Nashukuru kwa mchango wako ingawa picha kadhaa ulizoambatanisha hazionekani, nadhani kuna makosa ya kuzi-upload! OK!
Hoja yako ninakubaliana nayo kabisa kuwa itikadi ya neo-Nazism nchini Ukraine ipo. Kuna vikundi mbalimbali pamoja na taasisi zenye mrengo huo ambazo zimekuwa zikitumia nembo, kauli na ishara za Kinazi, kitu ambacho kimekuwa kikitumika na Urusi kama sababu ya kuivamia Ukraine kupitia hicho kinachoitwa denazification.
Lakini, suala hili la "neo-Nazism" ni suala linaloikabili Ukraine pekee? Je, kundi hili lenye itikadi kali lina ushawishi kiasi gani nchi Ukraine hasa katika vyombo vya maamuzi yanayohusu masuala muhimu ya kitaifa?
Vipo vyama vya siasa nchi Ukraine vyenye mrengo huo vinavyoungwa mkono na wafuasi wa itikadi kali za Unazi mamboleo lakini havijawahi kupata uwakilishi wowote wa maana katika utawala wa Ukraine hata katika chaguzi ambazo zimewahi kufanyika hivi karibuni. Iko hivyo hata katika mataifa mengine barani Ulaya ikiwemo Urusi, ambayo yana vyama vya siasa vya mrengo huo lakini havina ushawishi wa maana wa kisiasa na kiutawala.
Tukiachana na hilo, zipo taasisi za neo-Nazism nje ya vyama vya siasa zinazojiendesha kwa kujitegemea.
Ukifanya utafiti wa kutosha, hii itikadi ya neo-Nazism imeenea karibu nchi zote za Ulaya na hata Marekani pia. Vipo vyama halali vya siasa pamoja na taasisi mbalimbali zenye mrengo huo. Nimetoa mfano wa hiyo taasisi moja ya RIM ambayo ina ushawishi mkubwa tu kimataifa. Pia, ina mpaka kibali cha kumiliki jeshi na ku-supply wapiganaji kwaajili ya missions za serikali ya Urusi.
Kumbuka kuwa ni Urusi hiihii ambayo inasema kuwa utawala wa Ukraine ni wa Kinazi. Kuna viashiria vingi vya uwepo wa wafuasi wa itikadi hii nchini Ukraine kama ambavyo vimekuwepo katika nchi zingine lakini bado sijapata hoja yoyote yenye uthibitisho kwamba utawala hasa wa Ukraine ni wa Kinazi. Ndio maana nimeibua hoja hapa kuhusu matumizi ya taasisi hizi kwa maslahi ya serikali za nchi husika.
Ni sahihi sana unaposema kuwa wanasiasa wana mambo mengi nyuma ya pazia, ingawa mengine yapo hadharani kabisa yanaonekana. Nashukuru!