Sura ya Mungu kupitia Wajapani

Sura ya Mungu kupitia Wajapani

Kwa sababu sasa hivi niko Mara, Serengeti.
Sababu hiyo hiyo inayokufanya usikubali kwamba sasa hivi upo Geneva, Switzerland ukiiba benki, kwa kuwa upo Serengeti, Mara, ndiyo inayonifanya nisikubali kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya kutokea.

Sababu hii ni "contradiction".

Habari ikijipinga yenyewe kwa mambo ya msingi kabisa, haiwezi kuwa ya kweli.

Mathalani, kama kimantiki haiwezekani kwa wewe kuwa sehemu mbili kwa wakati mmoja, tuseme Serengeti na Geneva, hapo tutaona habari ya kwamba uko Serengeti na pia upo Geneva wakati huo huo inajipinga yenyewe, ina contradiction, hivyo haiwezi kuwa kweli.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea ni contradiction. Ni sawasawa na wewe kuwepo Serengeti na Geneva kwa wakati mmoja.

Kwa sababu, nature ya Mungu ya uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote haiendani na yeye kuumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu usioruhusu mabaya.

Hii habari ni sawa na kusema kuna baba anayependa watoto wake sana, ana uwezo wa kujenga nyumba yoyote, lqkini kaamua kujenga nyumba akaitegeshea mabomu yawalipue watoto wake.

Huyo baba haiwezekani awepo, uwepo wake una contradiction, kama kajenga nyumba yenye mabomu wakati aliweza kujenga nyumba isiyo na mabomu, basi hana upendo hivyo na wanawe hao, kama ana upendo na wanawe sana, asingejenga nyumba hiyo yenye mabomu.

Hapo utaona dhana ya Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu huu unaoruhusu maovu ina contradiction.

Ina contradiction kwa sababu si ya kweli.

Mungu huyo hayupo.

Ndiyo maana mpaka leo hakuna mtu anayeweza kuthibitisha kwamba huyo Mungu yupo.
 
Ila Wajapani kabla ya vita vya pili vya dunia walikuwa washenzi na wadhalimu sana. Walibadilka baada ya kushindwa vita vibaya sana.
 
Matukio ya kuuana Japan ni machache sana.
Ila pia inasemekana kuwa Mfumo wao wa maisha unawafanya wawe na stress na depression sana. Yani mfumo wao unawalazimisha kuficha mambo mengi yanawauma ndani kwa ndani kutoka na kuishi kwendana na expectation ya jamii juu yako.
Halafu ukifuatilia wana matukio yao ya kuuana ya ajabu sana aisee.
 
What is the worst about that?
Wewe mwenye dini una tofauti gani na wao wasio na dini?
Umewahi kusikia Japan wanasiasa wanapigwa risasi, wanapotea au wanapewa kesi za michongo n.k?
And the worst part about them ni kwamba,Wajapani hawana DINI...
 
Unaeleza vizuri sana ila Rudi kwenye swali langu la msingi.
Unaamini kuwa Mungu yupo ama Hayupo?.
Kiranga:Hana IMANI juu ya chochote yeye anaishi kwa facts,waaamini tunaishi kwa IMANI ya Mungu na facts juu ya Mungu.
Kiranga hataki kusikia kuhusu IMANI yeye anataka facts tu.
Ibilisi wa kiranga kambana kwenye akili na moyo wake kutaka kujiona na kuamini kuwa yeye anategemea zaidi facts kuliko imani wakati huo huo anasahau kama yeye mwenyewe anaamini(IMANI) kuwa anaendesha mambo au mienendo yake inapelekwa juu ya misingi ya facts.Je Kiranga anaweza akadhibitisha kuwa MUNGU hayupo kwa facts alizonazo au anarudi kulekule kwenye kuamini tu kuwa MUNGU hayupo kama atakuwa anaamini kuwa MUNGU hayupo basi hata yeye bado anaishi kwenye mzingo wa IMANI.
Na tunaoamini uwepo wa MUNGU tunaamini kuwa ni ibilisi shetani keshamtia upofu.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Nakwambia Mungu hayupo halafu unaniuliza tena kama yupo au hayupo?

Unajua kusoma wewe?

Mpaka hapa naona hujui kusoma.

Tutaweza kujadiliana kweli?
MUNGU yupo.
Najua utauliza yuko wapi?
MUNGU yuko mahali kote.
Najua utataka facts.
Facts tazama ulimwengu ulivyo mkubwa usio na mwisho unavyoenenda na ulivyoumbika ni kwa mapenzi na uweza wake.
Tazama viumbe wake na uhai na utashi uliopo ndani ya viumbe wake.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
MUNGU yupo.
Najua utauliza yuko wapi?
MUNGU yuko mahali kote.
Najua utataka facts.
Facts tazama ulimwengu ulivyo mkubwa usio na mwisho unavyoenenda na ulivyoumbika ni kwa mapenzi na uweza wake.
Tazama viumbe wake na uhai na utashi uliopo ndani ya viumbe wake.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
Umejuaje nitauliza Mungu yuko wapi?

Hujathibitisha Mungu yupo, umetoa logical non sequitur.

Thibitisha Mungu yupo.
 
