Spika Tulia: Tusichanganye Maadili ya Mtanzania na Imani za kidini. Lipi kosa la walimu waliosimamishwa kazi Kwa kucheza muziki? Warudisheni kazini

Spika Tulia: Tusichanganye Maadili ya Mtanzania na Imani za kidini. Lipi kosa la walimu waliosimamishwa kazi Kwa kucheza muziki? Warudisheni kazini

Tulia ni spika bora kuwahi kutokea bongo.
1699276830255.png
TRUE❣️ 👊
 
Sijawahi kuona mchaga mpumbavu kama huyu profesa. Yaani hajui hata taratibu ya kumfukuza mtumishi wa umma!!

Tanzania nchi yangu.
 
Kwa kosa la kupiga wimbo usio na maadili na wenye kuhamasisha ngono. Ni mjinga pekee anaweza kupiga wimbo wowote mahali popote. Mkuu wewe unaweza kupiga wimbo "Zagamua" mbele ya wanao?
Mkuu Acha waruhusu zipigwe tu
Wao si ndiyo wanataka hivyo
Asilimia kubwa mitoto ya walalahoi
Ndiyo uimba miziki hiyo
Wao watoto zao sjui kama wanakatikaga mauno

Ova
 
Serikali imekuwa ikifanya hivi mara kwa mara na hata imeshatokea mara kadhaa kwa wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali na maofisa wengine wa serikali kusimamishwa kazi inapotokea kiongozi au mtumishi ametuhumiwa kwa kosa fulani na lengo hasa ni kumzuia mtu huyo asiingilie uchunguzi utakaokuwa ukifanywa juu ya tuhuma dhidi yake na uchunguzi utakapokamilika ndipo hatua stahiki zinachukuliwa na pale inapobainika mtumishi hakuwa na makosa basi urudishwa kazini na kulipwa stahiki zake zote.
Na ni pale uchunguzi unapofanyika ndipo mtuhumiwa uhojiwa na kupata fursa ya kujitetea.
Siyo kila kitu kinaitaji kufanyika uchunguzi. Hili la mziki linaitaji uchunguzi gani? Huyu Prof. hafai kabisa kuwa waziri, kama maamuzi yake ni ya hovyo kiasi hicho. Wimbo huo unachezwa na kuimbwa kila pahala ikiwemo mikutano ya CCM. Yeye kama waziri kwanini hajawai kuchukuwa hatua ya kufungia wimbo huo?. Si maadili mtoto akiusikia huo wimbo shuleni, lakini akiusikiliza sehemu nyingine hayo maadili ubadilika? Prof. Kawaonea hawa walimu....ana sababu zake zaidi ya maadili.
 
Watoto wenu wanachezeshwa nyimbo za ajabu za watu waliopotea kumaadili huko shuleni, watoto wao wanasoma kwa bidii na kufuata taratibu za miongozo ya shule zao za mamilioni ya pesa.

Mko hapa mnaita Waziri mjinga na kupambania walimu wakuu wazembe walioshindwa kusimamia shule.

Watawatawala wao na wakizeeka mtatawaliwa na watoto wao na wajukuu, endeleeni kushabikia uzembe na ujinga ujinga.
Wadau wengi humu wanaotetea huu upuz ni wajinga,nahisi wanafurahia
Watoto zao kukatika mauno na wakiwapima bkr zote washatolewa
Acha waendelee kusikiliza miziki hiyo
Tu

Watoto wa viongozi wao wanalelewa kwenye mfumo mzuri,huwezi sikia mtoto anasikiliza na kumfatilia zchu
Au asikilize mziki ameyatimba

Lakini ndiyo hivyo,shauri zaooo
Ni kuachana nao Acha waendelee
Kukatika mauno ngonongono
Na mpaka 2030 vitoto vitakuwa vimechakaqq

Ova
 
Hawa walimu ingekuwa mimi ningewafukuza kabisa kazi. Ningekuwa tayari kupoteza uwaziri kwa sababu yao
Utakuwa umekurupuka kama waziri husika...yaani wimbo iruhusiwe na BASATA bila kusema wimbo zipi zichezwe wapi alafu unakuja kuwafukuza walimu.
 
