Licha ya Mkoa wa Mtwara kuwa na kituo chanzo kikuu cha uzalishaji wa Gesi asilia ,lakini mambo ni kinyume kabisa na mategemeo ya wananchi wa mkoa huu kwani tangia mwezi january mwaka huu 2017 kumekuwa na mgao wa umeme,katika maeneo mbalimbali umeme unakatika asubuhi na kurudi jioni au umeme kukatika jioni mpaka saa tano usiku.Mpaka sasa Uongozi wa shirika la Tanesco mkoa hawajatoa maelezo yeyote kuhusu mgao huu kuwa unasababishwa na nini na tatizo hili lini litakoma,cha kusikitisha hakuna chombo cha habari kilicho report juu ya mgao huu wa umeme mkoa wa mtwara ambao umekuwa kikwazo kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa Mkoa wa Mtwara.