Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Vyombo vya magharibi hata kama ni private, kwenye mambo yenye maslahi na nchi Yao basi huwa na mlengo mmoja!
 
wataalam.mtuelezee statement y jana ya putin kuwa sasa hatakubal kuuza mafuta yake ila alipwe kwa rubble.
huyu mwamba ana plan gan kichwan mana rube naona imeanguka ki exchage rate
Natamani nielewe pia PUT IN kalenga nini hasa
Maana mpaka sasa najua anamalengo mazuri ila sijajua atatoboaje
 
Naongezea nyama alisema watu walioshiriki yale maandamano hawakuzidi hata watu khamsini 50
 
Yes kama hivo, hatutaki upande sie [emoji119][emoji119][emoji119] wachokonoane wao kisha watuchagulie wakuungana nae wapi na wapi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wamelikoroga wao wenyewe ni uamuzi wao wenyewe kumwaga au kunywa wenyewe huko hukoo...
 
Nchi za Jumuia ya Ulaya zapigwa daflao, kiwewe, na kuchanganyikiwa kufuatia tangazo la Putin kuziuzia nishati zake kwa sarafu ya Russia.

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Robert Habeck asema atajadiliana na nchi zingine za EU kupata jibu la tangazo hilo.

Waziri mkuu wa The Netherlands Mark Rutte amesema muda zaidi wahitajika kufafanua matakwa ya Russia.

========

 
Sijui hata anatumia strategy zipi kupiga hii Vita.
Kwenye uwanja wa vita hakuna kitu kigumu kama kusonga mbele kwenye medani za kisasa, kwa mfano huwezi ku advance kama hauna air supremacy maana maana vikundi vidogo na vikubwa vinakosa ulinzi au msaada hasa vinapozingirwa na maadui, ndio maana unaona regiments za vifaru zinakaangwa Sana, Jana kuna mtaalamu mmoja aliandika humu kuwa soldiers win the battle but logistics win the war, hii ina maana kuwa ili ushinde vita unapaswa kuwa na mikakati Bora kabisa ya uwanja wa medani ndio maana wajamaa wenzetu warusi wanahenya sana kuwabonda ndugu zao wa damu Ukraine. Ushabiki ni hulka yetu watanzania tuvumiliane tu ila ukweli Mrusi kaonesha udhaifu kwenye medani za vita kwa hali hiyo mabeberu hayawezi licha ya kuyatishia nukes ambazo hata yenyewe yanazo
 
Wagombane wao ulaya halafu waturushie sisi na kutulazimisha cha kuamua!!! Wao NATO wapambane na Putin, wasitafute sympathy.
 
Natamani nielewe pia PUT IN kalenga nini hasa
Maana mpaka sasa najua anamalengo mazuri ila sijajua atatoboaje
Nachoamini hutojua chochote zaidi ya kusoma au kuelezwa fikra za watu tofauti tofauti kulingana na mwenendo husika lakini nini anawaza utakiona baada ya kile kitu kufanyika.

Kuna vita ya kiuchumi upande huo so sio rahisi mtu kuonesha 'karata' zake kwa adui yake ya kile nini anaenda kufanya 'next'.

NATO wanateam yao ya mipango na naamin Russia vivo hivo wana team yao ya mipango kwenye hilo linaloendelea.

Njoo tunywe Al kasusu Mujarrab tusubir tuone nan atapoteana Dk 90 zikiisha. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
GER kansela kaliweka wazi hili jana wewe nani?
Ingekua rahisi wangeishafanya
 
Wagombane wao ulaya halafu waturushie sisi na kutulazimisha cha kuamua!!! Wao NATO wapambane na Putin, wasitafute sympathy.
Mda sio mref utakuja ule mkwara kama wa kipindi kile kunyimwa misaada ka tulipogomea ushoga... na hivi Mama ndio vile kila kukicha anatembeza bakuli [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].
 
Baada ya kuzingirwa kwa wiki 4, waUkraine wajipanga msururu kwenye mistari kugaiwa mahitaji ya chakula kama enzi za Ujamaa Tanzania

Wakati hayo yakiendelea, serikali yao yadai ati wanashinda vita😇😇😇

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…