TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tanesco, mimi nina ushauri, kumekuwa na tariff za kutumia umeme chini ya unit 75 wana lipa chini ya tshs 10,000. Baada ya hapo wanaotumia zaidi ya unit 75 laki i chini ya unit 250 mmewachanganya na wenye viwanda vidogo.
Ushauri wangu , ningeona mutenganishe tena la watumiaji wa unit chini ya 250 ili kuwapunguzia gharama watumiaji wa nyumbani. Itapendeza
 
TANESCO Dar es Salaam City, Tegeta District nguzo zinakuja lini nimesubiri toka Januari mpaka sasa tatizo ni nini?
Nashangaa kule vijijini REA wamekazana kufunga kwa spidi ya Kimondo... Mji Mkuu wa Biashara doro. Majibu please.
 
Pale Tegeta ni jipu
Ila kwa kuwa umo humu basi Shida yako itatatuliwa fasta
Nakushauri funguka zaidi, toa maelezo yako yakiwa yamenyooka mbaka msomaji wa Tanesco akiyekuwa kwenye zamu yamguse aone kweli mteja unasumbuka
Mimi najishuhudia Mwenyewe niliingia humu nikafunguka kweli kweli
basi asubuhi yake nikapigiwa simu na Tanesco makao makuu wakanifungia Umeme mafundi kutoka makao makuu na sio wale wa Tegeta pale.
 
TANESCO TANESCO Naombeni majibu
 
Ndugu zetu watoa huduma kwa nn ukienda kununua huduma ya umeme kama wa 10000 unatoa 10300 wakati stakabadhi inakuja na malipo ya10000? Kiukwel mgekuwa wengi kama mitandao ya amu ningekuwa nisha hama hatahivo naenda kwenye solar naomba ufafanuz maana habar zenu ziko vifichon hamtangazii uma
 
Mwezi uliopita umeme wa 20 elfu nilipata units 94, mwezi huu 47... najua sikuwepo kwenye taarif 0 ila hii kitu kingn kimetokea wapi tena? Msaada tafadhali
 
Wakuu,

Nina kero nataka kuiwasilisha jukwaa la TANESCO nashindwa kuingia.

Tafadhali naomba maelekezo.
 
Napenda kuwafahamisha watu wa Tanesco kuwa, kuna nguzo yenu hapa Kimara King'ongo karibu na msikitini inakariba kuanguka. Tumeshatoa taarifa hii Mbezi zaidi ya mwezi sasa, lakini hakuna ufuatiliaji au mnata ianguke, iue ndio mje? Ripoti namba ni hii 5104. tunawasubiri nguzo ikishaanguka na kuua mje mtupe pole.
 
Tanesco Moshi mko wapi? Imeripotiwa na ndugu yangu kukosekana umeme eneo la bomambuzi tangu SAA moja usiku..nyumba baadhi zina umeme nyingine hazina. Tatizo hill limekua likijirudia rudia. Na linafahamika..ila kurudisha umeme inachukua mpaka masaa 12!!! Kulikooono????
 
Tanesco wanazingua sana mita yangu imeungua toka mwezi wa 10 mwaka jana ila hadi leo haijabadilishwa
 
TANESCO mmerudisha uchumi wa watu wa Misenyi nyuma sana. Kuna transfoma imeharibika pale Kassambya na kupelekea umeme kukosa karibia mwezi sasa. Hakuna juhudi zozote zinazofanyika, kutatua tatizo hili kwa haraka kana kwamba hawa wananchi hawalipi bill zao. Na taarifa ya chini chini inasema tatizo hili kuisha mpaka July 2018. Je, hii ni sahihi kweli?
 
Kawaida mtu akiomba umeme na kukamilisha hatua zote huwa mnachukua muda gani
 
Napenda kuwafahamisha watu wa Tanesco kuwa, kuna nguzo yenu hapa Kimara King'ongo karibu na msikitini inakariba kuanguka. Tumeshatoa taarifa hii Mbezi zaidi ya mwezi sasa, lakini hakuna ufuatiliaji au mnata ianguke, iue ndio mje? Ripoti namba ni hii 5104. tunawasubiri nguzo ikishaanguka na kuua mje mtupe pole.
TANESCO TANESCO TANESCO Mpanga nguzo ianguke iue ndio mje?
 
Back
Top Bottom