Tumejenga viwanda 3000 ndani ya miaka miwili,ccm woyeee awamu ya kutafuta kiki za kitoto
 
Kabisa aisee prof muhongo alikua mtu sahihi kwenye hii wizara.umeme ulifika mpaka vijijini.ni kweli alikua na mapungufu yake but maadamu tulipata umeme haina shida.wamrudishe tu hamna namna

Hatupaswi kujivunia Mtu flani badala Yake tunapaswa kujivunia mifumo thabiti na imara ambayo kupitia hiyo Mtu yeyote wa wastani (average person) anaejielewa na Mwenye weledi anaweza kuendesha Shirika kwa kushirikiana na wengine ili tuweze kuwa na uhakika wa kupata huduma kwa kila mwaka mzima (throughout the year).
 
Tumeingia kwenye janga hili sabb ya mihemko ya serikali hii. Ikumbukwe Songas walizima mitambo yao toka Mei 2016 baada ya bwana magogoni kutoa kauli za vitisho na hatimaye uongozi wa Tanesco kuogopa kuwalipa.

Haya ndiyo matunda ya ubabe sasa tutalinywa tupende tusipende
 
Yaani toka mkuu alipo mfukuza muhongo nishati na madini pamekuwa ni mapango ya wezi na wanyang’anyi
Hii nikweli hata mimi nimeiona baada ya mhongo tu kuondoka katikakatika ya umeme bila mpango ikaanza.
 
Nchi ipo gizani, Waziri wa Nishati mpaka sasa upo kimya, haujatoa walau tamko kwetu wananchi kutujulisha nini tatizo. Tunakuwaje Nchi ya Viwanda wakati Umeme wa uhakika haupo. Huo uzalishaji utafanyikaje? Nafikiri unapaswa kujitathimini zaidi ikiwezekana ujiuzulu kabisa kwani umepwaya sana katika nafasi hii.
 
Mafundi wa ushonaji wenye vyerehani hawapigi kazi muda huu

Ova
 
Serikali ya wazalendo na viwanda wanaficha mambo wazalendo
 
Bora usiwake tujue moja na watuambie, sio wanatusababishia hasara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…