Proof of address kwa mteja ni taarifa muhimu sana hasa katika utandawazi. Kama mteja akitaka kupewa lisiti ya aina hiyo ni vema akapewa au kukawa na utaratibu wa kutoa lisiti za aina hiyo Mara moja kwa mwezi au kwa maombi ya mteja.
Lisiti hizo kazi yake sio kusomea unit za umeme tu lakini wakati mwingine hutumika kumthibitisha mteja katika juu ya anuani yake. Hii kitu katika utandawazi ni mandatory requirements. Proof of address inafanywa kwa kutumia bili za utilities kama Maji, umeme na Gesi. Hivyo ni vema mkaliangalia hili Kama hitaji LA wateja wa katika ulimwengu wa utandawazi.
Mathalani, ukitaka kufungua akaunti za ebay, amazon, perfect money, okpay, adv cash etc, kwenye mitandao huwezi kuthibitishwa kama huna proof of address kutoka ama umeme au Maji. Na mnaweza kujaribu hili. Kwa dunia ya sasa hili ni hitaji muhimu kwa ajili ya online transactions. Ndio maana nasema matumizi ya lisiti yameongezeka na mtusaidie kuziboresha.
Maana sio kazi ngumu kuongeza field hizo kwenye report husika.