Subaru forester SJ5 / FB20 ni mgonjwa wa kansa anayetembea barabarani

Umetisha kaka. Sasa kabla haujatafuta gari we jiulizage haya:
-Budget
-Shape ya gari unayopenda (SUV, sedan, pickup, etc) au gari unazozipenda
-Matumizi makuu (ya kila siku)
-Uko radhi kufanya oil change kwa laki 1 au chini, au laki 2-3 ? Au utabadirisha brakes kwa elfu 45 au uko radhi kutoa laki 2 Bila shida??
-…

Hii itasaidia watu kukadiria gari gani utakua nalo comfortable
 
Iyo paragraph ya mwisho uko sahihi. Puma ni best alternative oil kwa premium cars. Nadhani hawapishani sana tech na Castrol.
 
Kwa hiyo bei ni Sahihi kuanzia 165,000-185,000.
Hawa wahindi ndiyo angalau wanauza oil original
 
Mkuu hiyo oil inauzwa Tsh ngapi ? Maana naogopa kubadilisha ovyo oil Mimi natumia Atlantic na Castrol Tu
 
Budget yangu ni Million 25 nikijivuta vuta mkuu 30 Million , napendelea design ya zile zilizofunuliwa kwa nyuma,Sasa sijui ni ipi kati ya hizo ulizotaja 😂 Me nimekariri ford ranger

matumizi ya kawaida tu kuendea route za mjini ambazo nazo sio za kila siku maana muda mwingi nautumia shambani So mjini mara nyingi ni kununua mahitaji ! Mfano mbolea na madawa na mahitaji ya familia
Na kutoka nilipo kwenda mjini kwa pikipiki huwa tunatumia dakika 30 tu ila ni barabara ya vumbi na milima.

Hapo kwenye kubadilisha oil ni kila baada ya muda gani ?
 
Wewe tafuta toyota kwa mazingira yako na gari unayopenda unaweza pata toyota surf niliwahi ona inauzwa around 30M , gari nje ya toyota itakutesa , uzuri wa toyota hata oil/spea ikiwa sio inaweza vumilia kidogo, sasa kwa mgeni wa magari lazima utakutana na hiyo mikasa
 
Mkuu,
Magari mengi huharibika si kwa sababu ya ubovu au makosa ya mtengenezaji, bali kwa sababu ya ushauri wa kimazoea kutoka kwa baadhi ya mafundi wa chini ya mwembe.

Kauli kama “engine hii ni mbovu” au “gearbox hii haifai” au "Bongo joto" mara nyingi si za kweli. Ukweli ni kwamba baadhi ya injini za kisasa hazivumilii uzembe au matunzo yasiyo sahihi, hasa kwenye matumizi ya engine oil.

1. Hoja ya 0W-20 kuwa nyepesi kwa joto la nchi za tropiki si sahihi kitaalamu.

Joto la nje (ambient temperature) halina uhusiano wa moja kwa moja na joto la ndani ya injini, isipokuwa wakati wa kuwasha gari. Joto la ndani ya injini hufikia hadi 100–110°C, so kusema huku bongo kuna joto si sahihi coz joto letu la 30–35°C la mazingira ya hapa bongo ni dogo kuliko la ndani ya engine.

Oil ya 0W-20 imeshapimwa na kuthibitishwa kufanya kazi kwenye joto hilo la ndani ya engine.

Pia, fully synthetic 0W-20 za kisasa zina high shear stability na hazigeuki “kama maji”. Ndiyo maana Subaru, Toyota, Honda n.k hawaandiki oil tofauti kulingana na nchi au hali ya hewa. Wanataja oil moja tu dunia nzima kulingana na walivyoiunda engine.

2. Hoja ya oil clearance ndogo
Ni kweli kwamba injini ya FB20 ina tight tolerances. Lakini hitimisho la kutumia oil nzito si sahihi. Ndiyo maana mtengenezaji ametaja oil nyepesi ya 0W-20 badala ya 5W-30. Oil nzito hupunguza oil flow kwenye maeneo nyeti ya engine, huchelewesha lubrication wakati wa kuwasha, na huongeza uchakavu wa crankshaft na bearings baada ya muda.

3. Kauli kwamba “SJ5 inakula oil na head gasket inaharibika kirahisi”
Hapa mkuu matatizo mawili tofauti yamechanganywa:

a) Kula oil husababishwa na kuchelewesha kubadili oil, kutumia oil isiyo sahihi au fake, uwepo wa tope la oil kwenye engine, oil kuvuja sababu ya kuchaa kwa seal za valve n.k. Hili si tatizo la Subaru SJ5 pekee.

b) Head gasket failure mara nyingi husababishwa na overheating, oil kuchelewa kusambaa kwenye injini, matumizi ya oil isiyo sahihi kama hivyo kuweka 5W30 badala ya 0W20, tatizo la cooling system n.k

4. Hoja ya 5W-30 kuua engine
Hoja hii ina sehemu ya ukweli, si kwa sababu 5W-30 ni oil mbaya, bali kwa sababu FB20 haikubuniwa kwa oil hiyo. Uzito wake husababisha kuchelewa kwa lubrication, kuongezeka kwa msuguano na uchakavu wa bearings. Hapo lazima engine ife.

Matatizo mengi ya magari ya kisasa yanatokana na kusikiliza ushauri wa kubahatisha au kukariri teknolojia za zamani. Ukifuata maelekezo ya mtengenezaji, injini itadumu bila matatizo makubwa.

Nimetumia 0W20 kwenye RVR na Prius kwa miaka, sikuona shida. Shida inaanza ukianza kuweka ubunifu wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…