Watakuja kukwambia BRICS, gesi na mafuta. Putin ni authoritarian na kawaida ya hawa ukiwaambia ukweli wanakutimua kazi, ukishafutwa kazi kwenye defense au intelligence community ya Russia ukiwa na cheo kikubwa basi wewe life expectancy inashuka.
Zelensky anakubalika sana na jeshi na ni mhunimhuni tu wala hajakaa kimadaraka, viongozi wake hata wa kijeshi wanamuelewa na hawamuogopi. We tazama wanadiplomasia aliotuma waende Belarus wengine wamevaa kapelo wengine majaketi ya mistari tofauti na wanyuka suti. Zelenskiy yuko approachable huna haja ya kumdanganya, jeshi lilimuhakikishia linaweza mount opposition mradi aweze kujiliza wampe silaha na alivyo Myahudi basi hicho ni kipaji chao. Ndio maana Marekani ilitaka imtoeoshe akagoma.
Wakati huo Putin intelligence community yake ilimwambia Ukraine kuna neo-Nazis tutawapiga, Zelenskiy hakubaliki na raia watalipokea jeshi la Urusi. Mambo yalipobadilika Putin akataka jeshi la Ukraine limpindue Rais wao.
Urusi haikujipanga, Ukraine tangu wanajeshi wake mwaka 2014 wajisalimishe pale Crimea bila kurusha hata risasi, then Donetsk na Luhansk zikatwaliwa basi nchi imejifunza kupambana. Haiwezekani ilikuwa inafanya mazoezi bure tu na kutumia gharama nyingi. Hata mauzo ya silaha iliyokuwa nayo imestop mfano Congo DRC ilikuwa imeagiza vifaru modification ya T-64 ila Ukraine wanazitumia wenyewe