Speed ya Rais Samia inawatisha wengi, wazungu wamefilisika

Speed ya Rais Samia inawatisha wengi, wazungu wamefilisika

Usituharibie funga zetu aisee maana umeandika utumbo hapa 😬😬😬
Funga utaiharibu mwenyewe kwa kinyongo chako. Rais Samia yuko bize na mkakati wake wa kuaachia tabasamu watanzania kabla hayaondoka 2030. Hasemi utani wala porojo, rekodi yake haitafikiwa na Rais yeyote mwenye makundi, ukabila, mpigaji, mwizi na asiyekuwa na hofu ya mwisho. Samia anaamini iko siku atakufa na iko siku atafufuliwa na hukumu. Anataka kuwaonyesha wavimbamacho kuwa wanawake wanajua na wanaweza.

Hawa wavimbamacho walitaka kumchukulia poa lakini hawatasahau walichokutana nacho. Wanzania/watanganyika tulikuwa na rasilimali nyiiingi lakini watanzania hawakuwa na maji kwa miaka 60 ya uhuru; mbwembwe tu za kuongea za akina Nyerere huku wananchi wao wakikosa hata sabuni ya kipande. Kanisa lilijiona Mungumtu, eti linahudumia watu kwenye elimu, matibabu, na misaada kuliko serikali, sasa ni kinyume chake na ndiyo chanzo cha hasira hizi. Serikali ya samia inajenga shule, vyuo, hospitali zenye vifaa kila kona ya nchi hii. Samia anaunda grid ya taifa ya maji, ataleta nishati safi hapa ya bei nafuu na barabara kila kona tena bila tambo nyingi. Pesa yote inayoikusanya anairejesha kwa watanzania wenyewe.

Wavimbamacho tunawahitaji sana kuwepo kwasabu wanaifanya CCM isisale na kubweteka. Bila CCM imara Tanzania itayumba, Nyerere.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya kusoma sana na kuelimika sana. Rais Samia ameelimika sana kuliko marais waliomtangulia. Anatumia elimu yake binafsi kufanikisha mambo ya watanzania wake kwa speed kubwa. Kwa muda mfupi sana amefanya makubwa sana kuliko alivyodhaniwa.

Rais Trump, viongozi wa ulaya na hata wachezaji wakubwa sasa hivi wanakimbilia nchi za Asia kusaka usaidizi na uwekezaji baada ya nchi zao kufilisika. Hata wachezaji wakubwa sasa hivi wameelekeza daluga zao huko Uarabuni kuzoa mapesa.

Tangu tz ipate uhuru tumeimba sana kuhusu wazungu wazungu wazungu, ulaya ulaya na marekani itusaidie na itukopeshe lakini tukaishia hapa tulipo (umasikini wa kutupwa, migogo isiyokwisha na ushoga) na madeni juu yasiyolipika. Viongozi wetu ilikuwa haramu kwao kwenda uarabuni kuomba misaada na mikopo isiyokuwa na riba kutoka kwa waislam ambao hawali riba. Kiongozi kama akioenekana anaelekea kuchukua msaada kutoka kwa waarabu alikuwa anakumbana na waraka na kunywea.

Rais Samia aligundua mapema kuwa wazungu wamefilisika, wanakwenda Asia ya uchina na uarabuni kuomba fedha, gesi, mafuta na wawekezaji. Mama Samia nae akapiga mbio harakaharaka kwenda hukohuko ambako wazungu wanakwenda kuomba ili kuwahudumia watanzania. Huku ni kuelimika kwa hali ya juu sana kwa kiongozi. DP world sasa hivi ndiyo habari ya mjini kwa makusanyo, na sasa anaelekea huko Qatar akazoe mapesa yasiyokuwa na mashariti makubwa na hatari kama yale ya wahuni wetu wa tangia ukoloni hadi leo.

Tumpe moyo aendelee kuwatekenya waarabu hadi wacheke kwa maslahi yetu. Hawa wavimbamacho wetu tuwaombee kwa Mungu awape upofu ili wasione na uziwi wasisikie namna nchi inavyochorongwa kila kona kujengwa.

