Habari za wana bodi!
Nimeona nije niulize kwenu wanabodi ili angalau nijiridhishe na ninayowaza, kuwa nipo sahihi au hapana!
Nafasi za uteuzi ni za kudumu kama mteuliwa anafanya kwa uadilifu mkubwa mpaka pale atakapostahafu.
Tofauti na ubunge, mpaka wananchi waridhike na utetezi na hoja zako bungeni.
1. Makonda
2. Ole sendeka
3. D. Kafulila nk
Hawakusikia au hawakuelewa mwenyekiti wao alipotoa tahadhari au hawakuelewa?
Hawajui kuwa wakishindwa kwenye kura za maoni au kwenye uchaguzi mkuu hatima yao kisiasa na kimaslahi itakuwa imekwisha?
JE HUU SIYO MPANGO WA KUPATA WATU WENYE KUJENGA HOJA BUNGENI (hata kama ya kipumbavu)NA KUISIMAMIA?
JE SIYO MPANGO WA KWENDA KUBADIRI UKO WA URAIS?
Ninashaka mwenyekiti wao ameona bunge lijalo halita kuwa na wabunge wa ccm wabishi wa hoja, ndiyo maana umepangwa huu mpango.
Tukumbuke kwamba amesema yeye ndiye anayeweza kumtoa hata mtu wa chini kwenye kura za maoni na kumpitisha kuwa mgombe ubunge.
Karibu tutafakari
Mods, tafadhari msiufute uzi wangu wala kuuchanganya na uzi wowote