Naomba ufafanuzi nina tatizo,Mita yangu ya luku ilikua imeharibika nikaenda kutoa taarifa kwenu, nikabadilishiwa lakin baada ya kupata usumbufu mkubwa sana, sasa baada ya kuwekewa mita mpya nilipewa unit 50 offer kwa minajili kwamba zikiisha nitazilipia hela za izo unit nilizopewa then ntanunua za kwangu.

sasa cha kusikitisha ni kwamba kwenye mita ya sasa unit zinakwenda si kawaida tofaut kabisa na matumizi yangu, kwa maana matumizi yangu ni madogo sana!zile 50 zimeisha baada ya wiki 2 nimenunua zingine nimepata 34 ndani ya siku 3 zimebaki 11 sasa sielew nimeenda kwenye branch yenu Ukonga wananiletea ubabaishaji tupu wanakataa hakuna kitu kama hicho...naomba ufafanuz wa tatizo langu tafadhal
 
Kama ulikuwa na mita ya zamani sana, lazma ilikuwa haikati kulingana na matumizi yako na kama mita ilikuwa na matatizo ilikuwa haikati sawa na matumizi yako ndio maan shirika tukakubadilishia na kiweka mita mpya ambayo inakata init kutokana na matumizi yako ndugu mteja.
 
TAARIFA KWA WATEJA WETU WA MKOA WA KINONDONI KUSINI

Tunazima njia ya umeme ya Kimara, Mbezi na Kiluvua kwa dakika
tm 25 ili kufanya marekebisho ya dharura kwenye "cable" maeneo ya kilungule.

Kwa mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook Tanesco Yetu

IMETOLEWA NA:

OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU

MACHI 22, 2018
 
Muda wowote kuanzia sasa huduma itarejea
 
Mita ya zamani ilikuwa ina-stuck kwenye button za kuingiza umeme hivyo nikaomba nibadilishiwe maana baadhi ya button hazibonyezeki sasa unavyoniambia ckuelew yaan kipindi cha nyuma walishakuja Tanesco wakafanya ukaguzi kwenye eneo letu wakaniambia mita ipo sawa na matumizi sasa siwaelew!?

ndo hayo majibu yenu baada ya mimi kujipeleka kwaajili ya kubadilisha....???Tanesco hebu fanyeni vitu Technically jaman
 
Naomba kuuliza. Kwa mkoa wa pwani wilaya ya Kibaha mjini. Inachukua muda gani tangu kulipia hadi kuunganishiwa umeme
 
Asante sana nyumba na kiwanja ni za mmliki mmoja isipokua wakaaji kwenye hizo nyumba ni familia tofauti, usalama wa nyaya ni wa usalama kwani nyumba zipo karibu.

Labda ni ulize tuu kupata mita mtu unatakiwa ufanye nini na nini na inagarimu kiasi gani na kwa muda gani?
Niwatakieni tena kila jema na huduma njema.
 
Tanesco hvi niwaulize mtu akidaiwa Tsh 28000 mnamkatia umeme alafua analaipa deni ilo na 50000 fine kweli?
 
*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA*

*TANGAZO LA MABORESHO*

Shirika la Umeme (Tanesco) mkoa wa Lindi linawatangazia Wateja wake wote wa Mkoa wa Lindi kuwa litasitisha Huduma ya Umeme kwa Wateja wake kesho siku ya Jumamosi ya tarehe 24/03/2018.
*Sababu* Kupisha kazi ya kuvuta waya kwenye laini mpya ya Mahumbika-Ruangwa iliyo karibiana na laini ya zamani.
*Muda* kuanzia SAA 3 ASB mpaka SAA 12:00 jioni.
*Maeneo Yanayoathirika*: Maeneo yote yanayopata umeme kutoka laini ya Nyangao yakiwemo maeneo ya Mahumbika,Kiwalala, Nyengedi, Mtama,Nyangao pamoja na wilaya za Ruangwa na Nachingwea.

*Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza*

*Tahadhari* usiguse wala kukanyaga wala uliokatika au kulala chini

*Wasiliana nasi*kwa namba *0684692786/0752518247*
 
Kwanini umeme huwa unakatwa maeneo ya kibamba, kiluvya GOGONI, Kwa kawawa, kuanzia saa tisa leo 23/3/2018chakuna umeme giza totoro
 
Turudishieni umeme, kiluvya GOGONI, hii keroo kubwa sasa, nini ratio???!!??
 
Tuna tatizo kubwa la kukatika katika umeme kwa baadhi ya nyumba eneo la Mbezi Makabe Mtaa wa Dubai. Tunaomba mtuletee transfoma maana tatizo la low voltage ni kero kubwa.
 
Nimewahi kuuliza kuwa kuna eneo hapa singida mjni karibu kabisa na substation panaitwa kimpungua hapana umeme halafu ni mjni kwanini tanesco mmeshindwa kupeleka umeme?
 
Tuna tatizo kubwa la kukatika katika umeme kwa baadhi ya nyumba eneo la Mbezi Makabe Mtaa wa Dubai. Tunaomba mtuletee transfoma maana tatizo la low voltage ni kero kubwa.
Tumepokea taarifa kwa hatua zaidi
 
nimenunua umeme tangu sa1 jioni hamjanitumia token mpaka saiz mbona mnatutesa huu umeme kama tunaomba wakati tunatoa pesa zetu

umeme niliokuwa nautegemea umeisha na huu ni usiku tunalalagiza sababu ya uzembe wenu, hivi huwa mnafeel hizi hali zetu?? TANESCO
 
Jamani wenzenu huku hatuna umeme tangia jana saa 4 usiku. Sasa hatujui ni shida gani hiyo iliyoenelea hadi leo. Na hatukupewa tangazo lolote kuhusu katizo. Huku wakijua kuwa leo ni ibada tunataka kunyoosha nguo ili tuwahi kanisani.

Sijui inakiuwaje?
 
Tanesco tunaomba ufumbuzi kuhusu katizo la umeme Tegeta Bahari Zoo,Mwaitenda road.Umeme umekatika tangu jana.
Tunaomba namba yako ya simu mpencwa mteja na ni wengi au peke yako
 
Naomba kuuliza, hivi rimoti ya kuingizia umeme ikiharibika au kupotea unaweza kupata nyingine na kwa utaratibu gani? Nimekuja nimekuta mpangaji wangu kahama na rimoti haionekani na alikohamia sijui sasa nafanyaje kuingiza umeme?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…