Swali gani gumu ulilowahi ulizwa na mtoto mdogo?

Swali gani gumu ulilowahi ulizwa na mtoto mdogo?

Tulipokuwa kuna mwanafunzi alimwuliza swali mwalimu "kama dunia inazunguka kweli kwanini hii darasa haizunguki? "

Mwalimu akajibu nitaelezea somo lijalo.Somo lijalo hakuigusa tena hilo swali
mwalimu wa jogi anashindwaje kujibu
 
Tulipokuwa kuna mwanafunzi alimwuliza swali mwalimu "kama dunia inazunguka kweli kwanini hii darasa haizunguki? "

Mwalimu akajibu nitaelezea somo lijalo.Somo lijalo hakuigusa tena hilo swali
mwalimu wa jogi anashindwaje kujibu
 
Pacha wangu wa kike aitwae Doyi mwenye miaka mitatu alimuona Kaka yake wa miaka sita akikojoa wima,sasa nadhani alivutiwa na ule mtindo wa kukojoa wima badala ya kuchutama.
Akaiingiza vidole kwenye suruali yake na akajipapasa kwa kisha akaniangalia usoni huku akiwa na huzuni akaniuliza:
"Baba na mimi nitengeneze kama huyu(kaka yake) niwe nakojoa nimesimama."
Ahahahaha
Sasa swali gumu lipo wapi hapo?
Doyi alitaka atengenezewe 'mdude'.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
YEYE: Baba kabla sijazaliwa mlikua mnanijua?
Mimi: hapana tulikua hatukujui kabisa
YEYE: sasa mlijuaje kama ndio mimi niliekua tumboni kwa mama?
Mimi: kimoyomoyo the kid has a point
 
Nipo mdogo hata sikumbuki umri wangu ulikuwa age gani ,ila kama kukisia ni 4-6, kuna mtu alikufa mtaani kwetu na nazani alikuwa jirani,nikamfata babu yangu ambaye alikuwa na mika 70+ kipindi kile miaka ya 90s,nikamuuliza " babu,mbona fulani amekufa?,yani yeye amekaa tu hadi anakufa! Ameshindwa kukimbia?,yani babu mimi sitakufa kabisa,yani hiyo siku nitakimbia hawatanipata kabisa,si unajua ninavyokimbia"

Mzee alitabasamu tu kisha akanambia kifo hakikimbiwi.Ila mimi yule marehemu nilimuona mzembe kabisa kwa kufa bila kukimbia na isitoshe nilikuwa namjua,nilibaki namulaumu kwa kutokuchukua hatua sitahiki za kutoka balu.Pia mimi nilikuwa naona nitakuwa mdogo siku zote ,yani wale wakubwa waliumbwa hivyo na mimi niliumbwa hivyo kadogo.

Pia nilipoanza la kwanza zile tarehe na mwezi zinabadilika ila mwaka haubadiliki,nikazua hoja tena kwa mwalimu,nikamuuliza mbona huku hakubadiliki kila siku tunaandika hivi hivi,akajibu huu ni mwaka,nikauliza mwaka ndio nini?,sikumbuki hata alinijibu nini.
 
Ili limekua likinikumba mno nakujikuta naduwaa nakubaki nangata lips kwa nguvu nikiwaza

Nimekua nikiulizwa maswali mno na watoto nyumbani, ila maswali mengine nimekua nikiishia kugoogle maana majibu nakua nakosa, na ili nisionekane sijajibu swali uwa na mimi nawauliza maswali magumu niliyo jiuliza at age of 20's [emoji41] japo nawakomaza ila nikuweka ubora wasinione mzembe[emoji58]

Ila leo jioni hii nimekutama na swali ambalo kwa kweli ninaomba msaada kwa wana jamvi mtoto kaniuliza

"Je hivi sasa mtu akiwekwa sayari ingine akiwa yeye na mwenzie mdada au mkaka wataweza fanya haya yafanyikayo duniani sasa ikiwa pamoja na kutengeneza nyumba nzuri nguo, chakula, kujua wanyama yupi wakufugwa na yupi hafai kufugwa, kipi chakula kipi sumu, lipi jiwe lipi dhahabu au kito chochote?

Bila kupata elimu yoyote kwa mtu yoyote wa dunia hii!!! [emoji52]

Kweli nimemwambia nitakuja na jibu badae acha nipumzike nimechoka ila sijachoka wala nini ila nimeona nikimjibu vibaya nitatengeneza nabii wa uongo apo badae

NB, kwa wenye watoto tu kama hauna basi soma tu majibu usijibu...
Mwambie sio sayari zote zina mazingira ya kuwezesha maisha kwa binadamu kama dunia, na ndio maana hatuishi huko. Akiuliza kwa nini, mwambie, nyingine zina joto kupita kiasi na nyingine baridi kupita kiasi.
 
Nina dogo wa kike ana 4years tunalala nae ndani kwenye chumba changu japo vitanda tofauti. Sasa nina kawaida kila asubuhi ninapojiandaa kwenda kazini lazma nioge pamoja na kujisaidia haja kubwa na ndogo, Choo kiko ndani ya chumba changu humohumo.

Siku hiyo niko chooni nasikia anamuuliza mama yake, Mama kumbe baba naye anakunyaga namuonaga kila siku asubuhi anaingia chooni

Tangu siku hiyo nikamhamisha dogo chumba
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jana Tunapata kifungua kinywa kamjomba kakaniuliza kwa Nini kwenye chai maziwa inatumika sukari kidogo kuliko kwenye chai ya Rangi......... Kapo Class One....nikaambia kwa sababu maziwa Yana Natural sugars..... Akaniambia natural sugar ndo zipi nkamwambia sukari asili akaniambia sijakuambia unitafsirie ...nikacheka ...nkamwambia kunywa chai ukacheze
[emoji1787][emoji1787]
 
binafssi katika vitu ambavyo siku ya kwanza nasikia vilinichanganya akilii kwamba siku naambiwa dunia duara sisahau mpaka leo.swali sasa inamaana kuna watu wanatembea kichwa juu chin wakati huo mm najua mvua ikinyesha inayesha dunia nzimaa😅😅😅
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom