Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kaka unajaribu kupinda maneno na habari. Hakuna neno kutoka Marekani (jinsi unavyodai) la kuthibitisha kuwepo kwa maabara ya kuunda silaha za kibiolojia.
Umoja wa Mataifa (kitengo kinachochungulia silaha) ulieleza hadharani hakuna dalili ya kuundwa kwa silaha za kibiolojia katika Ukraine.
Al Jazeera (isiyo kimagharibi) imeita madai ya Urusi fake (conspiracy theory..)

NATO haiko Ukraine (kama ingekuwepo Putin angeogopa kuingia, tazama Estonia ambako NATO iko)
 
Ndugu yangu. Hivi unajua Kama hayo madege na makombola yanayotumika.Niyakipindi Cha USSR, yaaani makombola ya Urusi yenyewe bado hayajatumika. Maana zile stop za zamani ndio zinafanuiwa usafi wataalamu wa silaha ( weapons technician) wameshauri zile silaha za miaka ya (1956 mpaka1980) ndio zitumike.

Yaaani huo Moto unao uona ilitakiwa WANATO ndio wapigane nao miaka ya 90s, Sasa kwa wataalamu wa mambo wanakwambia hayo makombola yanayopigwa ni yakizamani ambayo hiyo technician council imeshauri yaondolewe ili maghara yafanyiwe usafi waanze kuupakia mzigo mpya.

Just imagine kombola linapigwa more than 400 miles Tena na madege ya kizamani alafu linahit target more than 95%. Je likipigwa Iskander2Er2008 itakuaje au. Wao wamerika wanakwambia urusi waijuayo bado haijatumika nguvu zake.
Kwa maana nyingine Russia imetumia wapiganaji kutoka huko huko Ukraine majimbo ya mashariki na jamhuri za ndani za kusini mwa urusi, walio Anza kukusanywa kwa muda kidogo ili kuja kuiangueha serikali dhalimubya Kiev. Wakapewa na masilaha ambayo taifa tukufu la Urusi limeona hazina Tena thamani Katika stop zao.mimi nimewaambia pro NATO waniambie 4th+ au 5th generation ya silaha iliyo tumika Ukraine ndio na Mimi nianze rasmi kubishana.
Pia mkumbuke silaha wanaso zikimbia na kuzitelekeza Ukraine Russia anazichapa Z au V Kisha zinaendelea na mapigo kutokea upande wa Urusi, simm jionea jinsi walivyo ziacha makambini wilaha nyingi. Mrusi anakamata regiment ya vifaru alafu anaingia nazo mzigoni Kisha Ukraine wakipiga vifaru kumi Kati ya zaidi ya 80 vilivyo tekwa Basi inakua ndio Habari kuanzia CNN, BBC, na wengine wengi wengitu.
Kwa tafsiri ya kivita kuupiga mkoa wa lviv Ni kutoa onyo kua chochote popote panapigika. Hivyo supporters wanaweza kushambuliwa Bora wakae mbali na mziki mziki.
 
Duh....Asante Sana Ndugu ...thank you ...
 
Ndiyo kaka! Unaelewa unachoandika? Maana yake ni Jeshi la Anga la Kirusi lilishindwa kunyamazisha utetezi wa anga wa Ukraine.
Utetezi huu unafanywa na roketi za Kirusi aina ya SAM. Waliharibu sehemu kubwa, lakini walishindwa kumaliza kazi. Ambayo ni udhaifu
Menginevyo Warusi wanapambana na roketi ndogo za mbegani aina ya stinger. Hizi zinawalazimisha kukaa juu ya mita 3000, ambayo inaongeza ugumu wa kulenga vema. Na kutumia ndege zaidi wakati wa usiku. Pamoja na hayo idadi ya mabomu janja (intelligent bombs) waliyo nayo imeshangaza maana ni ndogo. Wanatumia mara chache, kama leo mashambulio ya Lviv.
Menginevyo wanapaswa kutumia mabomu ya kawaida hovyo, pamoja na mizinga, ambayo yote yanaleta uharibufu mkubwa ya miji na makazi.
Je wataweza kuvunja moyo wa Waukraine au kuongeza chuki tu ili warithi vita ya guerilla baadaye?
HAo wanaodai Jeshi la Kirusi linaendele polepole kwa sababu wanataka kulinda watu raina na kuepukana na uharibifu mkubwa: muangalie tu picha za mji wa Mariupol. Wala idadi ya watu raia waliuawa huko (karibu 2000 ) wala uharibifu wa nyumba za kawaida ina dalili yoyote kwamba jeshi la Kirusi linalenga kepukana na uharibifu.

Kama Kiev bado afadhali, kwa sababu badu hawakufika karibu
 
Viumbe waliostaarabika?? Machoni pangu hawaonekani Kiarabu sana (siyo maana ya ku-staarabika" ni kufanana na Waarabu?). Hijabu imepungua kidogo, au?

Lakini kupinga mauaji pamoja na au bila hjabu hakika ni tendo jema!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…