Amesema hayo akihoji kuhus Njia iliyotumika Kuwasimamisha walimu hao,Bila ya kufuata utaratibu wa kinidhamu wa kiutumishi,Hata hivyo ameongeza na kusema kuwa lisionewe kundi fulani tu kwani hata baadhi ya wabunge pia nao wanacheza miziki hiyo..

"Wapo mawaziri humu ndani na sisi wabunge huwa tunacheza mziki na hao wanafunzi, Tufafanuliwe hapa ili watu wajue nini cha kufanya la sivyo tutaendelea kucheza huo mziki na watoto wakiwepo shuleni alafu tutawapomza wale ambao watatakiwa kuchukuliwa hatua ,kwahiyo ni muhimu muwe na hatua zaidi ya hapa ili watu wote wawe na uelewa ni miziki gani inachezwa na ipi haichezwi itasaidia sana,Lakini tusiingize Huko hisia za kidini tusichanganye Imani ya dini na maadili ya mtanzania tusivichanganye" amesema Dkt tulia Ackson spika wa bunge la Muungano leo bungeni

hata hivyo aliendelea kumhoji waziri Njia iliyotumika kuwasimamisha walimu wao kazi na akasema kuwa njia hiyo haikuwa na usawa hivyo ameomba warudishwe makazini na njia sahihi zifuatwe

View attachment 2805936

View attachment 2805928
uwe unaandika taarifa sahihi, wale walimu hawakuondolewa kazini ila walishushwa vyeo maana walikuwa walimu wakuu. Hata hivyo bunge kupitia spika ilisema km kweli hawakuwepo kwenye vituo vyao vya kazi wakati ule muziki unachezwa ndio warudishiwe vyeo vyao. Km walikuwepo shuleni basi adhabu ya kushushwa vyeo ni sahihi na iendelee yaani wabaki walimu wa kawaida na siyo walimu wakuu. Kaa tulia kijana unawahi wapi mwisho unakuja kupotosha watanzania.
 
Bunge halifanyi kazi kwa kauli za mbunge mmoja mmoja na serikali inapaswa ifanye kazi yake kwa kuangalia maslahi ya kila upande sasa katika hilo uenda kuna wazazi wamelalamika hivyo katika hali hiyo ni wajibu wa serikali kufanya uchunguzi kabla hatua stahiki kuchukuliwa,serikali haifanyi kazi kama mganga wa kienyeji iseme itapiga ramli.
Kulalamika kwa wazazi hakuwezi kumfanya Waziri afanye maamuzi ya hovyo. Kinacho ongelewa hapa ni mziki usiokuwa na maadili uliopigwa na kuchezwa shuleni. Yeye kama waziri tena wa elimu, ameshidwa nini kuupiga burn huo wimbo? Watoto tunaishi nao kwenye jamii, waziri atuthibitishie kama kweli hao watoto hawajawai kuusikia na au kuucheza huo wimbo uko mitaani.
 
Wadau wengi humu wanaotetea huu upuz ni wajinga,nahisi wanafurahia
Watoto zao kukatika mauno na wakiwapima bkr zote washatolewa
Acha waendelee kusikiliza miziki hiyo
Tu

Watoto wa viongozi wao wanalelewa kwenye mfumo mzuri,huwezi sikia mtoto anasikiliza na kumfatilia zchu
Au asikilize mziki ameyatimba

Lakini ndiyo hivyo,shauri zaooo
Ni kuachana nao Acha waendelee
Kukatika mauno ngonongono
Na mpaka 2030 vitoto vitakuwa vimechakaqq

Ova
Wanawalea kwa nidhamu ili waje kuwaongoza watoto wanaokata viuno shuleni kwenye vumbi. Watoto wa darasa la nne tayari akili ipo kingonongono, Waziri akisimama kulinda maadili wanamuita mjinga.
 