Kuna post moja facebook ya mark zuckerberg alikuwa ameweka picha yake kipindi cha christmas.
Then akatokea mkenya mmoja hivi mweusi yaani ile black kabisa kama walivyo wakenya, yule jamaa akaweka picha yake na akaandika merry christmas from kenya.

Sababu ile post ni ya zuckerberg mwenyewe means watu wote wanaona kilichofuata ni huruma sababu walitokea hao wa Asia wakaanza kumtukana yule jamaa mpaka basi kisa ni mweusi.
Wengine walikuwa wanamwita orangutan yale manyani makubwa hivi na matusi mengine kibao.
Mara lips zake zimefanyaje mara mweusi kama asphalt ile lami nyeusi kabisa, mara wengine wanamwita BBC ila matusi ya kumfananisha na nyani ndio yalikuwa mengi.

Cha ajabu nilichokiona ni comment zote zilikuwa zinamshambulia jamaa hakuna exceptional hata moja na zote ni asians, yaani hawa waasia wanatabia na akili kama za wadudu zero sympathy zero emotional intelligence walikuwa wanamchukulia jamaa kama sokwe tu asiye na vigezo vya binadamu.
Jamaa nakumbuka alisema asante kwa matusi yenu na kutiatia huruma tu, kusema ukweli nilijisikia vibaya kuona mwafrika anafanyiwa vile.
Baadae wakenya wenzake wakamwambia afute ile picha lakini hakufanya hivyo.

Hawa mnawaita wana roho njema na kuwasifia lakini kwao mtu mweusi wanamwona nyani tu.
Katika watu wabaguzi kwa waafrika ni waasia, kwangu ni mbwa kama mbwa wengine tu.
 
Wewe sema tu ni mvivu wa kusoma.

Kwanza usiniite dogo hiyo ni dharau, hujui umri wangu.

That is very condescending. Halafu inakuonesha wewe ni mtu wa kufanya assumptions tu.

Kuhusu hoja yako kwamba kitu ambacho hakipo sitakiwi kukijadili, hapo unaonesha utapiamlo katika uwezo wako wa kufikiri kimantiki.

Nitakuonesha kwa nini, kwa mfano rahisi tu.

Kama kuna mganga muongo anasema ana dawa inayotibu ugonjwa mpya, na madaktari wanajua hakuna hiyo dawa, huyo mganga ni muongo, madaktari hao wana wajibu wa kukanusha na kusema hiyo dawa ni ya uongo haipo.

Wataijadili hiyo dawa ambayo haipo ili kuonesha watu kwamba haipo.

Wewe ni kama mganga muongo unayesema kuna dawa (Mungu) wakati hakuna kitu hicho.

Daktari anayejua hiyo dawa haipo (mimi) ana wajibu wa kuweka rekodi sawa na kuonesha uongo wako.

Kwa sababu, kuna watu wanaweza kuzembea kujikinga wakifikiri kuna dawa, kumbe habari za dawa kuwepo ni uongo.

Natumaini umeacha uvivu wa kusoma na umesoma mpaka mwisho.

Vinginevyo hatutawezi kujadiliana.

Mungu hayupo.

Kama unabisha, thibitisha yupo.
Una maneno mengi na inaonyesha unasoma mambo mengi ila uelewa wako ni finyu sana mithiri ya punje ya mchanga kwa maelezo ya hapo juu tu umechanganya mambo hayaingiliani kabisa na utasema watu wavivu wa kusoma.
Wewe hodari wa kusoma unasoma mambo yanakutia wehu unachanganya mambo mengi sana.
Nakushauri wahi ukapate Tiba ata hapo mirembe dodoma utapata nafuu.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Una maneno mengi na inaonyesha unasoma mambo mengi ila uelewa wako ni finyu sana mithiri ya punje ya mchanga kwa maelezo ya hapo juu tu umechanganya mambo hayaingiliani kabisa na utasema watu wavivu wa kusoma.
Wewe hodari wa kusoma unasoma mambo yanakutia wehu unachanganya mambo mengi sana.
Nakushauri wahi ukapate Tiba ata hapo mirembe dodoma utapata nafuu.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
1. Hujaweza hata kutaja hayo mambo uliyosema nimechanganya.Achilia mbali kuthibitisha kwamba nimechanganya.

2. Hujaweza kukanusha hoja zangu

3. Hujathibitisha Mungu yupo.
 
Nyongeza,
Tafiti zinaonyesha Wajapan Ndo jamii ya binadamu duniani inayoelekea kupotea ktk uso wa Dunia kwa Kasi zaidi.

Inatabiriwa kama hawatobadilika kufikia 2080,Hakutakua na wajapani wowote duniani.
 
Nyongeza,
Tafiti zinaonyesha Wajapan Ndo jamii ya binadamu duniani inayoelekea kupotea ktk uso wa Dunia kwa Kasi zaidi.

Inatabiriwa kama hawatobadilika kufikia 2080,Hakutakua na wajapani wowote duniani.
Wajanja sana sura ya karai. Wananchi fanya sasa ni kuchukua vijana wa kiafrika na kuwapa ajira na mikataba ya kuishi kwao kwa muda mrefu, lengo ni kuchanganya damu ilio moto. Wanajua wazi damu moto ikichachamaa huanzia watoto 3 na zaidi, huo mwaka ulio sema elewa kutakuwa na machotara wengi na maliasili watu itazidi.
 
Back
Top Bottom