TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tanesco veeeepeee mnaogopa kutumbuliwa upele? tafuteni uongo wa kutuambia basi mbona wenzenu TRA wanadanganya kwenye mapato kila mwezi? Mnashindwa kutuambia sie wajinga kuwa nyenyere wameingia kwenye electric dynamo ndiyo maana kuna mgawo wa umeme?
 
Huku Mbezi beach washakata tayari!!

Jana usiku pia walikata kuanzia saa 12 jioni hadi kwenye saa saba usiku.

Leo hii wamekata mapema...saa nne kasoro tu!

Eff them.
Kumbe mitaa yafanana.

Jana mbezi beach hapa niishipo umekatika saa 1 asubuhi, ukarudi saa 3.
Saa 2 usiku ukakatika.... Sijui hata ulirudi saa ngapi.

Leo kariakoo umekatika saa 4 hadi Sasa bila bila..
 
Tanesco veeeepeee mnaogopa kutumbuliwa upele? tafuteni uongo wa kutuambia basi mbona wenzenu TRA wanadanganya kwenye mapato kila mwezi? Mnashindwa kutuambia sie wajinga kuwa nyenyere wameingia kwenye electric dynamo ndiyo maana kuna mgawo wa umeme?
.....
.... hahahaha Mkuu umevunja bendi
 
Kumbe mitaa yafanana.
Jana mbezi beach hapa niishipo umekatika saa 1 asubuhi, ukarudi saa 3.
Saa 2 usiku ukakatika.... Sijui hata ulirudi saa ngapi....
Leo kariakoo umekatika saa 4 hadi Sasa bila bila..
......
....makiki kwanza
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

*TAARIFA YA KUANZA KUREJEA KWA UMEME *

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake kuwa umeme umeanza kurejea katika Mikoa ya Dodoma, Iringa na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Tanga.

Jitihada zinaendelea kuhakikisha huduma ya umeme inarejea katika maeneo yote nchini.

Tutaendelea kutoa taarifa zaidi.

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka

Kwa mawasiliano zaidi

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetultd
twitter.com/

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu

01/12/2017
Shirika la kipumbafu sana kuwahi tokea duniani....yaani ni biashara ambayo Wateja wapo tayari kwa huduma , lakini supplier anashindwa kutosheleza demand.

Hili shirika ni la hovyo sana ,bora magu alifute tu kama mifuko ya hifadhi ya jamii.
 
Ndugu husika na kichwa hapo juu.
Mimi ni mkazi wa tabata nauliza tu. Huku kukatika kwa umeme mpaka lini kutaisha??
Leo ni siku kuu vipi mbna mnanitenda sivyo?!
Sina hela la jenereta??
NAULIZA MTARUDISHA SA NGAPI UMEME??
 
Wakuu huu mgao wa umeme wa siri siri japo unaonekana kwa macho.. Nasema wa siri kwasababu huana maelezo ili watu tujipange kwa kununua ma generator.. Kwa mfano huku mbeya umeme ni kawaida kukatika sa mbili hasubuhi na kurudi sa tano usiku.

Ikumbukwe umeme kwa hii miaka ni muhimu sana kwa shughuli za viwanda vyetu vidogo vidogo kama saloon, welding n.k

Swali nnalo jiuliza ni nani wa kutumbuliwa kwa huu uzembe wa mgao wa umeme usio na kifani? Maana kama kutumbua kwenye sector ya umeme tumetumbua sanaaa hivi sahivi ni zamu ya nani!?

Na anayejua sababu ya umeme kukatika na huu mgao wa kutisha ni ipi?

nchi ya viwonder
Alijisemea Prof Muhongo, tusubiri baada ya muda tutamkumbuka. Wale wanaokumbuka vibanda vya simu za mkononi ukipita posta na baadhi ya maeneo mengi ya miji midogo na makao makuu ya wilaya utavikuta vingi vimeinama kwa uchakavu. Mark my words, kwa kauli ya Muhongo, ipo siku nguzo za umeme zitageuka kuwa "tuliwahi kuwa na umeme miaka ya 2017". Wakati huo tunawahadithia wajukuu zetu amabo kwa wakati huo kibatari ni kawaida. Haiwezekani udanganye watu umejenga viwanda 3006 huku ukiwa una power shading ya aina hii. shame!
 
Umeme ni mchache na huo mchache utakuwa Luangwa sasa hv kwenye Maulid,pambana na majoto tu mkuu.
 
hilo lishakua janga la taifa si huko tu
 
Hivi makonda hauoni huu umeme akatia mkwara ili usikatikeili apatie kiki
 
Lengo la Uzi huu ni kufikisha ujumbe kwa wahusika kuwa Mgao upo hata Kama hawasemi wazi kuwa upo.

Kwa hiyo Kama hapo ulipo umekatika sema na ukirudi sema.... Kwa Muda wa siku mbili tu tutakuwa tumeshapata data za kutosha kuwaambia wahusika kuwa watangaze wazi Mgao wa umeme na wasifanye Siri kwa sababu madhara ni Mengi kwa wajasiriamali na hata viwanda vikubwa.

-kwa kuanzia tu.... Hapa nilipo wameuchukua tangu saa mbili asbh.

Karibuni....

NB Kama kuna madhara umepata kwa Mgao huu, Povu ruksa.... Sio matusi lakini.
 
Hahahaaaa kuna Uzi wao kule....... Lakin huku wakiingia ni mapov mwanzo mwisho
 
Naona tumuombe Mr Musk wa tesla atusaidie
Lile battery kubwa Australia limeanza kupiga kazi
 
Back
Top Bottom