Asante kwa Taarifa Mkuu Tanesco.

Jitahidini hivi hivi inapendeza
 
CCM taifa hili limewashida hakuna jipya zaidi ya kuudanganya umma kua mnapendwa, nakumbuka wakati mnaingia madarakani 2015 mlisena kua matatizo sugu kama ya Umeme yatakua historia kwa uwepo wa basi kutoka Mtwara. Sasahihi ni mgao wa Umeme kimya kimya nchi nzima bila hata taarifa tofauti na zamani. Mnaogopa nini kuutangazia umma kua kuna mgao wa Umeme? Mnajua mnawaathiri vipi wananchi na biashara zao? Si bora mtu awe na raarifa ili aweke Sola au jrnereta kabisa kuliko usanii huu?

Mliingia kwa mbwembwe mkatimua Mkurugenzi mkuu wa TANESCO kwa madai kua anahujumu shirika, leo hii yapata miaka miwili serikali ya awamu ya 5 iko madarakani lakini matatizo ya Umeme yako pale pale, usanii mtupu. Mnashindwa nini kusema kua hali ni tete mkaeleweka? Kwanini mtaabishe wafanya biashara bila sababu hata hatuelewi nini kinaendelea.

Niulize, hayo mambo makubwa yanayofanywa ni yapi? Kufuta elfu 20 za ada za sekondari? Mambo makubwa ni kunyanyasa watumishi wa umma ambao hawapati stahiki zao kwa hadaa za nyongeza kiduchu cha mishahara?

Naamini, bila CCM kuondoka madarakani wananchi wataendelea kuteseka maisha yao yote huku wachache wakiendelea kuneemeka maisha yao yote.
 
Nimesikia wanaukusanya na kuuhifadhi ili siku ya kuzindua treni ya umeme usije kukatika maana serikali yote kuanzia sizo mwenyewe itasafiri kwa treni kwenda mwanza na kurudi... So wanaapply ile formula ya "akiba haiozi" TANESCO
 
Kwa kweli hili ni janga kubwa na bora kuwe na taarifa ili tujipange nimetoka nyumbani almost 26km kuja kibaruani nafika hamna umeme na jana kulikuwa hamna umeme pia Tanesco na wahusika wote
 
Huku kwetu ni balaa yanii ni bora mtu uwe na taarifa. Ofisi yetu kwa mwezi umeme wa Tanesco tunalipa wastani was laki moja na nusu lakini tokea shida imeanza takribani wiki mbili sasa wastani kwa wiki tunatumia mafuta ya shs laki mbili kwa ajili ya kuendesha genereta na uzalishaji umepungua

Nidhamu ya woga ni mbaya sana.. Au kwa sababu ikulu kuna umeme 24/7 ndo manaana tanesco inaogopa kutangaza mgao was umeme? Watu wanaogopa kutangaza mgao wa umeme kisa kuogopa kutumbuliwa.
 
Habarini za asubuhi wanajamvi,,na imani mupo salama kabla simu yangu haijazima kutokana na matatizo ya MGAO WA UMEME KUANZIA SAA 1 ASUBUHI HADI SAA 12 JIONI ningependa tu kuwashauri tununue POWER BANK
 
MAHANJU

Bunju umeme nimetoka washakata hadi tegeta na viunga vyake,,nadhani kuna mgao rasmi sasa
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…