TAKUKURU tunaomba Msaada: Kijana huyu alipata ajira Serikalini lakini akaporwa kituo cha kazi na kupewa mwingine

TAKUKURU tunaomba Msaada: Kijana huyu alipata ajira Serikalini lakini akaporwa kituo cha kazi na kupewa mwingine

Status
Not open for further replies.

Mkuu Liability pole kwa yote uliyopitia. Naomba usinipige mawe kwa nitayoandika hapa. Jambo lililokumba linaweza kabisa likawa ni kosa la kibinadamu tu na sio RUSHWA kama unavyodhani. Ukiangalia katika issue yako hakuna shaka yeyote katika hatua zote za awali (Usaili, kutangaza matokeo na uteuzi) unayoweza kuuelekeza TUME ya ajira. Ukiangalia kwa umakini utaona kwamba kilichotokea hapo ni kukosekana kwa mawasiliano mazuri kati ya maafisa wachache wa Tume ya Ajira na sio nia Ovu kama unavyodhani.

kilichotokea hapo ni kwamba Afisa mmoja anaita Interview ya nafasi fulani na Afisa mwingine anaangalia katika Database ya TUME na kumteua mwajiriwa wa nafasi ambayo watu wameitwa kwa interview. Unaweza usiniamini nilichoandika hapa lakini kama ukienda katika baadhi ya Taasisi za Serikali ukiwa kama raia wa kawaida jambo kama lako sio la ajabu.

Katika kujisomea kwangu kama mwananchi wa kawaida na ninapotembea banda la Utumishi katika maonyesho mbalimbali kuna kitu wanakiita maadili ya Watumishi/Utumishi wa Umma ambayo yamenifanya nipende kubakia tu Sekta binafsi na sio kukimbilia huko kwao. Kwa ulivyoandika hapo juu nachelea kusema kwamba huna maadili ya kuwa Mtumishi wa Umma. Nakushauri tu uungane na sisi katika Sekta binafsi.

Samahani kama nimetumia Lugha kali sana LAKINI hayo ndiyo mawazo yangu.

Ahsante
 
Nafikiri anahofia muda maana anasema hajapewa document yeyote ya yeye kusubiri
Ndugu yangu ajira za serikali huwa zinachukua muda..Kuna jamaa usaili alifanya mmwezi January mwaka Jana. Majibu ya usaili yalitoka Julai mwaka jana, kuanzia kazi ameanza mwezi huu.
 
Hana haki kwa kusema haki mkuu. Kwani ana mkataba tayari wa kuajiriwa kwamba alishaajiriwa??

Hata muajiri akisema sasa haajiri tena ameahirisha hakuna kitu anaweza akafanya hapo. Saa nyingine ni kuwa mpole na kuacha process ifanyike...
Umeongea point.
 
Mkuu Liability pole kwa yote uliyopitia. Naomba usinipige mawe kwa nitayoandika hapa. Jambo lililokumba linaweza kabisa likawa ni kosa la kibinadamu tu na sio RUSHWA kama unavyodhani...

Kwa hiyo hana maadili kwa kuwa amelalamika kuona kama haki yake imeporwa? Amejitahidi amefuata taratibu zote tena kwa gharama zake na haoni msaada, afanyeje? Kwahiyo kuwa mtumishi wa umma ni kuwa kondoo?
 
Mkuu Liability pole kwa yote uliyopitia. Naomba usinipige mawe kwa nitayoandika hapa. Jambo lililokumba linaweza kabisa likawa ni kosa la kibinadamu tu na sio RUSHWA kama unavyodhan...
Umeongea point hasa hapo kwenye MAADILI.

Nadhan hata wewe utaona kuna wakati mainjinia wanadhalilishwa na viongozi wa kisiasa hasa mawaziri lakini utaona wanakaa kimyaaaaa.

Na wengine mpaka wanatumbuliwa kabisa lakini baada ya siku kadhaa unawaona kazini tena!!

Hii issue ya maadili hii...

Na hapo wenda waka m-ref flag ma asishangae hata akipata nafasi hatakaa apewe nafasi za uteuzi kama ukuu wa idara etc..

Ila wenda mleta mada anaweza akapewa benefit of daught maana inawezekana bado hajaingia kwenye utumishi kwa hiyo bado haya mambo hayajui!!

Kama ikiwezekana afanye ufwatiliaji kimya kimya na ikiwezekana arudi tena utumishi uonane na mkuu wa utumishi umueleze kisa chake pia then atulie aache process ifwate!!

Pia ana option ya kudai kwa nguvu kama anavyo fanya lakin risk yake ndio hiyo, MAADILI!!
 
Umeongea point hasa hapo kwenye MAADILI.

Nadhan hata wewe utaona kuna wakati mainjinia wanadhalilishwa na viongozi wa kisiasa hasa mawaziri lakini utaona wanakaa kimyaaaaa...
Nimkama umesoma vizur hametoa sababu kwann analilia haki yake
 
Nicheki private nikuunganishe na muhusika
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wewe ndo unatakiwa umfate huyo jamaa mwenye Connection...Sio yeye "akuCheki"

Mcheki, halafu muunganishe na muhusika.
 
Umeongea point hasa hapo kwenye MAADILI.

Nadhan hata wewe utaona kuna wakati mainjinia wanadhalilishwa na viongozi wa kisiasa hasa mawaziri lakini utaona wanakaa kimyaaaaa...
Nimkama umesoma vizuri ametoa sababu kwann analilia haki yake
 
Haya mambo ya kazi magumu sana mtoa mada! We walishakupiga dafrau umepamabana sana sawa ila hio kesi ya kumshtakia mtumishi ukiwa mwananchi wa kawaida ni sawa na kumshitaki nyani aliekula mahindi yako kwenye mahakama ya Ngedere!

Pole mkuu walimwengu wabaya, afande sele aliwahi imba kunyang’anywa tonge mdomoni basi ndio kisanga cha aina yako komaa mungu atakusaidia kivingine pengine hata ungeipata hio nafasi usingeifanya kazi wa raha!
 
Mkuu pole Sana ,huyo bwana uliyemtaja nakumbuka na nimewahi kumuona akiambatana na GAIDI MBOWE Kwenye kampeni za 2020,nadhani kaingia kwenye nafasi hiyo kwa kutumia nguvu ya GAIDI MBOWE.

Allah akutie nguvu ili hili Jambo liishe salama oil sana ndugu yangu.

Narudia tena, Pole Sana,maana hapo inaonekana unapambana na mtu hatari Sana kwa nchi yetu.
 
Usikute dogo kapelekwa na kigogo hivyo kaona maji marefu usipime na kidole,

Nikikumbuka interview moja watu waliandika majina na kusaini kwamba walikuwepo lakini kesho yake jina la flani halipo kwamba hajahudhuria [emoji28], ilipigwa simu moja matata ikabidi warejeshe jina
Daa

Usicheze na kitu kinaitwa mamlaka😅
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom