Tabia ya wachezaji kutema mate uwanjani inanikera sana

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Katika vitu vinavyonikera na kunitia kinyaa ni tabia ya wachezaji kutema mate uwanjani,. Najua sometimes kuna sababu(jasho kudondokea mdomoni, n.k), ila lazima kuwe na hatua za ku-discourage hii tabia ili vitendo hivi vipungue viwanjani kwani inatia kinyaa sana,

Wachezaji wenyewe ndio waathirika zaidi pale wanapoanguka au kukaa chini uwanjani kwani wanakalia uchafu bora jasho ambalo haliepukiki,

Tutajifanya kutetea kwa kutoa sababu mbalimbali kwasababu hii ni soka lakini ni ukweli mtu mzima hata ukiwa kwenye kundi la watu huwezi tu kugeuka na kutema mate bali kwa mtu mstaarabu utasogea pembeni kabisa kutema mate tena huku nafdsi ikiwa inakataa, kukusuta na hata kuona aibu.

Wakati umefika FIFA waanzishe kampeni ya ku-discourae hii tabia katika mchezo wa soka ingawa ni vigumu kuiepuka kwa asilimia 100. Hata hivyo, kitendo tu cha kuiponda hii tabia, itapunguza tabia ya wachezaji wanaotema mate uwanjani kwa mazoe tu(wanatutia sana kinyaa).

Ushauri:viwanja viwe na sehemu maalumu za faragha kwa wachezaji kwenda kutema mate na kurudi uwanjani jirani na maeneo wanayokaa wachezaji wa akiba na mabenchi ya ufundi.
 
Ndugu Salary Slip umeshawahi cheza mpira au kushiriki mchezo wowote ule? elewa pale uwanjani kuna shughuli nzito mno kiasi kwamba mtu anakuwa sio kama wewe uliyekaa hapo kwa mume wa dada yako unatazama mechi. Kutema mate haiepukiki kwa mcheza soka au mwanariadha anapokuwa kwenye kazi yake. Ninakushauri wakati mwingine andika hata uzi wa mapishi jinsi unavyopika hapo kwa mume wa dada yako.
 
Katika vitu vinavyonikera na kunitia kinyaa ni tabia ya wachezaji kutema mate uwanjani,. Najua sometimes kuna sababu(jasho kudondokea mdomoni, n.k), ila lazima kuwe na hatua za ku-discourage hii tabia ili vitendo hivi vipungue viwanjani kwani inatia kinyaa sana.

Wachezaji wenyewe ndio waathirika zaidi pale wanapoanguka au kukaa chini uwanjani kwani wanakalia uchafu bora jasho ambalo haliepukiki.

Tutajifanya kutetea kwa kutoa sababu mbalimbali kwasababu hii ni soka lakini ni ukweli mtu mzima hata ukiwa kwenye kundi la watu huwezi tu kugeuka na kutema mate bali kwa mtu mstaarabu utasogea pembeni kabisa kutema mate tena huku nafdsi ikiwa inakataa, kukusuta na hata kuona aibu.

Wakati umefika FIFwaanzishe kampeni ya ku-discourae hii tabia katika mchezo wa soka ingawa ni vigumu kuipuka kwa asilimia 100 ila kitendo tu cha kuiponda hii tabia itapunguza tabia ya wachezaji wanaotema mate uwanjani kwa mazoe tu.
Mkuu unaona kinyaa mate, umewahi kuona mchezaji anaomba break akajisaidie haja ndogo wakati mechi inaendelea?
 
Katika vitu vinavyonikera na kunitia kinyaa ni tabia ya wachezaji kutema mate uwanjani,. Najua sometimes kuna sababu(jasho kudondokea mdomoni, n.k), ila lazima kuwe na hatua za ku-discourage hii tabia ili vitendo hivi vipungue viwanjani kwani inatia kinyaa sana,

Wachezaji wenyewe ndio waathirika zaidi pale wanapoanguka au kukaa chini uwanjani kwani wanakalia uchafu bora jasho ambalo haliepukiki,

Tutajifanya kutetea kwa kutoa sababu mbalimbali kwasababu hii ni soka lakini ni ukweli mtu mzima hata ukiwa kwenye kundi la watu huwezi tu kugeuka na kutema mate bali kwa mtu mstaarabu utasogea pembeni kabisa kutema mate tena huku nafdsi ikiwa inakataa, kukusuta na hata kuona aibu.

Wakati umefika FIFA waanzishe kampeni ya ku-discourae hii tabia katika mchezo wa soka ingawa ni vigumu kuiepuka kwa asilimia 100. Hata hivyo, kitendo tu cha kuiponda hii tabia, itapunguza tabia ya wachezaji wanaotema mate uwanjani kwa mazoe tu(wanatutia sana kinyaa).

