa mtoa taarifa kwa CIA na baadae mhaini huyo alikuja kugundulika kuwa ni bwana aitwae Igor Cherpinsky na baadae akapotelea kusikojulikana hadi leo yeye, mkewe na mtoto wao mdogo.

Akiongea leo Naryschkin asisitiza uzalendo na kuipenda nch yako na kuwa tayari kujitoa mhanga. Kidiplomasia Naryschkin ni mpole katika matumizi ya lugha kali kwani Putin ni tofauti. Kuna wakati Putin aliwahi kutoa vitisho kwa wasaliti wa nchi kwamba wataipiga ndoo.

Baada ya kuanguka kwa USSR mwaka 1991, Putin na Naryschkin waliacha kazi SVR na kwenda kufanya kazi katika manispaa ya mji wa St Petersburg. Waliendelea na shughuli zao lakini ni Putin ambae alikuwa na nia na uraisi wa Russia akaenda kuwa raisi wa nch hiyo. Baadae akiwa katika awamu ya pili mwaka 2004 ndipo alipomkumbuka Naryschkin na kumpa nafasi katika ofisi ya raisi.

Naryschkin mwaka 2007 akaja kuwa waziri mkuu wa Russia na mwaka 2008 Medvedev alipobadilishana nafasi na Putin na kuwa raisi huku Putin akiwa waziri mkuu, Naryschkin akateuliwa na Medvedev kuwa katibu mkuu ofisi ya raisi yaani chief of Staff.

Lakini wachambuzi wengi waliona hilo la Putin kumshauri Medvedev kumchagua Naryschkin kuwa katibu mkuu kiongozi (bila kufahamu) kufahamiana kwa Putin na Naryschkin na kumbe Putin alitaka Naryschkin amwangalie Medvedev twaita -" To keep an Eye.

Huo ndo ukawa mwanzo na kuimarika kwa kundi la Putin liitwalo "Sloviki" ambalo ni kundi kubwa la majasusi pamoja na wabunge na watu wenye fedha za kutisha waitwao "Oligharchs". Hawa ni pamoja na akina Roman Abramovich na mkuu wa sasa wa Wagna Group Yevgenvy Prigozhin.

Naryschkin akapanda na kuwa spika wa bunge la Russia maarufu kama Duma na hapo ndipo sera ya mambo ya nje ya Russia ilipoanza kushika tama. Hivyo Russia wakaanza kurudisha madai ya kutaka "Mother Russia" au "Russia Motherland" na katika kujiweka sawa kijiografia huku wakiwa na taarifa zote za mipango ya NATO kujitanua upande wa mashariki pembezoni na Russia wakaanza na kuichukua Crimea mwaka 2014.

Mwaka 2016 raisi Putin akampa kazi mpya Naryschkin ya kuongoza idara ya ujasusi wa nje ya Russia SVR na kuonekana amefurahia kurudi katika aneo lake la kujidai la biashara ya ujasusi. Tangia hapo SVR imekuwa wazi na Naryschkin amebadilisha idara kuwa rafiki, yenye nguvu na inofanya shughuli zake kitaalam. Tovuti ya SVR imekuwa na habari mpyampya. majasusi wa zamani wamekuwa wakiandika vitabu vya kijasusi na kuwekwa katika maktaba maalum, na hata vipindi vya runinga na filamu vimekuwa vikiruhusiwa kuchukua picha na filamu zinohusu idara hiyo.

Zipo tetesi kuwa Naryschkin huenda akateuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje wa Russia kuchukua nafasi ya Sergey Lavrov ambae nae atazamiwa kustaafu. Lakini yote yategemeana na anavowaza raisi Putin.

NB: Habari nimeitafsiri na kuifupisha kutoka katika kijarida kiitwacho SpyTalk.
Ngoja nieke kituo
 
Ule sio mchezo wa kuigiza ,ni jambo la hatari sana lililotokea kwa uongozi wa russia kwa ujumla,na tukubaliane kuwa kuna mahala putin amefeli,kugundua ukweli ni moja ya njia ya kujisahihisha ,kinyume chake ni kujidanganya.
Hivi wewe hapa ndo umendika Nini?
Maana shida ya mswahili ni kjiifanya unajua Kila kitu.
Hebu rudia kusoma ulichoandika.
 
Ule sio mchezo wa kuigiza ,ni jambo la hatari sana lililotokea kwa uongozi wa russia kwa ujumla,na tukubaliane kuwa kuna mahala putin amefeli,kugundua ukweli ni moja ya njia ya kujisahihisha ,kinyume chake ni kujidanganya.
Upo sahihi kabisa.... Putin hana udhibiti kamili wa nchi kama wengi wanavyodhani ndio maana hata Wagner walipata ushirikiano kutoka kwa askari wa Urusi na Prigozhin alishangiliwa mno na wakazi wa hiyo miji iliyotekwa japo alikuwa tayari anasakwa na FSB kwa kuhatarisha usalama.
 
Pole sana!!! Mimi Ile taarifa nilipata mara ya kwanza kutoka notification ya Sputniknews(nimesubscribe)! Nikashtuka. Nikawaza, kama Sputniknews wametoa taarifa hii basi western Media hii habari itakuwa Sasa ndiyo habari inayotanda na watakiwa na taarifa za kina kwa sababu yawezekana PMC wamefika bei.

Mbio, nikaenda BBC nikakuta hakuna kabisa habari hiyo, huyo CNN, Aljazeera, DW kote hola. Sasa nikarudi RT ndiyo nao wakawa wameweka nembo Yao nyekundu ya breaking news. Na habari ikiwa shallow! Nikaanza kuchambua kuwa hii inaweza kuwa mchezo!! Baada ya lisaa nikarudi BBC nao Sasa wakawa wameweka habari hiyo, kusoma maelezo kwa jicho la tatu nikagundua nao hawako well informed na nikama wamepigwa na butwaa nao !

Hapo kidogo wasiwasi ukapungua.
Baadaye nikapata taarifa kutoka hizi micro-blog kuwa helicopter ya Russia imeangushwa nikashtuka Tena...Baadaye Putin akaenda hewani....na nikaona Putin yupo firm wakati anaeleza suala hilo. Nikajua Sasa mchezo umeisha.

Ni kweli wapenda amani na ustaarabu wa kuheshimu uumbaji wa Mungu tulistuka kidogo.
Hakuna neno hata moja litakaloshindwa kutimizwa US wanalazimisha Mungu Ni mwema.
 
Back
Top Bottom