Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?


T14 Armata unaitwa kujibu maswali
 

Ukraine ni hapo hapo jirani wa Urusi, sasa unawaita waarabu waje wakusaidie vita vya mtaani kupigana na ndugu zako.
Ni kama leo muachike na Zanzibar kwenye muungano halafu muwafuate kupigana nao, kwenye mitaa yao, Waswahili wenzenu tena ndugu kabisa, kisa wanataka kujiunga muungano na Oman, muanze kuomba usaidizi Jamaica.....wapi na wapi....haviendani.
 
Dead on arrival, alafu naona kuna watu wamelike huu ujinga. How can those
moja ya sababu zinazokwamisha hizi jumuiya kama SCO na BRICS ni kwamba baadhi ya members wanataka ziwe ni zakiuchumi na kibiashara na si kisiasa, mfano mchina aliinjinia kuanzishwa kwa AIIB, Hii bank ni km inataka kuja kushindana na western dominated institutions km WB na IMF lakin inaendeshwa km institution zngne za kimataifa na ina members wengi tu ambao ni mataifa makubwa ndani ya EU pamoja na australia na wana voting power kubwa tu humo so ni pure bussiness but kuna mataifa km IRAN au RUSSIA wao wana mtazamo mwngine wanatk hizi institutions zinazoanzishwa na wao huku ziwe na political role pia mfano kpnd hiki urusi wako sanctioned basi zimprotect against sanctions kitu ambacho ni tofauti maana baada ya hizi sanctions AIIB imesimamisha baadhi ya dealing zake urusi ila si kwakumsapoti marekani au kumuumiza urusi bali ni sababu za kibiashara, so china na urusi wana ideologies zinazofanana but sehemu zingine wana mitazamo tofauti kabisa ya jinsi gani dunia iende
 
Akijibu unitag mkuu
 

Mzozo wa Ukraine: Mashambulio matatu ya Urusi mtandaoni yanayotia hofu nchi za Magharibi​


Rais wa Marekani Joe Biden ametoa wito kwa makampuni na mashirika ya kibinafsi nchini Marekani "kufunga milango yao ya kidijitali", akidai kuwa ripoti za kijasusi zinaashiria kwamba Urusi inapanga kushambulia Marekani mtandaoni.

Mamlaka za mtandao nchini Uingereza pia zinaunga mkono wito wa Ikulu ya White House wa "kuongeza tahadhari za usalama wa mtandao", ingawa hakuna hata mmoja aliyetoa ushahidi wowote kwamba Urusi inapanga shambulio la mtandao.

Urusi iliwahi kusema kuwa shutuma hizo ni za "Russophobic" -kuogopa Urusi.
Hahata hivyo, Urusi ni nchi yenye nguvu kubwa zana hatari mtandaoni, na wadukuzi wenye uwezo wa kfanya mashambulizi makubwa mtandaoni.

Ukraine haijatetereka na mashambulio ya Urusi mtandaoni lakini sasa wataalamu wanahofia Urusi huenda ikalipiza kisasi kwa kuwafanya mashambulizi ya kimtandao dhidi ya washirika wa Ukraine.

"Onyo la Biden linaonekana kuwa sawa, haswa wakati nchi za Magharibi zilipotangaza vikwazo zaidi, wanaharakati wa udukuzi wanaendelea kujiunga na vita, na masuala uvamizi huo yanaonekana kutopangwa," anasema Jen Ellis kutoka kampuni ya Rapid7 inayojishhughulisha na usalama wa kimtandao.
​
Hii ni udukuzi unaoogopwa zaidi na wataalamu.
BlackEnergy - ililenga kushambulia miundombinu muhimu

Ukraine mara nyingi huelezewa kama uwanja wa michezo wa udukuzi wa Urusi, ambayo imefanya mashambulio yanayoonekana kujaribu mbinu na zana.

Mwaka 2015 mkonga wa umeme wa Ukraine ulikatizwa na shambulio la mtandao linalofahamika kama BlackEnergy, ambalo lilisababisha kukatika kwa umeme kwa muda mfupi kwa wateja 80,000 wa kampuni ya huduma magharibi mwa Ukraine.

Takriban mwaka mmoja baadaye shambulio lingine la mtandaoni lililojulikana kama Industroyer iliyokatiza umeme wa Kyiv, mji mkuu wa Ukraine, kwa karibu saa moja.

NotPetya - Uharibifu usioweza kudhibitika
NotPetya inakisiwa kuwa ni shambulio la gharama kubwa zaidi la mtandaoni katika historia na mamlaka za Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya zinahusisha mashambulio hayo na kundi la wavamizi wa kijeshi wa Urusi.

Programu hiyo ya uharibifu ilifichwa katika programu ya software maarufu ya uhasibu inayotumiwa nchini Ukraine, lakini ilienea duniani kote kuharibu mifumo ya kompyuta ya maelfu ya makampuni na kusababisha uharibifu wa takriban dola bilioni 10.​
 
Fake news
 
Hatujalinganisha. Tunachopinga ni kuibeza Urusi kuonyesha kama vile Afrika haijanufaika nayo kwa chochote.
 
Unagombana na jirani, waliomshawishi aanzishe ugomvi wanamsaidia.
Na wewe upo ukipata wa kukusaidia unaungana naye mnapigana kila mtu anajua nyuma yangu siwezi kupigwa kuna mshirika wangu atapambana upande huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…