Uchaguzi 2020 Tamaa za Wateule wa Rais kutia nia Ubunge zitawaponza wengi. Ushahidi huu hapa wa Rais Magufuli na Humphrey Polepole

Hapana mkuu imekuwa vigumu sana kufanya kazi na huyu baba kwa kweli haelewi hata ufanye nini. Ana mambo yake na anaweza tu akaamua kukutumbua tu bila sababu yoyote ile kwanini kufanya kazi naye si afadhali nigombee ubunge niwajibike moja kwa moja kwa wananchi wangu? Naye anapenda mno kuogopwa na kuabudiwa, hapana acha abaki peke yake.
 
Tusiwalaumu. Wanawasiwasi na nafasi wanazokuwa wanashikilia hasa baada ya uchaguzi mkuu.
 
Mbona yeye alikimbia ualimu akaenda kwenye siasa?.
 
Wa kule wa Dodoma kutumbuliwa juu ya kupenda wake za watu huku anafamilia. Wanaogopa kuharibiwa ndoa zao pia😃
 
Mimi nadhani ni vyema kuyaheshimu maamuzi yao hata mh. Rais naye tuliyaheshimu maamuzi yake alipoamua kugombea ubunge akaachana na ualimu
 
Kwann kwene hii awamu wateuliwa kwenda kutafuta ubunge inaonekana ni tamaa mara sijui wamemdharau rais....sio kweli mi najua siasa mbali ya kuwa ajira ni ndoto...Kila mwanasiasa ana ndoto yake ndani ya siasa kama ilivo kwa kazi zingine, huwezi mzuia mtu kwenda kwene siasa za kibunge eti tu kwasabab ulimpa ukuu wa mkoa hapana kabisa Kila mtu anandoto yake na maamuzi yake
 
Asinge kuwa na "Uchu na Tamaa ya Madaraka" asingefika hapo alipofika na kufanya ayafanyayo. Sijui wewe unatumia busara gani kuwananga watu wanaotimiza wajibu wao kikatiba.

Mbona yeye alikimbia ualimu akaenda kwenye siasa?.
Kuna watu hupenda kuimba nyimbo za huyu baba bila kuchanganya na za kwao. Wamepima wameona ni muda muafaka watoke-sasa hapo kuna shida gani. Pia nafasi walizo acha zitachukuliwa na watanania wengine.

Acheni wananchi waamue.
 
Katambi aliwahi kutamba na cheo cha uenyekiti BAVICHA taifa, baadaye akajilinganisha na karai la kuchengea ghorofa, ghorofa likikamilika kujengwa, karai hutupwa.

Katambi akajiunga chama tawala, baadaye Rais wetu mpendwa, akampa UDC, aliyepewa UDC hakuridhika na baadaye kakimbilia kutia nia.

Je, u-DC ni salary kidogo kuliko alichokuwa anapata kwenye uenyekiti wa BAVICHA? Au ndio tamaa ya kutaka kupata vyote haraka?

Karibu kwa maoni wadau.

Tanzania kwanza, vyama baadaye.
 
Hawa vijana tayari wamekwisha kupata "exposure" na kama walikuwa na akili za kiuchumi, watakuwa tayari wamekwishafanya "savings" za kutosha na hata kuwa na miradi kadha wa kadha ya kibiashara. Hivyo basi, wakiikosa bahati ya ubunge itawapasa waingie chimbo na kijiendeleza zaidi kielimu.
 
Wakati wanahamia kwenye chama chetu walidai kuwa hawahami kwa ajili ya kutafuta vyeo Bali wameridhishwa na utawala wa awamu ya tano chini ya uongozi wako.

Sasa ombi langu kwa kwako Ni Moja tu, kwa wale wote watakaoshindwa kufanikiwa Katika mchakato wa uchaguzi unaoendelea, usiwateue katika nafasi yoyote ile kwa miaka yote mitano, ili kuwapa fursa ya kukitumikia chama chetu wakiwa Kama wanachama wa kawaida. Lengo Ni kutaka kupima imani Yao kwa Chama, Kama kweli hawakuhamia CCM Kama njia ya kutafuta vyeo.
Ni imani yangu kuwa ombi langu litakubariwa
Asante!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…