Taja Taasisi ya Serikali ya Tanzania ambayo ilipaswa ifutwe mara 1 bila majadiliano ya Bunge

Taja Taasisi ya Serikali ya Tanzania ambayo ilipaswa ifutwe mara 1 bila majadiliano ya Bunge

Idara za Aridhi na mipango miji.!

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Ongezea na TUME ya matumizi bora ya ardhi, yaani hawa wamefeli kabisa kwenye issue ya kuhakikisha mipango ya matumizi bora ya ardhi za vijiji inafanya kazi na hivyo kuondoa migogoro isiyoisha ya ardhi kati ya wafugaji na wakulima.
 
Habari!

Serikali ya TANZANIA ina taasisi nyingi, ni zaidi ya 450 kama sitakosea.

Kila taasisi iliundwa kwa lengo na dhumini maalumu, ingawa baadhi ya taasisi zimefeli kwa % nyingi kutkana na uongozi mbovu wa taasisi husika au kukosa fedha za kuiendesha.

Kuna taasisi hazifai kabisa, zimeonyesha failure kwa kiwango kikubwa. Zilipaswa zifutwe haraka hata bila majadliano ya Bunge.

Binafsi BASATA ifutwe haraka.
Bodi ya chai
Mpiga chapa
Katibu tarafa
Bakita
Tbc
 
OSHA,
GAMING BOARD
Hizi zote hazina faida zaidi ya kuwanufaisha watu wachache na kulikandamiza kundi kubwa la watu,hamna taasisi zinapenda rushwa kama hizi
 
Habari!

Serikali ya TANZANIA ina taasisi nyingi, ni zaidi ya 450 kama sitakosea.

Kila taasisi iliundwa kwa lengo na dhumini maalumu, ingawa baadhi ya taasisi zimefeli kwa % nyingi kutkana na uongozi mbovu wa taasisi husika au kukosa fedha za kuiendesha.

Kuna taasisi hazifai kabisa, zimeonyesha failure kwa kiwango kikubwa. Zilipaswa zifutwe haraka hata bila majadliano ya Bunge.

Binafsi BASATA ifutwe haraka.
Hivi polisi ni taasisi?
 
NIDA wameupiga mwingi.
Kila mtu kajeruhiwa na NIDA
Nilienda NIDA kufatilia kitambulisho changu, jamaa namueleza shida yangu anarukia ulijiandikishia wapi? namtajia (Ni mkoa tofauti) ananijibu nenda ulipojiandikishia!

Nikamuuliza mzee kweli kuniangalizia kitambulisho kama kimetoka na kipo ofisi gani mpaka nisafiri safari ya masaa 12? Ilibidi niondoke tu na sijawahi fatilia tena natumia namba tu
 
Ndugu kwa ujumla tunaita taasisi hata vile vyombo sita vya Ulinzi na usalama tunaviita taasisi. Ingawa kwa namna nyingine neno taasisi linajitenga maana kuna ofisi zingine title zake ni TAASISI.
Siko hapa kubishana. Ni heri kila mtu abaki na analolijua
Kwa uelewa wangu mdogo mkuu wa taasisi zote ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, unaposema uliambiwa na mkuu wa taasisi zote, basi kaka we mtu mzito sana
 
Back
Top Bottom