Swali gani gumu ulilowahi ulizwa na mtoto mdogo?

Swali gani gumu ulilowahi ulizwa na mtoto mdogo?

Kuna siku mtoto wa miaka 12 aliniuliza swali ambalo hata wewe nikikuomba jibu baadhi sidhan kama mtapatia.
Swali, kaka hivi kila siku tunachota maji kisimani hayaishi kwa nini?
Nikamjibu kisima chini kuna chemchem ambazo zinatoa maji. Akasema ahaa nimeelewa akaongeza swali sasa je tusipo yachota yatajaa mpaka yaje juu ya ardhi??
Nikamjibu kitaalamu akaelewa!!
Ebu naomba jibu na wewe leo, ni kwa nn hivi visima ambavyo maji hupatikan mita kadhaa kwenda chini huwa havijaii mpaka juu akati ukiwa unachota unaweza ukateka maji zaidi ya tank kadhaa za maji???

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulimjibu vp kitaalam tuelewe kwanza, yawezekana na wewe ni mtoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dunia yetu imeumbwa na Mungu na hawezi ruhusu hicho kitokee
Juzi hapa dogo alikuwa anasikiliza redio,kulikuwa na taarifa kwamba dunia itagongwa na kitu gani sijui tarehe 29..sasa dogo akauliza papi hivi kwa mfano hii dunia ikigongwa na hicho kitu,ikatikisika, ikayumba,halafu ikadondoka,itadondokea wapi?..
Dah nikataka kujibu haraka haraka nikashtuka!...nikamwambia haiwezekani,acha kuuliza maswali ya kijinga..
Dogo akatulia kimya akawa mnyongee,ila baadae jioni nikawaza dizaini kama "swali la dogo lina mantiki kimtindo"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mdogo wangu alipata mtoto so alikuwa haishi na baba wa mtoto huyo. Miaka ikasonga baadae akapata mchumba ambae kwa sasa wa naishi wote. Huyo mtoto akaanza kumuita huyu mwanaume baba. Anampenda kweli.

Siku moja mtoto huyo anacheza na baba yake mpya swali la kwanza.

1: hivi kweli wewe ni baba? Shemeji akajibu ndio.akamuuliza tena

2: kama wewe ni baba mbona Mimi na mama chiku nyingi tulikuwa tunalala peke yetu? Shemeji kimya, akamuuliza tena

3: chiku jote ulikuwa WAP?

Hapa mama yake mtoto ambae ni mdogo wangu alikuwa nje anapika. Akivyomsikia fasta akamuita njoo haraka sana.maswali yakaishia hapo.

Mdogo wangu akanipigia tulicheka sana sio kwa maswali Yale[emoji3][emoji3]
Mbona wewe hujazaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biblia imeandika vizuri.
Musa alikufa akafufuliwa yuko mbinguni
Ibrahim yupo alipozikwa

Mtu akifa amelala usingizi wa umauti.

Siku Yesu akija kila jicho litamuona. Watalatifu wataenda mlaki Mawinguni. Wenye dhambi watakufa mara ya 2
Unakwenda wapi kiongozi? Ili siku nyingine nisijekosea swali hili tena? Vipi akina Musa na Ibarahim wako wapi mpaka sasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ili limekua likinikumba mno nakujikuta naduwaa nakubaki nangata lips kwa nguvu nikiwaza

Nimekua nikiulizwa maswali mno na watoto nyumbani, ila maswali mengine nimekua nikiishia kugoogle maana majibu nakua nakosa, na ili nisionekane sijajibu swali uwa na mimi nawauliza maswali magumu niliyo jiuliza at age of 20's 😎 japo nawakomaza ila nikuweka ubora wasinione mzembe😑

Ila leo jioni hii nimekutama na swali ambalo kwa kweli ninaomba msaada kwa wana jamvi mtoto kaniuliza

"Je hivi sasa mtu akiwekwa sayari ingine akiwa yeye na mwenzie mdada au mkaka wataweza fanya haya yafanyikayo duniani sasa ikiwa pamoja na kutengeneza nyumba nzuri nguo, chakula, kujua wanyama yupi wakufugwa na yupi hafai kufugwa, kipi chakula kipi sumu, lipi jiwe lipi dhahabu au kito chochote?

Bila kupata elimu yoyote kwa mtu yoyote wa dunia hii!!! 😐

Kweli nimemwambia nitakuja na jibu badae acha nipumzike nimechoka ila sijachoka wala nini ila nimeona nikimjibu vibaya nitatengeneza nabii wa uongo apo badae

NB, kwa wenye watoto tu kama hauna basi soma tu majibu usijibu...
Baba, kwanini tulidai Uhuru toka kwa mkoloni?
Sikuwa na jibu la kumpa.
 
Back
Top Bottom