Swali kwa Ayubu Rioba: Siku hizi sera ya Taifa inaruhusu taasisi za kidini kunufaika na fedha za walipa kodi kupitia TBC?

Umesema kweli sana.Huyu atakuwa sio mtanzania,karibia familia nyingi za kitanzania,wako nusu waislamu na nusu wakristo,na wanashirikiana kwenye misiba na furaha.
 
Wewe bado una mawazo ya enzi za mawe za biashara ya utumwa.Biashara ya utumwa,hakuna kabila halikuwahi kutoshiriki biashara hii duniani,wapo pia waarabu waliuzwa utumwani.Na sisi waafrika,yapo makabila yaliuza pia wenzao utumwani,kwa kuwauzia wageni.Unafikiri mgeni aataweza kufanya biashara bila baraka ya mwenyeji?
 
Nyie wafia dini mna matatizo makubwa sana.
Hakuna anayejishughulisha na watu wa dini moja kushirikiana na dini nyingine. Kinachopingwa na taasisi za serikali kama TBC kuwa jukwaa dini YOYOTE.

Wewe Sheikh nenda Redio Maria au Sauti ya Injili kawaombe wakupe kipindi cha kaswida au mawaidha na hakuna mtu atakayejisumbua na huo ushirikianao.
Umesema kweli sana.Huyu atakuwa sio mtanzania,karibia familia nyingi za kitanzania,wako nusu waislamu na nusu wakristo,na wanashirikiana kwenye misiba na furaha.
 
Ni akili ya ajabu kutaka kumtenganisha,mwenye dini kutumia baadhi ya miundombinu ya walipa kodi,na kumuachia huyo huyo atumie miundombinu mengine ya walipa kodi,kwa kisingizio cha dini.Umzuie asutumie Tv ya Taifa,huku anatumia barabara,shule,vivuko,viwanja vya michezo,viwanja vya ndege,madaraja nk
 
Huwezi kumtenganisha mlipa kodi,na alichokilipia kodi,kwa kukitumia kwa njia yoyote iwayo,madhali hajavunja sheria.
 
Duh! haueleweki.

Hicho kiswahili mbona nacho kina maneno kibao tu kutoka kwenye lugha zengine hata maneno ya kiarabu yamo humo ,sasa nashindwa kukuelewa?

Halafu huwezi kuweka makabila ya watu ukatoa imani zao.
 
Sioni kama unaelewa maana ya tunu ya uvumilivu. Jisomee tena bandiko, sehemu inayojadili pingamizi na jawabu lake.
 
Duh! haueleweki.

Hicho kiswahili mbona nacho kina maneno kibao tu kutoka kwenye lugha zengine hata maneno ya kiarabu yamo humo ,sasa nashindwa kukuelewa?

Halafu huwezi kuweka makabila ya watu ukatoa imani zao.
Taifa ni kitu kimoja chenye vitu vingi ndani mwake.

Umoja wake unatokana na sifa mtambuka (universals)

Kitu kimoja kimoja ndani ya Taifa, mfano kabila lako, kinatambulishwa na sifa za kipekee (particulars)

Kabila lako linazo sifa za kipekee zipi? Ni hizi hapa: Lugha ya kikabila, mila, na desturi zenu.

Taifa la Tanzania ni kitu kimoja kwa sababu ya sifa gani Mtambuka? Hizi hapa: Lugha ya Taifa, akili, utashi, vinasaba vya kibinadamu, serikali moja inayosimamia sera, sheria na taasisi zisizofungamanisha masuala ya kidini, nk.

Taasisi mojawapo ni TBC.

Hapo vipi?

NImeeleweka!
 
1. TBC ni chombo cha umma na kinachoendeshwa na fedha za walipakodi.
2. Walipakodi wa Tanzania ni waumini wa dini mbalimbali na wadau wa vyama mbalimbali vya siasa na pia wanatoka sekta rasmi na isiyo rasmi.
3. Kipindi chochote kinachowahusu Watanzania kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni (dini au imani ni sehemu ya utamaduni) kinaweza kurushwa na TBC kwa utaratibu usioweza kuleta manung'uniko kutoka kwa wadau wengine.
4. Kipindi chochote kinachowagawa Watanzania kwa namna yoyote ile hakipaswi kurushwa na TBC.
5. Vipindi ulivyovitaja kama havihusiani na No 4 havina shida kama vikirushwa na TBC maana wenye dini au imani hizo ni walipakodi pia na ni sehemu ya umma wa Watanzania.
 
