Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

SmartSelect_20220324-122437_Twitter.jpg
 
Sasa RT inamilikiwa na serikali ya Urusi unategemea nini?

New York Times ni private owned hakuna mamlaka zinazolazimisha nini kisemwe.
NYT iko public traded, hawalazimishwi kusema uongo. Mimi ni mfatiliaji wa RT kuliko hata CNN, NYT na media nyingine za Westerns ila RT ujinga wao ni kutoa petty issues, huwa habari zao zinapuuza ajenda kubwa zinatoa mambo irrelevant na ya kawaida. Aljazeera inaizidi mbali sana RT, hata documentaries za Aljazeera ni next level
View attachment 2161974
Vyombo vya magharibi hata kama ni private, kwenye mambo yenye maslahi na nchi Yao basi huwa na mlengo mmoja!
 
wataalam.mtuelezee statement y jana ya putin kuwa sasa hatakubal kuuza mafuta yake ila alipwe kwa rubble.
huyu mwamba ana plan gan kichwan mana rube naona imeanguka ki exchage rate
Natamani nielewe pia PUT IN kalenga nini hasa
Maana mpaka sasa najua anamalengo mazuri ila sijajua atatoboaje
 
***** mpaka muda huu chakula kilichopnda urusi ni sukari tena sio sana

kwamujibu wa profesa musa mtanzania anaye fanya kazi kwenye chuo kimoja huko urusi ambapo jana alihojiwa na dw kiswahili anasem
a

nukuu: "warusi wengi wanaiunga mkono serikali mfano angalia tamasha la juzi pale crime maandamano yaliyo fanyika siku za mwanzo yale yalikuwa madogo ukilinganisha na jumla ya idadi ya warusi wote mimi naona kama hakukuwa na maandamano bali ni kelele"
alisema musa
Naongezea nyama alisema watu walioshiriki yale maandamano hawakuzidi hata watu khamsini 50
 
Siku moja baada ya Ujumbe wa mabalozi wa nchi za Ulaya nchini Tanzania kuitaka Tanzania na nchi nyingine za Afrika kupaza sauti kukemea uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, nchi hiyo imetoa msimamo wake leo na kusema yenyewe haifungamani na upande wowote.

View attachment 2162649Msimamo huo unapigiwa mstari na uamuzi wa taifa hilo la Afrika Mashari la kutokupigia kura azimio la baraza Kuu la Umoja huo, UNGA kupitisha lililopitishwa mapema mwezi huu, kuitaka Urusi kusimamisha mara moja mashambulizi yake dhidi ya Ukraine na kuyaondoa majeshi yake katika nchi hiyo.

Waziri wa Masuala ya kigeni wa nchi hiyo, Liberata Mulamula amesema kwa miaka mingi sasa Tanzania inaamini katika kutafuta muafaka na marudhiano kwa kutumia njia ya diplomasia ili kumaliza migogoro.
Kutokana na muafaka na maridhiano kutopatikana katika mzozo wa Urusi na Ukraine, Waziri Mulamula anasema: “ndio maana katika kupiga tukaamua kutofungamana na upande wowote, lakini ilikuwa sio kutofungamana na pande zote mbili lakini ni kutoa ujumbekuonyesha kwamba sisi msimamo wetu na sera yetu na msingi wetu wa sera ya mambo ya nje ni kutokufungamana na pande zozote hasa katika hali kama hii”, alisema Mulamula.

Tanzania ilikua miongoni mwa mataifa 35 wanachama wa Umoja wa Mataifa ambayo hayakupiga kura kuunga wala kukataa azimio hilo lililoungwa mkono na mataifa 141, huku mataifa matano ya Urusi, Belarus, Syria, Korea Kaskazini na Eritrea, yakipinga azimio hilo.

Hapo jana ujumbe wa Mabalozi wa nchi za Umoja wa Ulaya nchini Tanzania pamoja na kuzitaka nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kupaza sauti zao kulaani uvamizi huo wa Urusi, waliitaka pia Urusi kumaliza mzozo wake na Ukraine bila kupigana vita.​
Yes kama hivo, hatutaki upande sie [emoji119][emoji119][emoji119] wachokonoane wao kisha watuchagulie wakuungana nae wapi na wapi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wamelikoroga wao wenyewe ni uamuzi wao wenyewe kumwaga au kunywa wenyewe huko hukoo...
 
