Tabia gani za walevi huwa zinakushangaza?

Ikawaaje aisee ulilifuata asubuhi
 
😂😂😂😂
 
Sahihi kabisa. kuna kipindi nilipitia joto la maisha wahuni walikuwa hawaniachi kwenda kula bata tena hoteli za gharama nikabahatika kupata connection ya kazi kupitia vibopa hawa asee mlevi siwezi muona wa hovyo hata siku1.
Kuna jamaa tulikuwa tunamuita Dangote alikuwa kota wa dhahabu yule fala anaweza kuwaua kwa pombe iwe nyama hata kama starehe yako ni mademu jamaa alikuwa hana hiyana. Msela alikufa na ajari ya ajabu kweli wanatoka kwenye mizunguko wakakuta maji yanapita juu ya barabara si wakasemezana na mwenzake maji haya yanapitika kwa gari ndo ukawa mwisho wao.
 
Mke wangu akilewa anaanza kufukua makaburi ntatukanwa hata majanga ya mwaka juzi yatafufuliwa siku hiyo na hapiki nguvu anakua hana nishazoea
Balaaa zaidi kukojolea godolo aisee mtu ana mtoto mchanga kalewa na pempasi hajamvesha katoto kakojoe na yeye aisee godoro langu lina ramani ya dunia mpaka sayari zingine zote.
Siku izi akilewa namvesha mwanangu pempasi yeye analala sakafuni mpaka pombe zimuishe na akakojoe toi ndo apande kwa bed.sitaki maujinga ujinga hayo mimi
 
Na Bado mnalewa 😂😂
 
Mie nikilewaga tu nakumbuka kifo cha marehemu babu naanza kulia kwa sauti
 
MAji yameua raia wengi sana hasa kwenye madaraja yasiyo na kingo.kuna mwamba nae alikua kalewa ni bosi wa daradara dereva kamwambia hatuwezi pita hapa maji yamejaa bosi na pombe kamtukana dereva akamwambia niachie siti mwamba akafosi kupita walisombwa na maji.akaua abiria kibao ilikua wilaya ya kwimba mwanza
 
Hatari sana. Kuna siku naenda chato nikapita katoro pale nikapiga kama bia5 hivi halafu nikapanda haice kufika huko mbele konda si kaanza kudai nauli nikamwambia nitakupa nikifika wala hakuwa msumbufu. ile nafika sijui ilikuwaje tu nikamwambia wee maskini mbwa wewe unaniabisha kwa kuniomba nauli nauli yenyewe ni kidogo asee nae akapnic wacha wanichangie kunipiga palichangamka pombe ikaisha nikatimka mbio hadi nikaangukia kwa Traffic. Sitasahau kabisa halafu trafic mwenyewe alikuwa mwanamke sijui angenisadia vipi. Acha tu
 
Ha ha ha ha katoro wanga wengi ungeendaa piga bia malendeja bar ushirombo
 
Kila siku unakutana walevi wageni?
Ikiwa hapana upande wangu hakuna kitakachoningaza kutoka kwa mlevi.
 
Kitu kizuri wanakubali kuwa zinakimbilia chini Yani mtu kunambia mwanaume au mwanaume mlevi sio mzinz Huwa nakataa kabisa labda anakunywa nyumbani
Nyumbani anaweza mbaka dada wa kazi.
Mie nawasiwasi hawa jamaa de liboloz zao hazifanyi kazi mpaka wagonge monde bora mie nankibamia changu kinasimama chenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…