Ushauri:viwanja viwe na sehemu maalumu za faragha kwa wachezaji kwenda kutema mate na kurudi uwanjani jirani na maeneo wanayokaa wachezaji wa akiba na mabenchi ya ufundi.
mimi enzi zangu nilikuwa sitemi tu mate bali hadi makohozi nayo nilikuwa nayatema na nilikuwa nikifurahishwa mno na kohozi likiwa linadondoka ardhini huku likiwa zito na la njano kabisa
 
Ndugu Salary Slip umeshawahi cheza mpira au kushiriki mchezo wowote ule? elewa pale uwanjani kuna shughuli nzito mno kiasi kwamba mtu anakuwa sio kama wewe uliyekaa hapo kwa mume wa dada yako unatazama mechi. Kutema mate haiepukiki kwa mcheza soka au mwanariadha anapokuwa kwenye kazi yake. Ninakushauri wakati mwingine andika hata uzi wa mapishi jinsi unavyopika hapo kwa mume wa dada yako.
Mbona unakuza mAmbo sana
 
Mazoezi (any physical activity) huzalisha kiwango kikubwa cha protini kinachoingia kwenye mate, aina hii ya mate huitwa MUC5B. Hii husababisha mate kuwa mazito zaidi hivyo kuwa ngumu kumeza na option rahisi inakiwa kuyatema.

Ndugu mleta mada hii ni science sio kuwa wanapenda na ingekuwa haijakuwa proved scientifically basi kutokana na masuala ya hygiene tungekuwa tunaona wachezaji wakiadhibiwa kwa uchafuzi wa mazingira.

Hebu jaribu kesho kufanya hata jogging ya kilometer 5 ulete mrejesho.
 
Nafahamu sana ila kama mchezaji anaweza kutoka na kwenda kugangwa nje wakati mechi inaendelea, itashindika nini kwa wachezaji kutoka nje ya uwanja na kukimbilia sehemu maalumu za kutema mate na kukimbia kurudi uwanjani?Kuwe na sehemu za faragha pembezeno mwa uwanja na mchezaji kuingia katika hizo sehemu asisubiri idhini ya refa bali awasiliane na wachezaji wenzake na akiona mazingira yanaruhusu anatoka faster anaenda kutema mate kisha anakimbia kurudi uwanjani au kutumia ile break ya kunywa maji kutema mate.
 
Hata VAR kuna watu waaliipinga ila leo imeanza kuzoeleka.
 
Wewe hata sheria za soka unazijua? mbona unaandika mambo ya hovyo sana?
 
Mkuu haya mambo yapo kisayansi, hata hali ya wachezaji kuwa aggressive uwanjani na kugombana imeshawahi kuelezewa kisayansi kuwa ni level ya testoreno inakuwa juu hivyo wachezaji wanakuwa na hasira haraka.

Kama sio mfuatilia wa sports science huwezi elewa haya mambo.
 
Hata VAR ililipingwa, Mfumo wa vyama vingi Bongo ulipingwa ,n.k. Hii ndio nature ya binadamu kupinga mabadiliko kwa kitu alicholizoe hivyo sikushangai na hata wakati naandika hii mada nilijua reaction ya baadhi ya watu itakuwaje.
 
Mkuu haya mambo yapo kisayansi, hata hali ya wachezaji kuwa aggressive uwanjani na kugombana imeshawahi kuelezewa kisayansi kuwa ni level ya testoreno inakuwa juu hivyo wachezaji wanakuwa na hasira haraka.

Kama sio mfuatilia wa sports science huwezi elewa haya mambo.
Mada haisemi wasiteme mate bali hoja ni wateme wapi/wateme vipi. Tatizo hapa ni mazoea tuliyonayo.
 
Ndugu Salary Slip umeshawahi cheza mpira au kushiriki mchezo wowote ule? elewa pale uwanjani kuna shughuli nzito mno kiasi kwamba mtu anakuwa sio kama wewe uliyekaa hapo kwa mume wa dada yako unatazama mechi. Kutema mate haiepukiki kwa mcheza soka au mwanariadha anapokuwa kwenye kazi yake. Ninakushauri wakati mwingine andika hata uzi wa mapishi jinsi unavyopika hapo kwa mume wa dada yako.
Akicheki Tv ya shemeji 🤣🙌🙌🤣

Juhudi za kiuno cha dada kinampa mpaka yeye ufadhili
 
Back
Top Bottom