Fedha sasa hivi iko Asia twendeni huko, dunia yote inaelekea huko.
Hakika wewe ni kavulana!
 
Zezeta katika ubora wako, maboss wako wanatambaa kwenda kupiga magoti huko ulaya halafu wewe kidampa unapanua panua hapa mdomo kama chiriku kusema ulaya wamefilisika?
20260223_100200.jpg
20260223_100204.jpg
 
Kuna chawa mwenzenu hapo , anaomba msaada wa matibabu ameshindwa na mmemtelekeza.
20260223_100911.jpg
20260223_100714.jpg
 
Zezeta katika ubora wako, maboss wako wanatambaa kwenda kupiga magoti huko ulaya halafu wewe kidampa unapanua panua hapa mdomo kama chiriku kusema ulaya wamefilisika?
View attachment 3547660View attachment 3547661
Hata EU wanajua kuwa Samia ni bora kuliko JPM, wapinzani walimchokoza wenyewe. Baba yangu aliniambia kuwa kwenye cha bure kila mtu hana. Yaani kama uko kariakoo halafu ukakuta tajiri mmoja anagawa fedha hata kama unazo za kwako hutaacha kuzichukua na wewe. hata wakigawa chumvi bure na wewe hutaacha kuchukua chumvi hiyo ya bure. Kuna ubaya gani kwenda kuchukua fedha za bure za EU hata kama tunazo za kwetu?

Nakumbuka Tanzania ilinyimwa fedha za Covid 19 kwasababu ya JPM, lakini Samia akaenda kuzichukua akaja nazo hapo. Hata hizi za bure lazima watazitoa tu kwakuwa hata wazungu wanafaidika na tanzania; wanatuhitaji sisi sana kuliko tunavyowahitaji wao.
 
Ni kazi na mtutu , chawa huyo hapo anatembeza bakuli la msaada kama akina Kombo.
Siasa ni jukwaa tu la wewe kufanyakazi kukidhi mahitaji yako. Kazi ya siasa ni kulinda usalama wako tu basi. Vijana kule Marekani wanafanyakazi kama punda ili waweze kuishi marekani. Vijana wengi hawana vyumba vya kulala, wanalala kwenye magari yao waliyokopeshwa. Yaani kila mtu ana deni la kulipa. Ndiyo maana kule ushoga ni njenje tu kupata mahitaji yako.
 
Siasa ni jukwaa tu la wewe kufanyakazi kukidhi mahitaji yako. Kazi ya siasa ni kulinda usalama wako tu basi.
Hapa umeandika nini hebu rudia kusoma, kulingana na mada .
Vijana kule Marekani wanafanyakazi kama punda ili waweze kuishi marekani. Vijana wengi hawana vyumba vya kulala,
Hii inahusiana nini na nilichoandika?? Marekani ni ulaya??
wanalala kwenye magari yao waliyokopeshwa. Yaani kila mtu ana deni la kulipa. Ndiyo maana kule ushoga ni njenje tu kupata mahitaji yako.
Unaelewa hata ulichoandika?

Wewe ni zezeta , mada uliyoandika ni ulaya sasa tangu lini marekani ikawa ulaya ??
 
Zezeta katika ubora wako, maboss wako wanatambaa kwenda kupiga magoti huko ulaya halafu wewe kidampa unapanua panua hapa mdomo kama chiriku kusema ulaya wamefilisika?
View attachment 3547660View attachment 3547661
Kaka hata Marekani na nchi za Ulaya zinakopa China vibaya sana, zina madeni lakini zinatoa misaada kwa nchi nyingine. kaka wakati mwingine misaada na mikopo ni biashara kama biashara nyingine. Yaani naenda kukopa china kwa riba ya 0.25%, nikishazipata hizo pesa naenda kuikopesha tz kwa riba ya 7%. Wakati mwingine ninatoa msaada ili kurahisisha kupata kitu kikubwa kwako kama mgodi, korosho, wanyamahai au kuwekeza kwako kwa bei nafuu. Usihamaki na misaada hii, wazungu hawana kitu cha bure hata kimoja. Tuliza mshono kaka kama hujui mambo haya.
 
Hata EU wanajua kuwa Samia ni bora kuliko JPM, wapinzani walimchokoza wenyewe.
Weka hapa huo ushahidi wa EU waliposema hayo.
Baba yangu aliniambia kuwa kwenye cha bure kila mtu hana.
Ila baba yako hakukuambia anasikitika amepata mtoto zezeta kama wewe??
Yaani kama uko kariakoo halafu ukakuta tajiri mmoja anagawa fedha hata kama unazo za kwako hutaacha kuzichukua na wewe. hata wakigawa chumvi bure na wewe hutaacha kuchukua chumvi hiyo ya bure. Kuna ubaya gani kwenda kuchukua fedha za bure za EU hata kama tunazo za kwetu?
Wewe si ndio umesema ulaya wamefilisiika habari ya kugawa pesa za bure umekuja nazo kutoka wapi?
Nakumbuka Tanzania ilinyimwa fedha za Covid 19 kwasababu ya JPM, lakini Samia akaenda kuzichukua akaja nazo hapo.
Kwanini Samia alienda kuchukua kwa watu waliofilisika kama ulivyosema?
Hata hizi za bure lazima watazitoa tu kwakuwa hata wazungu wanafaidika na tanzania; wanatuhitaji sisi sana kuliko tunavyowahitaji wao.
Wewe mbona unafanya "contradiction" katika mada yako , mwanzo umesema wamefilisika na sasa unasema wanagawa pesa bure tangu lini mtu aliyefilisika akawa na uwezo tena wa kugawa pesa bure?

Unaona ulivyo zezeta kama ninavyokwambia.
 
Hapa umeandika nini hebu rudia kusoma, kulingana na mada .

Hii inahusiana nini na nilichoandika?? Marekani ni ulaya??

Unaelewa hata ulichoandika?

Wewe ni zezeta , mada uliyoandika ni ulaya sasa tangu lini marekani ikawa ulaya ??
Nikosoe kama unaweza, ninasema ninachokijua, sijawahi kuropoka wala kudanganya wasomaji wangu. Setu tu kuna wakati nakwambia kile ambacho hupendi kuambiwa. Kazi ya siasa ni kuweka policies kwa watu wake baaasi. Mwananchi tumia fursa ulizosongezewa kukidhi mahitaji yako. Asikwambie mtu kwamba akiingia Ikulu atakununua chupi mpya, uongo. Jenga barabara mimi nisafirishe mbuzi wangu kwenda sokoni baasi. Mbuzi lazima wawe wa kwako, ama umewafuga au umewanunua kwa mfugaji.
 
Kaka hata Marekani na nchi za Ulaya zinakopa China vibaya sana, zina madeni lakini zinatoa misaada kwa nchi nyingine.
Habari ya Marekani kukopa au China imetokea wapi?

Kwani hii mada yako si ilihusu matajiri Tanzania na waliofilsika Ulaya ?

Kwanini huwezi kutetea mada yako bila kutoka nje ya mada?
kaka wakati mwingine misaada na mikopo ni biashara kama biashara nyingine. Yaani naenda kukopa china kwa riba ya 0.25%, nikishazipata hizo pesa naenda kuikopesha tz kwa riba ya 7%. Wakati mwingine ninatoa msaada ili kurahisisha kupata kitu kikubwa kwako kama mgodi, korosho, wanyamahai au kuwekeza kwako kwa bei nafuu. Usihamaki na misaada hii, wazungu hawana kitu cha bure hata kimoja. Tuliza mshono kaka kama hujui mambo haya.
Halafu mimi sio kaka yako, sina ndugu zezetw kiasi hiki, wewe hizi habari za China umezitoa wapi , kwani Tanzania mikopo iliyonayo imemalizika kulipwa?

