jamani toka January 2018 todate umeme.amjafunga nafuatilia majibu yaleyale nguzo na waya inasikitisha kwa kweli issue nadhani ni kuescalate futher
 
Kule kibamba kunahospital kubwa sana lakini hapiti siku au katika siku moja umeme unakatika hata mara mbili au tatu na siku nyingine ni siku mzima hili mnalichukuliaje?
 
Shukrani za pekee, zimfikie Rais Mh John Joseph Pombe Maghufuli, Makamu wake Mama Yangu mpendwa Samoa Suluhu Hassan, Waziri Mkuu mh Kassim Majaliwa Kassimu, Mbunge Wangu Mh ULEGA ,Viongozi Wa wilaya na kijiji, pamoja na shirika la Umeme TANESCO.

Nimetoa shukrani hizi ,kwa viongozi hawa kwa kutoa maagizo,kusimamia na kuongoza mpaka Leo hii ninapoandika hili kijiji chetu cha MKOKOZI wilaya ya MKURANGA ,nguzo, nyaya, transfoma zimeishafungwa ,na wananchi kutakiwa kwenda kuchukua fomu Tanesco.

Mazoezi yote yamefanyika kwa ufanisi mkubwa sasa wananchi tunakisebusebu na kiroho papo tunaomba MASAVEYA nao wawe na Kasi ile walioanzisha viongozi.
 
Hivi malipo ya kuunganishiwa umeme naweza kulipia popote au ni kwenye kituo tu nilichoomba umeme? Kuunganishiwa ni Igoma Mwanza mimi nipo Sumbawanga kwa sasa.naweza kulipia Tanesco sumbawanga na nikaunganishiwa umeme Igoma?
 
nimenunua umeme jana asubuhi kupitia voda line lakini sikupata umeme mpaka kufikia usiku nikapiga sim voda waniambie kuna tatizo gani wakasema nisubiri watanijibu mwishoe wakanitumia unit TOKEN no. niingize nimejaribu kuingiza inaniambia no. USED zimetumika. hivyo nikabidi nitumie kununua umeme mwingine kwa tigo line ndio nikapata. naomba mnirudishie umeme wangu nilionunua kupitia sim no. 0743004005
 

Attachments

  • tanesco.jpg
    29.2 KB · Views: 70
Naomba kufahamu baada ya kufanya malipo na nikaambiwa site yangu inhitaji nguzo moja kwahiyo nikae baada ya miezi mitatu ndio nitaletewa nguzo na kufungiwa umeme::: sasa huu ni mwezi wa nne na risiti za malipo niliwaletea kumaanisha nimesha fanya malipo yoye crdb bank:

Naomba kujua nikae tena kwa muda gani nikiendelea ku Subir baada ya hii miezi minne naelekea watano sasa
 
Hongereni TANESCO kwa kazi nzuri, ila huku kwetu Maeneo ya Mwembe Mdogo, Amani gomvu, mwanzo mgumu, Kigamboni. Zimechimbiwa nguzo na zimeishia katikati bila kufika kwenye nyumba yoyote wakalaza nguzo zingine hadi karibia na na nyumba zetu mara wakazichukua kuuliza wakasema mradi haufiki kwetu tukauliza mbona mnatoa wakasema subirini awamu nyingine ya mradi, sasa mbona nguzo mlitandaza mwanzo kama haukuwa mradi kwanini mlitandaza bila kuchimbia leo umnazichukua? hapo mlipochimbia mbona hakuna maana kwasababu hakuna mtu anae hitaji huduma kwanini msilete hapa na si zaidi ya nguzo tatu, ila wamegoma kabisa. Tumesubiri umeme kwa muda mrefu sana ila umekuja unaishia pasipo maana. Najua nyie nu watendaji wazuri hebu tunaimba mtusaidie kwa hili maana inaonekana kama kuna watu wanapelekewa nguzo kimjuano.
 
Nataka kujua mtumiaji wa umeme wa nyumbani analipa sawa na yule anayefanya biashara?
 
Mita inakata umeme nikiwasha dryer ya nywele tu vingine haikati biashatlra ya saluni imebidi tuhame fremu
 
Kupika kwa umeme haijawahi kuwa rahisi, ila tekinolijia mpya ya induction
*sifa za majiko*
[emoji871] yanatumia umeme kidogo sana inawezekana.
[emoji871] Majiko haya yanaitwa induction electric coocker,
[emoji871] yanatumia umeme kidogo kwa asilimia 80% ukilinganisha na majiko ya kawaida. Yaan kama utatumia umeme wa Tsh. 10000/= kwa jiko la kawaida, kwa jiko la induction utatumia umeme wa 2000/= hivyo kufanya liwe na gaharama nafuu kuliko hata gass.
[emoji871] Jiko hili unachomeka popote hata kwenye extension ndogo tu na waya hautachemka, tofauti kabisa na jiko la kawaida ambapo ni lazima pawepo socket ya coocker ilounganisha moja kwa moja kutoka mainswitch.
[emoji871]Jiko hili ni touch screen hivyo kufanya matumizi yake kuwa marahisi sana,
[emoji871]ni jepesi kubeba hivyo unaweza kusafiri nalo popote kwenye bag la kawaida.
[emoji871]Kuna yanayotoa joto kwenye plate(hayachagui sufuria) , na yasiyotoa joto (yanachagua sufuria)
[emoji871]moto wake ni mkali kuliko wa gess, na jiko la umeme la kawaida, hivyo hufanya upikaji kuwa wa haraka sana hivyo husaidia kupunguza matumizi ya umeme ya muda mrefu.
[emoji871]Kama unahitaji hili jiko linapatikana kwa gharama ya ths.150,000/=tu. Tunapatikana musoma mjini, tupigie simu 0782183441. Kwa walio mikoani tutatuma jiko kwa garama za mteja, baada ya kufanya downpayment.
 
 
Nikitaka kubadilishiwa tarriff nafanyaje jamani
 
Tanesco kuna tatizo
Mkoa: morogoro
WIlaya:kilombero
Tarafa: mlimba
Kata: utengule
Kijiji: utengule
Tatizo ni matawi ya miti kuangukia kwenye waya za umeme zinazoenda nyumbani zipo chini kabisa hatari sana kwa afya
 
Hivi kwenye shirika lenu mnaongozwa na wataalamu au na wanasiasa?

Mnawezaje kupeleka umeme sehemu ambapo hakuna wateja? Mnapeleka umeme vijijini alafu kuna miji ambapo huduma zenu hazijafika kabisa.

Mnapeleka umeme sehemu ambapo ikitokea janga la moto zimamoto hawafiki.

Inakuwaje mnatumia mtaji wa wateja wakati hamuwalipi? Hapa namaanisha hivi .. ikitokea nikavuta umeme mnaniuzia nguzo lakini mkitaka kutumia hizo nguzo kwa ajili ya wateja wengine hamnilipi?

Mapungufu hayo ndiyo yaliyonifanya nitumie huduma mbadala kwa sababu huduma zenu chengachenga.
 
Nilimsikia Mh. Waziri akisema kua siku hizi kuunganishiwa umeme ni ndani ya siku 7 kwa waliolipia (http://www.mwananchi.co.tz/habari/D...sco-Arusha/1597578-4346758-nop3boz/index.html),, Mbona wengine inakaribia mwezi wa pili toka tulipie na bado hatujaunganishiwa na kila siku ukienda kwa Manager na Engineer wote wanatoa sababu?

Je kuna tatizo ambalo wananchi tulistahili kuhabarishwa mana Waziri anasema ndani ya siku 7 na Kampuni inatukalisha zaidi ya miezi miwili bila huduma?
 
Jumamosi ya Tarehe 28/02/2018 nilikuja kuunganishiwa umeme hapa kimara baruti, kama mteja mpya ni lazima umeme wa kwanza nikanunue kwenu, ila mpaka leo nilivyoenda wananiambia mita yangu bado haijasajiliwa, na siku hizi mita mpya mnatoa uniti 10 tu, si kama zamani mlikua nnatoa kianzio cha unit 50, sasa tatizo liko wapi wiki nzima hhamsajili na vi unity 10 mlivyonipa ndio vimeisha, narudi gizani tena, nn shida hamnisajili?
 
Masharti kabla ya kupewa umeme kwenye ile form,, kunamasharti yameandikwa kwa nyuma,,plz ninaomba kwa kiingereza,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…