KERO Supervisors wa Wanafunzi wa Masters - UDSM ni kero, wanatukwamisha wengi, Uongozi wa Chuo uchukue hatua

KERO Supervisors wa Wanafunzi wa Masters - UDSM ni kero, wanatukwamisha wengi, Uongozi wa Chuo uchukue hatua

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hii hali hadi UDOM ipo, 2023 kati ya master learners 78 waliohitimu ni only 2. 2024 kukawa na kikao kati yao na VC, wakamwambia hivi "Sisi tuna majukumu mazito ya kifamilia kama mnaona ni fashion kutushikilia hapa huku tukiingia gharama tupeni ada zetu tuondoke"

Basi VC akajifanya hakujua kinachoendelea kawa mpole na kuwahakikishia mambo kukaa sawa. Sijui mwaka huu mambo yatakuwaje maana pale watu hukaa hata miaka 10 kisa Masters.

Mi itoshe kwa level nilofikia Tz, kama ni progress nitaenda away hata Kenya but home hapana. kwanza topic nyingi ni repeatedly throughput the time of learning nilihisi kuchoka tu with same things.
SIJAKUELEWA,KWAMBA mwaka 2023 Kati ya wanafunzi 78 wahitimu ni wawili tu Masters?
 
Pole sana ndugu yangu kwa haya. Hata hivyo simulizi yako imejaa maneno mengi yasiyo na hoja. Kwa kiwango cha elimu uliyonayo, moja ya mambo muhimu kwenye mjadala ni kujenga hoja na hoja hujengwa kwa ushahidi. Tuhuma nyingi zimeelekezwa kwa wataaluma hawa wa udsm, lakini je umetoa ushahidi wowote kuthibitisha tuhuma zako? Je, ni mwalimu yupi kwa mfano ambaye amekuwa hasomi wala hakutani na wanafunzi? Je, hili la kwamba ukishtaki wanateteana, ulishtaki kwa nani na ni majibu gani ulipewa? Hoja kwamba waalimu wanaweza kuamua kuwachelewesha wanafunzi pasi na sababu sio za kweli. Wakati mimi nasoma hapo udsm, kulikuwa na online supervision ambapo ukituma kazi kwa mwalimu inaonyesha tarehe na siku atakayokurudishia. Je kwako ilikuwa hivyo? Kama ndivyo kwa nn hukupeleka mashtaka angalau kwa mkuu wa IDARA ilhali mfumo unakupa ushahidi wa kutosha?
Mwisho, kazi ya supervision ni ngumu sana. Hawa jamaa wanapangiwa wanafunzi wengi na hivyo juhudi ya mwanafunzi huamua kumaliza kwake.
Malipo pia kwa hawa jamaa ni kidogo sana. Niliwahi kuambiwa kwamba hulipwa 150k kwa kila mwanafunzi wa masters wamayemsimamia. Hii pia inaweza kuwa sababu kwamba hawana morali na kazi yao hii ya kunoa bongo za vijana.
Nihitimishe kwa kusema kwamba pamoja na mapungufu ambayo hawa wanataaluma wanaweza kuwa nayo bado wanastahili pongezi badala ya lawana tu kwa kazi wanayofanya pamoja na kuwa kwenye mazingira magumu sana. Usiombe upite udsm kipindi hiki cha joto, utawakuta maofisini wameloa maji kisa joto kwani hata AC ofisi zao hazina hahaa
Ni kweli kabisa na hii hali ipo vyuo vyote vikuu vya serikali.
 
Mimi na wenzangu kadhaa tunaosomea Shahada ya Uzamili (Master of Public Health - MPH) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) tuna changamoto moja kubwa ambayo imekuwa kero kwa muda mrefu na kuendelea kuifumbia macho itakuwa ni sawa na kuendelea kufuga mtatatizo.

Tatizo letu kubwa ni kuhusu utendaji unaofanywa na Wasimamizi wa Kazi za Utafiti za Wanafunzi (Supervisors wa Research), hawa watu wa muda mrefu wamekuwa ni tatizo na kama hali hii haitekemewa au kuchukuliwa hatua watakuwa ni kati ya sababu zitakazokimbiza Wanachuo kusoma UDSM.

