DOKEZO TAHADHARI: Afisa TRA ahatarisha maisha ya wakazi Mbezi Juu Kwa Sanya kwa kujenga ghorofa 4 bila kibali, kwenye msingi dhaifu wa nyumba ya chini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Oyaa mbona jengo limesimama vyema tu? Nauhakika mafundi wa mtaani hawana uwezo wa kunyoosha ukuta hivyo. Hapa kuna tatizo na walalamikaji.
 
Na kweli ila huenda jina la kiwanja na mjengo kafanya kama Hakimi.
Hata huyo mama ake atafuatiliwa, unadhani hii case inahusu Gold digger?? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Boni analo hili.
 
Kuna watu wana roho za kimaskini jamani duuh hivi mtu unakuwaje na roho mbaya? mbona mimi siwezi kuumizwa na maendeleo ya mtu!

Kweli binadamu tunatofautiana!

Tafuta hela Mkuu ujenge na wewe lako.
Dear hapanaaa, hapa nakupingaaa watu wailoko huko kwa system wanatunyonya sisi wa chinii.

Mwanzoni nilikua nna mtazamo km wako. Ila lilipokuja kunikutaaa, nilibadili akiliii.

Wanyonge tunanyonywa had jasho, afu wao wana neemeka khaaah.
 
Kuna watu wana roho za kimaskini jamani duuh hivi mtu unakuwaje na roho mbaya? mbona mimi siwezi kuumizwa na maendeleo ya mtu!

Kweli binadamu tunatofautiana!

Tafuta hela Mkuu ujenge na wewe lako.
Umeelewa kilicholalamikiwa?
Ghorofa nne ilipaswa kuwe na bango nje la kuonyesha details za jengo. Wao wanaohoji usalama wao wapo sahihi, goba mwaka Jana limewahi kuporomoka na majirani wakafa
 
View attachment 2630959View attachment 2630960

Afisa wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), Boniventure Pascal Madia (pichani), maarufu kama Boni amezua taharuki kubwa kwa wakazi wa Mbezi Juu kwa kujenga jengo la ghorofa 4 bila kibali cha Manispaa na bila kufuata viwango vya kitaalamu vya ujenzi na kutishia maisha ya wakazi hao kwa hofu ya jengo hilo kuanguka siku zijazo.

Wakazi wa Mbezi Juu/Goba bado wana kumbukumbu ya kuanguka kwa gorofa eneo la Goba kwa Awadhi mwaka 2021 na kuuwa watu wanne na sasa wanahofia maafa mengine kwenye Mtaa wa Nia Njema eneo la Mbezi Juu kwa Sanya.

Hofu ya wakazi wa eneo hilo ni kuwa afisa huyo wa TRA anajenga magorofa hayo chini ya viwango kwa kutumia nondo zenye milimita ndogo na mafundi wa mtaani bila kibali cha ujenzi cha manispaa.

Wakazi wa Mbezi Juu wanasema Boni alinunua nyumba ya chini iliyojengwa kwa msingi hafifu halafu akaigeuza kuwa jengo la gorofa 4 kwa kupandisha gorofa juu, huku akitumia mafundi wa mtaani, bila kibali cha ujenzi na bila kujenga msingi madhubuti unaoweza kujenga jengo la gorofa 4.

Hofu kubwa ya wakazi hao ni kuwa jengo hilo la gorofa linaloendelea kujengwa chini ya viwango huenda litadondoka siku zijazo na kuuwa watu kwenye eneo hilo.

Kila siku, wakazi hao wanapigwa na butwaa kuona afisa huyo wa TRA akiongeza gorofa kupanda juu kwenye jengo hilo, huku wakijua kuwa limejengwa kwenye msingi hafifu wa nyumba ya chini.

Viongozi wa serikali ya mtaa wa Mbezi Juu Kwa Sanya na Mtaa wa Nia Njema wameshindwa kuchukua hatua yoyote kuepusha maafa hayo na wanaachia gorofa hilo liendelee kujengwa bila kibali na chini ya viwango na kuhatarisha maisha ya wananchi.
Kwanza TAKUKURU/Sekretariati ya Maadili waanze na huyu wamfanyie Lifestyle audit. Kulinganisha kipato chake na uwekezaji anaoufanya.

Huyu atakuwa kwenye kutengo ambacho anakamua rushwa sana kutoka kwa wafanyabiashara
 
View attachment 2630959View attachment 2630960

Afisa wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), Boniventure Pascal Madia (pichani), maarufu kama Boni amezua taharuki kubwa kwa wakazi wa Mbezi Juu kwa kujenga jengo la ghorofa 4 bila kibali cha Manispaa na bila kufuata viwango vya kitaalamu vya ujenzi na kutishia maisha ya wakazi hao kwa hofu ya jengo hilo kuanguka siku zijazo.

Wakazi wa Mbezi Juu/Goba bado wana kumbukumbu ya kuanguka kwa gorofa eneo la Goba kwa Awadhi mwaka 2021 na kuuwa watu wanne na sasa wanahofia maafa mengine kwenye Mtaa wa Nia Njema eneo la Mbezi Juu kwa Sanya.

Hofu ya wakazi wa eneo hilo ni kuwa afisa huyo wa TRA anajenga magorofa hayo chini ya viwango kwa kutumia nondo zenye milimita ndogo na mafundi wa mtaani bila kibali cha ujenzi cha manispaa.

Wakazi wa Mbezi Juu wanasema Boni alinunua nyumba ya chini iliyojengwa kwa msingi hafifu halafu akaigeuza kuwa jengo la gorofa 4 kwa kupandisha gorofa juu, huku akitumia mafundi wa mtaani, bila kibali cha ujenzi na bila kujenga msingi madhubuti unaoweza kujenga jengo la gorofa 4.

Hofu kubwa ya wakazi hao ni kuwa jengo hilo la gorofa linaloendelea kujengwa chini ya viwango huenda litadondoka siku zijazo na kuuwa watu kwenye eneo hilo.

Kila siku, wakazi hao wanapigwa na butwaa kuona afisa huyo wa TRA akiongeza gorofa kupanda juu kwenye jengo hilo, huku wakijua kuwa limejengwa kwenye msingi hafifu wa nyumba ya chini.

Viongozi wa serikali ya mtaa wa Mbezi Juu Kwa Sanya na Mtaa wa Nia Njema wameshindwa kuchukua hatua yoyote kuepusha maafa hayo na wanaachia gorofa hilo liendelee kujengwa bila kibali na chini ya viwango na kuhatarisha maisha ya wananchi.
Anapata wapi hela nyingi hivi?
 
Leo kwa kustaajabu sana, nimepokea meseji 4 kwa mpigo kutoka TRA eti wananiita ofisini nikakutane na meneja kuhusu kodi ya mwaka jana hadi juzi. Yaani haya majamaa kumamake wana nia gani na mimi? Niende ili wanikamue nichangie miradi yao binafsi? Huyu kijana kapata wapi pesa ya kujenga nyumba ya gorofa 4 kwa mshahara wa serikali? Halafu kwanini waniite ofisini wkt sina kampuni wala sina biashara yoyote niliyoandikisha kisheria?
 
Ulishawahi kuona mtoto wa bilionea anaajiriwa hovyo hovyo ?.

Ukiuliza huyo Bon anafanya biashara gani na analipa kodi iasi gani utabaki kushangaa na kusikitika.
Leo hii hakuna trafic asiyekuwa na usafiri wa uhakika,nyumba nzuri kwasababu ya rushwa za barabarani,jiulize kwanini askari anyelinda bank hana hata baskeli !.

Nchi yetu inahitaji viongozi watakao kuwa tayari kupambana na mifumo ya rushwa.
Kwa Dar huu ni mtihani WA kwanza WA Mheshimiwa Mkuu WA Mkoa Chalamilla, hao polisi WA usalama waliongezwa mara kumi na Makonda, sasa ni Muda muafaka kuwapunguza Kwa kupangiwa Majukumu mengine, ila Rushwa ya Hawa Ndugu inatisha
Mwenye ile Video ya Makonda atuwekee hapa kuhusu polisi
 
Back
Top Bottom