Unazungumziaje deni la taifa alilopokea Samuya kutoka kwa jiwe likiwa Trilioni 64 na hadi mwaka jana limefika trilioni 107 ?

Ukiweka mchanganuo wa bajeti ya Tanzanja haijitoshelezi 40% ni misaada kutoka kwa hao mnaowaita mabeberu halafu wewe unakuja kupanua panua mdomo hapa eti wamefilisika.

Migodi ipi unayozungumzia wewe zezeta hivi watanzania wa kawaida wananufaikaje na madini yao?

Stori za migodi na mbuga tulishazisikia na ni sehemu ambayo wananchi wake wanazunguka tu hawana maji safi na salama na wanaishia kupigwa risasi wakisogelea maeneo ya mgodi?
 
Nikosoe kama unaweza, ninasema ninachokijua, sijawahi kuropoka wala kudanganya wasomaji wangu. Setu tu kuna wakati nakwambia kile ambacho hupendi kuambiwa.
Unataka kukosolewa vipi , kwani hapa huonei navyokosoa uzezeta ulioandika?
Kazi ya siasa ni kuweka policies kwa watu wake baaasi. Mwananchi tumia fursa ulizosongezewa kukidhi mahitaji yako. Asikwambie mtu kwamba akiingia Ikulu atakununua chupi mpya, uongo. Jenga barabara mimi nisafirishe mbuzi wangu kwenda sokoni baasi. Mbuzi lazima wawe wa kwako, ama umewafuga au umewanunua kwa mfugaji.
Na kuua , kuteka , ufisadi nazo ndio policies zenu?
 
Weka hapa huo ushahidi wa EU waliposema hayo.

Ila baba yako hakukumwambia anasikitika amepata mtoto zezeta??

Wewe si ndio umesema ulaya wamefilisiika habari ya kugawa pesa za bure umekuja nazo kutoka wapi?

Kwanini Samia alienda kuchukua kwa watu waliofilisima kama ulivyosema?

Wewe mbona unafanya "contradiction" katika mada yako , mwanzo umesema wamefilisika na sasa unasema wanagawa pesa bure tangu lini mtu aliyefilisika akawa na uwezo tena wa kugawa pesa bure?

Unaona ulivyo zezeta kama ninavyokwambia.
Sio kila mtu anaekupa msaada yeye hana shida. Unaweza kumnunulia mchepuko wako chips mayai wakati mwanao anadaiwa ada hujalipa, na mama yako mzazi anakula ugali na mchunga kama sungura. Kiwango cha ukosefu wa ajira ulaya kimeongezeka, wamepandisha riba za mabenki na tozo nyingine ili kujaribu kuziba nakisi ya bajeti. Kule ufaransa hata muda wa kustaafu umesongezwa mbele. Shida wewe huna unachofahamu cha maana kwenye dunia hii zaidi ya samia samia samia kama mwehu.
 
Sio kila mtu anaekupa msaada yeye hana shida. Unaweza kumnunulia mchepuko wako chips mayai wakati mwanao anadaiwa ada hujalipa, na mama yako mzazi anakula ugali na mchunga kama sungura. Kiwango cha ukosefu wa ajira ulaya kimeongezeka, wamepandisha riba za mabenki na tozo nyingine ili kujaribu kuziba nakisi ya bajeti.
Kwanini Tanzania iende kukopa Ulaya na sio Ulaya waje kukopa Tanzania ?

Hadi hapa hujioni ulivyo zezeta kwa aina ya mifano ya kijuha unayotoa?

Una bahati saa hizi nina muda ndio maana nakujibu.
Kule ufaransa hata muda wa kustaafu umesongezwa mbele. Shida wewe huna unachofahamu cha maana kwenye dunia hii zaidi ya samia samia samia kama mwehu.
Hii inahusiana vipi na kufilisika ulikokusema?

Unaweza kunipa rekodi ya pato la mtu mmoja mmoja kwa Ufaransa na Tanzania?
 
Back
Top Bottom