Swali gani gumu ulilowahi ulizwa na mtoto mdogo?

Swali gani gumu ulilowahi ulizwa na mtoto mdogo?

Nina dogo wa kike ana 4years tunalala nae ndani kwenye chumba changu japo vitanda tofauti. Sasa nina kawaida kila asubuhi ninapojiandaa kwenda kazini lazma nioge pamoja na kujisaidia haja kubwa na ndogo, Choo kiko ndani ya chumba changu humohumo.

Siku hiyo niko chooni nasikia anamuuliza mama yake, Mama kumbe baba naye anakunyaga namuonaga kila siku asubuhi anaingia chooni.

Tangu siku hiyo nikamhamisha dogo chumba

na kabla ya hapo siku za nyuma kidogo nikiwa namgegeda mama yake usiku sana kumbe akawa anasikia, asubuhi akaniuliza "Usiku mama alifanyaje mpaka ukampiga, mbona alikuwa analia? nikaona ohooo hiki kitoto kishakuwa tatizo.
Hii chai
 
Mie mzee wangu aliniambia nilipokuwa mdogo niliwahi muuliza eti kwanini neno "Giraffe" lina "double f" na siyo "single f"
 
nakumbuka nikiwa 6-7 yrs nilimuuliza jamaa mmoja alikuwa mshikaji sana wakati huo yeye yuko kwenye 28 hivi.

nikamuuliza hivi mwakajana itakuja tena??[emoji28]

kama umeshawahi kutulia peke yako,kuna wakati memory flani za miaka hata miwili au mitatu nyuma zinakuja halafu unatamani zijirudie,hapo ndipo msingi wa swali ulianzia.bahati mbaya jamaa hakunielewa,na hata angenielewa asingeweza kunielewesha.
Haha, mm mwenyewe cjkuelewa
 
Nina mtoto wa miaka minne ni mtundu sana sasa kila wakati mama yake humwambia unanisumbua. Sasa mwezi uliopita baada ya kuambiwa hivyo ilipidi amuulize mama yake "mama unaonaje si bora nife ili nisikusumbue?"
Mama yake kachoka mpaka leo.
 
Juzi hapa dogo alikuwa anasikiliza redio,kulikuwa na taarifa kwamba dunia itagongwa na kitu gani sijui tarehe 29..sasa dogo akauliza papi hivi kwa mfano hii dunia ikigongwa na hicho kitu,ikatikisika, ikayumba,halafu ikadondoka,itadondokea wapi?..
Dah nikataka kujibu haraka haraka nikashtuka!...nikamwambia haiwezekani,acha kuuliza maswali ya kijinga..
Dogo akatulia kimya akawa mnyongee,ila baadae jioni nikawaza dizaini kama "swali la dogo lina mantiki kimtindo"
Majibu kama haya huwafanya watoto wasijiamini na kuacha tabia ya udadisi.
 
Back
Top Bottom