Amma? ... lakini maudhui ya kawimbo mbona yanafungamanafungamana na uhabarishaji!!!?
... INA MAANA KWELI MWANA KAPONA? 😅
Zamani ilikuwa ni wizara moja Wizara ya Habari,Utamaduni na michezo ila wakazitengenisha wakapata wizara mbili ya kwanza ikawa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambayo Waziri ndo nape na
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo waziri wake ni Proff Ndumbaro na naibu ni mwanaFA
 
Kma umemuelewa alishindwa kusema moja kwa moja kwamba kwanini hawakuanza na Zuchu mwenyewe halafu wakafata walimu halafu na wwngine wakafata kuonea upande mmoja haifai wanatakiwa wawarudishe waalimu halafu zuchu ale Ban ya kwenda halafu ndo ziendelee mishe zingine
hivi hata taarifa za kiswahili hamuwezi kuelewa, hakuna mwalimu aliyefukuzwa kazi, ni kwamba walishushwa vyeo wale waliokuwa walimu wakuu wa zile shule 2. Bunge kupitia spika limesema km wale walimu wakuu walikuwepo shuleni wakati watoto wanachezeshwa ule muziki basi adhabu ya kushushwa vyeo ni sahihi. Hata hivyo spika akaongezea kuwa yeye ana taarifa ya ziada kutoka vyanzo vingine ya kuwa wale walimu wakuu hawakuwa shuleni wakati wa lile tukio. Akasema km hivyo ndivyo basi warudishiwe vyeo vyao bila kuwataka kukata rufaa kwa mamlaka yao ya nidhamu ambayo ni mkurugrnzi mtendaji wa Halmashauri husika
 
Siyo kila nyimbo inapigwa kila mahali, watoto wanapaswa kufundishwa maadili mema, Maudhui ya ile nyimbo yanafaa watu walioko kwenye ma-bar na magenge mengine ya wahuni
Haka kama mama kima ni ka-hovyo sana. Mbona kenyewe hakafuati taratibi sehemu nyingi tu. Kanataka ku-lecture watu kufuata taratibi wakati kenyewe ndiyo ibilisi mkubwa wa kuvunja taratibu?
 
uwe unaandika taarifa sahihi, wale walimu hawakuondolewa kazini ila walishushwa vyeo maana walikuwa walimu wakuu. Hata hivyo bunge kupitia spika ilisema km kweli hawakuwepo kwenye vituo vyao vya kazi wakati ule muziki unachezwa ndio warudishiwe vyeo vyao. Km walikuwepo shuleni basi adhabu ya kushushwa vyeo ni sahihi na iendelee yaani wabaki walimu wa kawaida na siyo walimu wakuu. Kaa tulia kijana unawahi wapi mwisho unakuja kupotosha watanzania.
Ok sawa
 
hivi hata taarifa za kiswahili hamuwezi kuelewa, hakuna mwalimu aliyefukuzwa kazi, ni kwamba walishushwa vyeo wale waliokuwa walimu wakuu wa zile shule 2. Bunge kupitia spika limesema km wale walimu wakuu walikuwepo shuleni wakati watoto wanachezeshwa ule muziki basi adhabu ya kushushwa vyeo ni sahihi. Hata hivyo spika akaongezea kuwa yeye ana taarifa ya ziada kutoka vyanzo vingine ya kuwa wale walimu wakuu hawakuwa shuleni wakati wa lile tukio. Akasema km hivyo ndivyo basi warudishiwe vyeo vyao bila kuwataka kukata rufaa kwa mamlaka yao ya nidhamu ambayo ni mkurugrnzi mtendaji wa Halmashauri husika
Kuna sehemu umeona nimeandika kufukuzwa kazi mkuu Au wewe ndo umekuja na perception zako kichwani..
Taarifa ni kwamba wamevuliwa vyeo wakati huo huo wamesimamishwa kupisha uchunguzi
 
Naona mambo mengi muhimu zaidi ya bunge kuongelea kwenye ripoti ya CAG, kuliko hii issue ndogo, au ni mimi sielewi??!
 
Back
Top Bottom