Tabia ya kupiga simu zaidi ya mara mbili inakera sana

Tabia ya kupiga simu zaidi ya mara mbili inakera sana

Hii sio kweli mkuu, mimi tangu siku nilipoanza kumiliki simu sijawahi kuwa napenda kupokea simu, mara nyingi huwa napendelea mtu anitumie SMS inayojieleza hususani ikiwa ni namba ngeni, mara nyingi nikiona mtu ananipigia simu zaidi ya mara mbili bila kutuma ujumbe mfupi huwa na assume hamna jambo la msingi hapo
Inakera Sana kaka
 
Mm naongoza hasa nikiwa kwenye relationship iliyonishika[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaani Huwa Sina kias ni kukugongea calls muda wowote niwe mkweli[emoji23][emoji23]

ila Kwa pipo zingine hapana Huwa sipig sana naweza hata nisifungue missed call hata siku 2 Tena namba ngeni ndio sizipendi
Shangazii unayawezaaaa!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama sehemu hairuhusu?
Wewe nae acha kujikuta special sana aseeee kama unaona wewe ni wa ivyo basi uwe unaweka simu silent na uifunike usione kinacho endelea mpaka utoke kwenye io sehemu yako ambayo hairuhusu lasivyo basi wewe itakua ni wale washamba anaweka mwito wa simu on kila simu ikiita inasikika alafu analalamika kua anapigiwa sasa kwanini usiweke silent ili umtafute badae .

Watu tunakua kwenye vikao nyeti na simu zikipigwa tunawajibu kwa sms kua tutawasiliana badae nk. Sasa wewe unajikuta special kinyama kumbe hola.
 
Na huu ndo ustaarabu.

Kuna watu wanapenda ustaarabu, lkn wao hawawezi kuuishi. Shwain
 
Huwa nakata simu na block hapohapo nikikumbuka baadae nita unblock na kujua ulikuwa na shida gani bila kusahau kukukumbusha kwamba kupiga simu mwisho ni mara mbili kama haijapokelewa basi mwenyewe hajaiona au hataki
 
Hiyo Tabia anayo jamaa yangu fulani anakubip hata mara 4 na unakuwa busy na mambo mengine au muda wa maongezi unakuwa hakuna lakini yeye atabip tu. Akiona hauja repond atatafuta hata namba nyingine akupigie halafu hata analokwambia zaidi ya salamu tu au kuulizia jambo fulani aliloliona kwenye mtandao au kwenye group la whatsapp. Yaani huyu jamaa huwa simuelewagi sana halafu na amenizidi umri kama mwaka 1 na miezi mitano, na huwa namthamini sana kutokana na background yangu na familia yake.
Lakini kwenye simu hapo huwa ananikera sana
Kataa kubali ila itoshe kusema anatoka kanda ya ziwa ,sitaki kutaja kabila maana ni wajomba zangu 😀
 
Back
Top Bottom