Tabia ya Hawa wafanyakazi wenzangu, inaninyima raha

Wambie kuwa leo siendi goba,wakibisha benda nao huko waache parking waangakie sinema zetu we endelea na ratiba zako
 
Hii ni ishara ya udhaifu kitu chako nacho una kililia humu , Bila shaka nyie ndo wale ambao ata mkiombwa pesa na mwanamke hata kama huna uwezi sema sina na upo tayari uka kope uumpe
 
Msaada au lift hailazimishwi..ni kweli tunasaidiana lakini tusijiendekeze! Ikitokea mara moja moja sawa... kusaidiana kupo ila busara itawale..

Sema mletaa mada kama huna amani usibebe mtu ueleweke kua huzimiki hayo mambo hutaona mtu akijileta.... usijistukie ..mbona mimi siombwi lifti ila tu watu wanajuaga sipendi haya mambo ya ujima..navimba mwenyewe kwenye chuma la watu 7.

Siku nikiwa sina gari hua nakwea mwendokasi
.bolt au bajaji sisumbui mtu.
 
Hyo kitu inakela kwakwel, nina boxer yangu natoka mishemishe nina mzigo mkubwa pia nimepata abilia njian..
Nikapigwa mkono njian na mdada tunafahamiana nae anaomba lift jaman nikamwambia nafas hamna ila kakomaa ikabid akae juu ya mzgo mda huo njia ilikua ni kupanda mlima. ilipga mayowe pikipk mpaka niliihulumia.
Yey tukamwacha njian alifka, na bahat mbaya mafuta yakatuishia njian ikabid tusukume ila chanzo tumegawa lift.
 
Mkuu kwan anakuwa amekuomba akausindikize unapoenda ww au umsogeze anapoenda yeye? C unamwambia tuu kuwa utamshusha njian mana ww unaenda njia tofauti, Yn mm umenipa lift naanzaje kwenda huko unapokwenda ww.
Ipo Mimi nakuomba lifti wewe unsniliuza naenda wapi? Mimi nakujibu kwa kukuliza kwani wewe unaenda wapi ili swali linakua la kimtego ili usininyime lifti, Popote utapsema unaenda basi mimi nitasema utaniacha sehemu fulani.
 
Kuishi na watu hutakiw kuishi kinyonge,inatakiwa wakat mwingine ujifunze kusema hapana,maana wengine hufanya makusudi ili watumie vitu vyako kwa kukuona wew huwa hukatai na kuna mwingine atakuja kuliharibu tu makusudi ili uteseke kulitengeneza wakat yeye akifurah

Siku ukiwa na ratiba zako uwe unaliacha nyumban
 
Wewe utakuwa na roho mbaya mkuu. Huku Afrika siyo ulaya huwa tunashirikiana.
Mfano unatoka posta unaenda mbweni ukimpa lift mtu ukamuacha mwenge unapungukiwa nini hapo?
Kanichangia mafuta? Anajua navyoondoka asubuhi napasua kichwa nilipe umeme au nijaze mafuta kwenye gari..... Kwenye hiyo dilema wanakuwepo?
 
Kanichangia mafuta? Anajua navyoondoka asubuhi napasua kichwa nilipe umeme au nijaze mafuta kwenye gari..... Kwenye hiyo dilema wanakuwepo?
Dah wanangu mna roho mbaya kinoma, mara nyingi anayeomba lift anakuwa pekee ake tena bila mzigo mkubwa wakiwa wengi n wawili tuu, sasa hapo n mafuta gani yatakayoingia kwenye matumizi kisa umempa mtu lifti?
 
Mleta mada pamoja na umasikini wetu ila hata wewe una udhaifu mkubwa sana, unashindwaje kuwaambia ukweli? Mbona options zipo nyingi tu.

1. Mkitoka ofisini pamoja, pitia filling station then waambie wachangie mafuta, mtu aliyezoea kutoa nauli ya 1,000 mwendokasi ukimwambia atoe 5,000 ya mafuta kesho harudi tena kwenye gari yako.

2. Waambie ukweli kama una safari zako binafsi, usikwepekwepe. Ujamaa ndio umetuharibu, tunapenda vya bure.

Nakumbuka siku moja tulikuwa kanisani mchana kukawa na trip fupi, wengine wakachukua boda, wengine bajaj, na kulikuwa na magari binafsi...jamaa wakapanda kwenye gari ya mwenzao, ile gari ni five seater, kuangalia hivi jamaa anaona nyuma wamekaa wanne. Akawaambia live, hii gari inabeba watatu nyuma, mmoja apungue.

Usiumie nafsi wakati unaweza kuwa huru kwa kusema ukweli.
 
Mtu akinunia gari kwa mkopo hua hataki hata kutoa lift. Hua anahisi mkopo unaongezeka 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Yn mafuta yaishe kisa kugawa lift ya mtu mmoja?

Dah 🙌 namshukuru Mungu sina usafiri ila sio rahisi kuomba lift kwa watu ndo mana sikutan na watu wenye roho mbaya kama hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…