Hiyo TBC umeijua leo kuhusu kujipendekeza?
Walakini nakuona wewe ni wale wenye wenye udini udini kwenye mbongo zao.
Kama wewe ni mkristo basi unapaswa kujua Kuwa UKRISTO unatangaza UPENDO na MSAMAHA.
 
3. Kipindi chochote kinachowahusu Watanzania kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni (dini au imani ni sehemu ya utamaduni) kinaweza kurushwa na TBC kwa utaratibu usioweza kuleta manung'uniko kutoka kwa wadau wengine.
Maneno "dini au imani ni sehemu ya utamaduni" yana utata.

Dini unayoitaja ni sehemu ya utamaduni wa kabila au ni sehemu ya utamaduni wa Taifa?

Tanzania tuna utamaduni wa kitaifa.

Lakini, Tanzania hatuna dini ya kabila.

Pia, Tanzania hatuna dini yaTaifa.

Kwa hiyo, hoja yako hapo juu unapata ubutu mkubwa, na kimsingi inakufa.

Irekebishe.
 
Sasa lugha ya taifa ambayo ina maneno ndani yake na mengi kutoka lugha za mataifa mengine hili unalizungumziaje?

Na yapi ni mavazi yetu kama taifa la Tanzania?
 
Hoja yako iko hivi:

  1. Kila mlipa kodi anayo haki ya kutumia miundimbinu ya walipa kodi kama vile barabara, shule, vivuko, viwanja vya michezo, viwanja vya ndege, madaraja, vyombo vya habari kama vile TBC, nk, endapo hiyo ni miundombinu ya umma;
  2. Vyombo vya habari kama vile TBC ni sehemu ya miundombinu ya umma
  3. Kwa hiyo, kumzuia mwenye dini kutumia TBC ambayo ni sehemu ya miundombinu ya walipa kodi na kumuachia atumie miundombinu mengine ni undumilakuwili.
Hoja yako ina tatizo moja. Hujasema huyo mlipa kodi anaruhusiwa kutumia miundimbinu hiyo kwa ajili gani.

Miundombinu ya umma ni maslahi ya pamoja. Muumini akipita katika barabara kwenda kwenye eneo lake la kusalia sawa.

Lakini akitumia barabara kama kituo cha sala ni kosa, maana anawakwaza wasioamini naye, kwa kuwazuia kuendelea na ratiba zao.
 
Sasa lugha ya taifa ambayo ina maneno ndani yake na mengi kutoka lugha za mataifa mengine hili unalizungumziaje?

Na yapi ni mavazi yetu kama taifa la Tanzania?
Lugha ya Taifa ni mali ya Taifa.

Neno la Kiingereza au Kiarabu likikopwa na kutoholewa linaanguka katika lugha mpya.

Mfano neno shirt limekopwa na kutoholewa likawa shati.

Hili sio neno la Kiingereza tena.

Ni Kiswahili.

Ni vivyo hivyo kwa mavazi.
 
Nawachukia wakristo kwa sababu wanajali dini yao kuliko watu, wamejaa unafiki. Akitawala mkristo hata akiua wanakaa kimya, watu wakipotea wanakaa kimya. Lakini mama ametufanya tutabasamu nyinyi mnanuna, alafu wanatulazimisha tusiyaone mema anayotutendea bali tumtazame kama muislamu na hivyo kumchukia yeye na mema yake.
 
Kumbe tatizo ni maandishi yaliyoandikwa chini ya TV screen eti

"MASHINDANO YA TAIFA YA QURAAN"
Mashindano ya taifa hiyo ndo nyuzi yenyewe, TV ya taifa ipo kwa ajili ya kutangaza habari za kitaifa whether ni mambo ya Dini, Siasa, Uchumi au Kabila. Chamsingi ni ukubwa wa habari.

Nahisi muandishi anasumbuliwa na chuki ya Udini. Natamani angetumia muda wake kuandika mambo muhimu yenye maslahi aachane na hizi chuki.
 
Utaumiza moyo wako kukaa na chuki za kijinga na kupumbavu, wape elimu mahali unadhani msimamo wao hauwasaidii, halafu wewe uwe na maisha meupeee moyoni mwako
 
Kwa ujumla mwandishi kaandika Andiko la kijinga lisilo pakegi ya yupi ndiye Mtanzania na yupi anastahili kuitumia TBC na nini maana ya Utaifa Kwa ujumla na Sura hiyo ya Utaifa inayo sehemu ipi ukitazama unauona huo utaifa

Anayelipa Kodi ili TBC ifanye kazi ni Nani, mwandishi na Andiko lake hajamtaja ni Nani mlipa Kodi anayesababisha TBC iwe hewani??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…