Kabla ya kuanza kusoma Masters hapo UDSM baadhi yetu tuliambiwa na waliosoma kuwa bora tutafute chuo cha binafsi kuliko kusoma hapo, tulipouliza tukaambiwa ni jambo gumu sana kuhitimu Masters na ukifanikiwa mara nyingi lazima uwe nje ya muda hata kama unasoma vipi na kujituma.

Utaratibu uliokuwepo siku za nyuma ilikuwa unapofika muda wa kukamilisha kazi yao na ukazidisha ilitakiwa mhusika alipe Tsh. 50,000 kwa kila mwezi, lakini sasa hivi utaratibu ulivyo ukichelewa kukamilisha Reasearch yako unatakiwa kulipa hela ya Semister nzima ambayo ni Tsh. Milioni 2.5

Uongozi wa UDSM unafanya hivyo kwa kuwa hauambiwi ukweli kuwa asilimia kubwa wanaosababisha Wanafunzi wanashindwa kukamilisha tafiti zao ndani ya muda ni Supervisors.

Supervisors wanajiona kama Miungu watu, kwanza unapopewa akusimamie picha linaanza kuja kumpata ni unatakiwa kuacha kazi upate kazi ya kumtafuta yeye.

Ukifanikiwa kumpata anaweza kukupa maelekezo ya kazi au ukamkabidhi kazi yako ili aipitie lakini akachukua zaidi ya miezi miwili kuipitia au kuja kumuona tena.

Tuna wenzetu ambao tulianza nao Masters pamoja, wao wapo katika vyuo vya binafsi kama ilivyo Chuo cha SAUT, sasa hivi wanaelekea kuhitimu, sisi ndio kwanza tunaendelea kuimba mapambio ya kuwatafuta Supervisors.

Mfano darasa letu tulikuwa Wanafunzi kati ya 25 hadi 30 lakini hivi tunavyoandika hapa wanaotarajia kuhitimu ni wawili tena ambao nao wamechelewa.

Supervisors ni shida, hawapatikani kirahisi na baadhi yao ukiwapata hawakupi majibu mazuri.

Ukisema uende ukashtaki au kuwasilisha malalamiko yako juu ya Supervisors, huwezi kupata msaada kwa kuwa unaenda kushtaki kwa wenzao.

Pili, suala la kutakiwa kulipa ada ya Semister nzima kwa uzembe unaofanywa na Mtumishi wa Chuo ni maumivu makubwa kwetu tunaosoma.

Kozi ya Miezi 18 unajikuta umeisoma Miaka mitatu, hapo unalipa ada ya Tsh. Milioni 7+ kisha uambiwe tena ulipe Tsh. Milioni 2.5 ni mateso yasiyo na maelezo hasa kwa kuw wengi wetu tunaosoma chuo hicho ni Wafanyakazi na wengine tuna familia.

Tunakuwa hatueleweki, kutumia muda mwingi kusoma, hela ya familia pia tunaipeleka

Uongozi unapewa taarifa tofauti
Tumefuatilia na kugundua kuwa Uongozi haufikishiwi taarifa sahihi, wanajulishwa Wanafunzi ndio wenye shida lakini uhalisia ni tofauti.

Hii ikiendelea UDSM itaendelea kukimbiwa kwa kuwa hakuna anayeweza kuvumilia usumbufu huo na kupoteza hela bila sababu za msingi.
UDSM kimekua chuo cha ajabu sana, kuna kipindi kiliitwa majalalani na hili halikupingwa, kuna kipindi wasomi wa hapo walitumika kwenye kamati mbalimbali za kiserikali mfano walikaja na matokeo kuwa kuchafuka kwa mto Mara imetoka na vinyesi vya wanyama (Ng'ombe). Udsm bado ina wafanyakazi ambao ni useless kama ma bursar kuna mimama haitumii akili ku reason kitu kidogo too many complications yanatakiwa yawe yameshafukuzwa kazi muda mrefu. UDSM imekua ya ki local na inasemekana ni full ndumba nangai pale mfano kugombania nafasi za uongozi, kwenda kula per diem au kwenda nje ya nchi this is shame to large extent. UDSM imekosa kuwa na hadhi kama ya zamani ya kuwa mihadhara yenye tija kwa nchi hakuna tena imegeuka kuwa chawa na soon it gonna change to bed burgs. UDSM postgraduate supervisors wengine wamekua Miungu watu ila kuna wengine ni wazuri sana. UDSM it must change, and changes must start Now.
Take home... 1. Fire all useless people. 2. They must adhere to good succession plan as they use to preach in class. 3. Maintain water availability all the time. 4. Treat postgraduates with manners and make sure they graduate on time.
 
