Swali gani gumu ulilowahi ulizwa na mtoto mdogo?

Wazazi mbona mnazingua kinyama!
Mnawaharibu watoto kuwajibu hivyo bora uje utafute jibu kama hujui..

Tena hayo ya kisayansi ya anga uwe unaniletea Mimi akikuuliza..
Kweli aise, alimkatili sana mtoto, hofu yng hatauliza tena maswali,

Sent using kidole gumba
 
😂😂😂
 
Nakumbuka sehemu niliyokuwa naishi kulikuwa na mashamba makubwa ya mpunga .baadhi ya wamiliki walifahamika kwa majina.

Siku isiyokuwa na jina napita na mtoto wangu mpendwa aliniuliza"baba mbona watu wana maeneo makubwa sisi hatuna hata eneo Dogo".nilikosa jibu ikabidi nitafakari upya swali ili nimpe jibu sahii

Nilimjibu "Mimi ni baba bora ambaye nakujali mwanangu natakeleza unayoyataka ,hilo nitalifanyia Kazi mwanangu".akakosa jibu na swali la kuuliza tena

Swali lile lilinisaidia kipindi napitia magumu nilitamani kuuza kiwanja changu baada ya kuishiwa kila kitu.nilijipa moyo nimeahidi mimi ni baba bora wacha nitekeleze .nashukuru Mungu Leo kiwanja kile nimejenga nyumba ya familia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto alimuuliza mama yake mbona hajaliona soko la watoto ambalo yeye alinunuliwa kila anapopita masokoni maana anaambiwa watoto wananunuliwa baada ya kuulizwa huyu mwingine nae kanunuliwa...
 
Pacha wangu wa kike aitwae Doyi mwenye miaka mitatu alimuona Kaka yake wa miaka sita akikojoa wima,sasa nadhani alivutiwa na ule mtindo wa kukojoa wima badala ya kuchutama.
Akaiingiza vidole kwenye suruali yake na akajipapasa kwa kisha akaniangalia usoni huku akiwa na huzuni akaniuliza:
"Baba na mimi nitengeneze kama huyu(kaka yake) niwe nakojoa nimesimama."
Ahahahaha
 
Umenikumbusha mbali Sana, Mimi kuna mtoto wa kaka yangu aliniuliza, hivi baba mdgo wangu kuku walitoka wapi?
Nikamjibu viumbe wote waliumbwa na Mungu, likaja swali lingine Huyo Mungu kwanini aliwafanya wasiweze kuongea kama sisi binadamu?

Nikajibu, Eee alitupendelea sisi binadamu sio wanyama, ila hakuridhika huyo dogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah kweli anayo desire nzuri mno
 
Daah kajisikia huzuni kweli kama namuona asa ukamjibu vipi na baada ya kumjibu ajakusumbua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…