TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Enzi za prof Muhongo umeme ulikuwa unakatika kwa nadra sana.hashitagi bringbackmuhongo
 
  • Thanks
Reactions: nao
Wakuu huu mgao wa umeme wa siri siri japo unaonekana kwa macho.. Nasema wa siri kwasababu huana maelezo ili watu tujipange kwa kununua ma generator.. Kwa mfano huku mbeya umeme ni kawaida kukatika sa mbili hasubuhi na kurudi sa tano usiku.. Ikumbukwe umeme kwa hii miaka ni muhimu sana kwa shughuli za viwanda vyetu vidogo vidogo kama saloon, welding n.k

Swali nnalo jiuliza ni nani wa kutumbuliwa kwa huu uzembe wa mgao wa umeme usio na kifani? Maana kama kutumbua kwenye sector ya umeme tumetumbua sanaaa hivi sahivi ni zamu ya nani!?

Na anayejua sababu ya umeme kukatika na huu mgao wa kutisha ni ipi?

nchi ya viwonder
Mwenye Nchi yake
 
Mambo kama haya Chadema ndo yalipaswa kuyatolea matamko, lkn kwenye matatizo ya msingi ya watanzania Chadema hujificha, ila akikamatwa Heche polisi, hayo matamko utakayoyasikia sio ya Nchi hii
 
Tumeipokea kwa hatua zaid
Kila siku mnakatakata umeme, haya juzi hitilafu tumekubali!

Lakini kabla ya hiyo juzi umeme mlikuwa mnakata na taarifa za kwa nini mnakata hamtoi.

Leo mmekata tena, je na hiyo ni hitilafu?

Tuambieni kama ni mgao tujue, tujinunulie majenereta au mnaogopa kutumbuliwa?

Acheni kufanya kazi kwa uoga na kuficha ficha uozo ili muonekane mnafanya kazi!

Nyakati za hapo awali mlikuwa mnatuambia kama kuna mgao basi tunajua.

Lakini hivi sasa mnafanya kazi ili kumfurahisha mkulu,ili apate sifa aonekane anapiga kazi na hakuna tatizo la umeme...!

Lengo la kuja humu jf ni pamoja na kutoa matongotongo tuliyonayo kwa kutupa ukweli...
Mgao upo ama haupo???
 
Sina Umeme kwa sasa najipanga punde niwe na umeme wangu
Nikushauri kitu,weka umeme wa TANESCO

tumia hiyo njia mbadala wakati wa matatizo kama haya.
Ukitaka kuelewa kitu ninachokwambia zungumza na wenye viwanda uone gharama wanazoingia
wakiendesha generator kuendesha mitambo Vs gharama za tanesco.

japo wawekezaji wengi sasa wameamua kutumia generator
zinazotumia gesi asilia hizi uendeshaji wake ni nafuu kuliko ya diesel.
 
*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)*

*TAARIFA YA KUANZA KUREJEA KWA UMEME *

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake kuwa umeme umeanza kurejea katika Mikoa ya Dodoma, Iringa na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Tanga.

Jitihada zinaendelea kuhakikisha huduma ya umeme inarejea katika maeneo yote nchini.

Tutaendelea kutoa taarifa zaidi.

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka

Kwa mawasiliano zaidi

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetultd
twitter.com/

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu

01/12/2017
 
Badala ya kuwaachia watu binafsi washughulike na utengenezaji wa nguzo, wao wajikite kwenye uzalishaji na usambazaji wa umeme, wanajiongezea majukumu!!
Tanesco ni pasua kichwa mramba embu rudi tu
 
Tanzania ya magu, Tanzania ya viwanda, tutafikaje kwenye uchumi wa kati kwa style hii? Magu acha kutudanganya?
 
Ninaomba kujua kama kwa sasa niko katika tariff 1 nikitaka kuhama kwenda tariff 4 je kuna malipo ninayotakiwa kulipia?

Maana kuna watu zaidi ya watatu nimeona wametakiwa kulipia elfu 25 ili kurudishwa kwenye rarif 4
 
Watanzania bhana, unauliza chooni kunanuka nini wakati unatoka huko huko?

Matendo hukidhi maridhiwa kuliko maneno shekh....

Mgao sio mpaka tuambiwe, umesahau wamejitoa kwenye serikali yenye uwazi?

Unataka watangaze mgao ili nao waonekane wameshindwa?

Hii ni serikali ambayo iko KIKI-ORIENTED.

NB: Arusha Sakina umekatika saa tatu asubuhi.
.....
.....Kamanda Kiki kwanza umeme sio kipaumbele chetu
 
Mambo kama haya Chadema ndo yalipaswa kuyatolea matamko, lkn kwenye matatizo ya msingi ya watanzania Chadema hujificha, ila akikamatwa Heche polisi, hayo matamko utakayoyasikia sio ya Nchi hii
KWANINI NYIE CCM AMBAO MNAJISIFIA MNAPENDWA NA WANANCHI HADI KUPATA KATA 42 MSITOE MATAMKO? AU CHADEMA TU NDIO WANAUMIZWA NA MATATIZO YA WANANCHI
 
Huku upanga wametukatia.

Yaah!!! Huku Masaki umeme hukatiki tumeunganishwa na laini ya whitehouse, so pambaneni na hali zenu, hakuna namna...

images
 
Back
Top Bottom