Hii tabia ni sugu sana kwa vyuo vingi nakumbuka miaka ya nyuma wakati nasoma shahada ya uzamili kama wewe wanafunzi wengi tulikutana na changamoto kama ya kwako/kwenu.

Supervisor kumpata ni shida ukimpata ukimpa kazi kusoma hasomi kwa wakati inafika wakati kazi inachukua mwezi kakaa nayo tarehe za defense zinasogea.

Mfano unakuta supervisor mmoja ana wanafunzi 5 na wote hawa graduate mwaka husika kisa research sasa unashindwa kuelewa wanafunzi wote watano ni wazembe au supervisor ni mzembe sana.

Kwakeli majority ya hao Dr’s na ma prof wanapenda kusujudiwa sana na niwasumbufu sana hawapendi vitu viende kwa njia nyepesi.

Baadhi ya classmate wali graduate baada ya miaka 3 (yani course ya miezi 18 unasoma miaka minne hadi mitano) wengine waliamua kuacha chuo kabisa baada ya kuona usumbufu umezidi.
Vyuo vingi kwa Sasa vina supervisor wawili ,kama mmoja hatoi ushirikiano komaa na anayetoa ushirikiano.Mambo kama haya yalikuwepo Mzumbe lakini kwa Sasa hakuna unapewa supervisor wawili ukishindwa kuhitimu kwa wakati shida inakuwa ni wewe.

shida ya UDSM wahadhiri Kwanza wengi wanapewa kazi maalum wako busy Sasa kama anakusimamia na Yuko peke yake lazima ukwame.

Ni kweli tunapenda Brand ukipata gamba lao Kuna sehemu kupenya itakusaidia lakini kulipata Sasa.Ada yao iko chini ila kupata gamba lao.
 
Lazima wote wawili watoe comments zao kwenye kazi hata kama ni kwa wakati tofauti.

Huwezi kugraduate kwa kusimamiwa na supervisor mmoja huu ni utaratibu wa TCU.
 
Sasa inakuwaje supervisor wote wawili ulopewa wawe wavivu.Nakumbuka Kuna Dr.mmoja yeye alivyoona mwenzake ni mvivu akaendelea kupiga kazi mwamba amekuja kustuka kazi inawasilishwa idarani na jamaa akagraduate kwa wakati .Naamini Two supervisors wote hawawezi kuwa wavivu aisee.Ukiwa serious watafanya kazi tu.

Lazima wote wawili watoe comments zao kwenye kazi hata kama ni kwa wakati tofauti.

Huwezi kugraduate kwa kusimamiwa na supervisor mmoja huu ni utaratibu wa
 
Hilo la uvivu na ubusy ni tatizo ila standard inatakiwa Supervisor wako wote

wawili watoe mchango wao ili research yako iwe bora na kama Supervisor mmoja
ni mvivu au yupo busy unatakiwa uombe ubadilishiwe ila sio utaratibu kuwa na inputs za Supervisor
mmoja tuu kwa level ya master na PhD.
 
Tatizo hilo mkuu. Kuna vyuo mpaka tunaogopa kwenda kusoma shida ni hizo.Ada uipate kiugumu ujitume darasani kwa nguvu zote alafu Mtu anaanza kukwamisha it's not fair.
Hilo la uvivu nq ubusy ni tatizo ila standard inatakiwa Supervisor wako wote

wawili watoe mchango wao ili research yako iwe bora na kama Supervisor mmoja
ni mvivu au yupo busy unatakiwa uombe ubadilishiwe ila sio utaratibu kuwa na Supervisor
na inputs za Supervisor mmoja tuu kwa level ya master na PhD.
 
Tatizo hilo mkuu. Kuna vyuo mpaka tunaogopa kwenda kusoma shida ni hizo.Ada uipate kiugumu ujitume darasani kwa nguvu zote alafu Mtu anaanza kukwamisha it's not fair.
Vyuo kama vipi hivyo?
 
Back
Top Bottom