Nchi za Jumuia ya Ulaya zapigwa daflao, kiwewe, na kuchanganyikiwa kufuatia tangazo la Putin kuziuzia nishati zake kwa sarafu ya Russia.

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Robert Habeck asema atajadiliana na nchi zingine za EU kupata jibu la tangazo hilo.

Waziri mkuu wa The Netherlands Mark Rutte amesema muda zaidi wahitajika kufafanua matakwa ya Russia.

========

SmartSelect_20220324-120336_Chrome.jpg
Screenshot_20220324-120744_Chrome.jpg
Screenshot_20220324-120841_Chrome.jpg
 
Sijui hata anatumia strategy zipi kupiga hii Vita.
Kwenye uwanja wa vita hakuna kitu kigumu kama kusonga mbele kwenye medani za kisasa, kwa mfano huwezi ku advance kama hauna air supremacy maana maana vikundi vidogo na vikubwa vinakosa ulinzi au msaada hasa vinapozingirwa na maadui, ndio maana unaona regiments za vifaru zinakaangwa Sana, Jana kuna mtaalamu mmoja aliandika humu kuwa soldiers win the battle but logistics win the war, hii ina maana kuwa ili ushinde vita unapaswa kuwa na mikakati Bora kabisa ya uwanja wa medani ndio maana wajamaa wenzetu warusi wanahenya sana kuwabonda ndugu zao wa damu Ukraine. Ushabiki ni hulka yetu watanzania tuvumiliane tu ila ukweli Mrusi kaonesha udhaifu kwenye medani za vita kwa hali hiyo mabeberu hayawezi licha ya kuyatishia nukes ambazo hata yenyewe yanazo
 
Yes kama hivo, hatutaki upande sie [emoji119][emoji119][emoji119] wachokonoane wao kisha watuchagulie wakuungana nae wapi na wapi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wamelikoroga wao wenyewe ni uamuzi wao wenyewe kumwaga au kunywa wenyewe huko hukoo...
Wagombane wao ulaya halafu waturushie sisi na kutulazimisha cha kuamua!!! Wao NATO wapambane na Putin, wasitafute sympathy.
 
Natamani nielewe pia PUT IN kalenga nini hasa
Maana mpaka sasa najua anamalengo mazuri ila sijajua atatoboaje
Nachoamini hutojua chochote zaidi ya kusoma au kuelezwa fikra za watu tofauti tofauti kulingana na mwenendo husika lakini nini anawaza utakiona baada ya kile kitu kufanyika.

Kuna vita ya kiuchumi upande huo so sio rahisi mtu kuonesha 'karata' zake kwa adui yake ya kile nini anaenda kufanya 'next'.

NATO wanateam yao ya mipango na naamin Russia vivo hivo wana team yao ya mipango kwenye hilo linaloendelea.

Njoo tunywe Al kasusu Mujarrab tusubir tuone nan atapoteana Dk 90 zikiisha. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa muda mfupi bei zitapanda, bila shaka. Kwa muda mrefu si vile. Uchumi wa kibepari, au tuseme uchumi unaoongozwa na soko unabadilika haraka. Si idara ya serikali fulani. Meli zinaongezwa, meli zinakuwa kubwa zaidi, gharama za kubeba gesi kwa meli zitashuka (jinsi zilivyoshuka tayari).
Kusafirisha gesi kwa bomba ni ghali pia, maana unahitaji kukadiria gharama ya bomba na utunzwaji katika kila m³ ya gesi inayopitishwa. Kadri bomba ni ndefu una gharama za vituo vya kuongeza shinikizo ndani ya bomba. Kuanzia umbali fulani gharama zinaanza kulingana. Hivyo kuna nchi nyingi zinazopata gesi yote au asilimia kubwa kwa meli.
GER kansela kaliweka wazi hili jana wewe nani?
Ingekua rahisi wangeishafanya
 
Wagombane wao ulaya halafu waturushie sisi na kutulazimisha cha kuamua!!! Wao NATO wapambane na Putin, wasitafute sympathy.
Mda sio mref utakuja ule mkwara kama wa kipindi kile kunyimwa misaada ka tulipogomea ushoga... na hivi Mama ndio vile kila kukicha anatembeza bakuli [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].
 
Back
Top Bottom